Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Hawa watoto wetu wanaopata Division one za 7 points, huko ndio wanakofikiri kuna hela za fasta fasta. Wengi wamepigwa sana. Waanzilishi wa Forever Living wale wahandisi wawili, hivi wako wapi?
 
Forever Living, GNLD na the millions like that sio Utapeli (ingawa wanachama wao huenda ndio matapeli)

Hii sio Ponzi Scheme / Pyramid as kuna product....

Business Model ya Hii (multi level marketing / direct selling / network marketing) ni kuuza vitu kwa kutumia hii chain ya watu wanaojuana kwa kufanya recruiting ya wengine pia kufanya hivyo. Tatizo la hii kitu ni wahusika ku-oversell ukweli, kuwa wadanganyifu n.k. Pia kutumia membership fee za watu kama kipato as well as kulazimishana kununua product za kuuza.....

Kwahio nadhani ni busara kuangalia products je ni nzuri au ni kulazimishana kununua products hafifu ili watu wapate pesa

Kuna nyingine AVON ambayo imejikita kwenye Direct Sales ilikuwa ina-recruit sana home-workers (kina mama) wanauziana beauty products ambazo ni bei ndogo (kutokana na kwamba kampuni inapunguza marketing costs) hivyo kuwapa faida hio sales agents wake....
 
Wanaoanzisha hizo schemes huwa na ponzi schemes in mind, ika wanatumia hio MLM kama disguise tu ya kuficha ukweli, zote ni DECI tu
 
Wanaoanzisha hizo schemes huwa na ponzi schemes in mind, ika wanatumia hio MLM kama disguise tu ya kuficha ukweli, zote ni DECI tu
Ponzi Scheme ; Deci hazina product..., ni payment ya wale wanaokuja kwa kutumia pesa anazoweka aliyetoka (Hizi Pyramid Scheme mwisho wake ni kama unavyojua...

MLM, Direct Marketing, kuna Products na faida kubwa inapatikana kwenye mauzo ya vitu na sio recruitment ya watu hence hata bila mtu ku-recruit unaweza kuuza na kupata faida recruitment unapata faida tu ya commission kutokana na kumtafuta mteja na kumfanyia mentoring....

Hata Mpesa, Tigo et al Mawakala Wakuu wanakula Commission kutoka kwa Mawakala wakawaida kutoka na kazi wanayofanya ila it has nothing to do with Pyramid / Upatu....

Its a solid business model ila utendaji na wengi wanaofanya hii kitu ni matapeli (wanauza illusion na sio uhalisia) badala ya kuuza product zaidi wanauza recruitment zaidi na kudanganyana utajiri ambao haupo (ukizingatia product zao ni bei mbaya sio kulingana na uhalisia) just imagine product zao zingekuwa ni mpaka jero, jero hali ingekuwaje
 
Hata hizi ambazo wanasema wana product ni zuga tu, maana haiingii akilini eti dawa ya mswaki unauza laki 3 , au saa ya laki 1 unauza milioni 5, eti kisa ina vitu gani sijui, so hapo lengo ni wewe kulipa kiingilio cha hiyo DECI halafu serikali ikija kuuliza mnasema kwamba amenunua dawa, hajalipa kiingilio, ni uhuni tu
 
Naam product lazima iwe valuable na iwe ina market..., yaani watu waje sio ili watengeneze pesa bali waje ili wapate huduma (kama kila mtu anakuja ili awe millionaire na sio ili kutumia bidhaa basi biashara hio sio sustainable)..., Yaani watu wawepo ili ku-facilitate sales na huduma..

Ni kama vile ilivyo Dunia ya Sasa kuanzia Pension Funds mpaka mfumo wa Pesa (FIAT MONEY) vyote ni Utapeli tu wa level tofauti tofauti....

Ninakadhia upya hata nikiwa nina mfumo wangu wa biashara Direct Sales na Multi Level Marketing is a sound business model.., hapa tutofautishe a Business Model na Shady Businesses zinazotumia a certain Business Model (Kampuni kama AVON yenye kuuza cosmetics za kina mama tena nyingi more or less prices zake ni kwenye one Dollar) they are sound; as the business is built around the product ingawa sales ndio zinatumia direct selling
 
Wewe unaongelea what MLM should be. Ila mimi ninakueleza what MLM is in PRACTICE. Watu huenda hapo kutajirika kwa kulipa viingilio kwa mfumo wa kununua bidhaa kama kisingizio tu, hivyo kwa bongo hapa, kwa MLM zilizopo, zote ni Utapeli, labda wewe ndio uanzishe mpya itakayofuata misingi, ambapo hata hivyo utapata shida kushindana na hawa wanaoahidicwatu utajiri na kuwachota akili. Hata hiyo Avon, inabidi tuichunguze kama watu hawaahidiwi utajiri.
 
Muda wa mchana au jioni wanasalimiana 'goodmorning' ukiwauliza kwa nini salamu hiyo isiyolingana na muda, wanadai huyo kiongozi wao ndio alivyowaambiaga. Nikatoka nduki!
 
Ujanja ujanja tu yaan mtu kakomaa na Hizo biashara miaka zaidi ya 10 Leo hii kanunua Alphard yeye ndo anaona kayapatia
Siku hizi Caffee ziko wazi. Hazina kabisa wale wasomi wanaofundisha wenzao kuwa matajiri kwa network marketing strategies. Na reference yao kila ukiwauliza, ni Kayosaki kasema. Mburaaah
 
Huu Uzi ,ID nyingi hawapo tena, last activity ni miaka mingi sana!
Sijui wazima,au wamebadirisha ID?
 
Ningekuwa na Mamlaka ningezifuta zote hizi ndude za aina hii zisioperate nchini

Huu ni ukoloni mambosasa wa kuwatajirisha wazungu

Ni aibu tupu, watu wanafanywa misukule bila wao kujua
 
M
Mtoa mada hauna adabu
 
Daah, kweli wajinga hawataisha duniani, nipo sehemu hapa napata supu, naona kuna mtu kawaweka watu kikao anawaelekeza wajiunge na huu upuuzi wa kupanda mbegu.., daah; na inaonekana wameshaingia laini, maana wanamsikiliza kwa makini sana, na wanapeana moyo kwamba kwa hii fursa lazima wanunue magari tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…