Mnawafahamu waliompachika Dkt. Salim Ahmed Salim jina la Hezbollah katika kugombea Madaraka?

Mnawafahamu waliompachika Dkt. Salim Ahmed Salim jina la Hezbollah katika kugombea Madaraka?

Mtandao wa Jakaya ulitumika kumuangusha Dr Gharib Bilal mwaka 2000 kwny NEC ya Bara na kumuibua Karume aliekuwa wa pili kutoka mwisho kwny kura za NEC ya Znz

Jk akajigeuza akiwa Waziri wa Mambo ya nje nakumbuka akajigeuza Kampen Manager wa Aman Karume hadi nakumbuka alionekana kwny Magazeti akimfungulia Mlango wa Gari Karume wakati anaingia Dodoma Chimwaga kwny kura kuashiria ndio Mgombea wake hivyo Wanamtandao wote wampe kura na ndicho kilichotokea

Ilipofika 2005 ikawa sasa zamu ya Karume kulipa fadhila kwa kuhakikisha Salim kwanza hapati kura za Wa Znz wenzie lakin pia aoneshwe yeye ni Hizbu na Mpinga Mapinduzi na baya zaid akapakaziwa alikuwa kwny mpango uliofanikiwa wa April 7,1972 pale Kisiwandui
CCM ndani ya chama chao wanashindana kwa fitna, majungu, ulozi na fedha nje ya chama chao wanashindana kwa bunduki, marungu, visu, mapanga na mabomu ya machozi.

Politics beyond humanity.
 
Genge lilio ongoza kumpiga vita Salim mwaka 1985 liliongozwa na Getrude Mongela..
Mongela alikuwa anafata maagizo ya 'taaasis' Fulani ya kidini
Iliyosema waunguja ndo moderate muslim so bora Mwinyi.. wapemba hawaaminiki ..wengi extremists..

Salim kusoma Misri pia kulimuongezea maadui...kuna mtu mmoja hapa Maarufu sana
Aliwahi kujaribu kum link Salim na Muslim Brotherhood'..

So fitina dhidi ya Salim ziko deep sana
Taifa limekosa huduma ya Kichwa Muhimu sana.

Salim ni Kiongozi Mzuri sana Mwenye Maono makubwa na asiye na Makuu kabisa.
 
Mzee Mwinyi jana kuna sehemu pia alizungumzia Fitna alizopigwa Dr Salim japo hakumtaja Jina

Anasema 1985 wakati wanajadili jina la Mgombea Urais wa Jamhuri kutokea Upande wa Znz kulikuwa na Majina mawili;
1) Jina lake Ally Hasan Mwinyi akiwa Rais wa Znz wakati huo
2) Jina la pili ambalo amestahi kwa kutolitaja alikuwa Dr Salim Ahmed Salim ( wakati huo alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri) ambae anakiri alipigwa Jungu kuwa kila akiongea huwa hatumii ile kauli mbiu ya 'Mapinduziiii Daimaaaa' kwa hiyo ikaonekana alikuwa mpinga Mapinduzi

Fitna zimeanza kitambo
Ukiandika kitabu kilichoficha, kilichopendelea au kilichopindisha ukweli; kinabaki kuwa simulizi.
 
Mzee mwinyi kwenye kitabu chake kaandika kuwa kwa kuwa yeye Muislam eti walikuwa wanamtuhum kuwa alikuwa anateua viongoz kwa upendeleo wa kidini,kumbe wagalatia drama hizi za fitna za udini hawakuanza leo hawa jamaa
Cha ajabu na kushangaza wao wanajifanya sio wadini na wala hawalalamikii udini.

Ni hatari sana hawa wanafki.
 
Jana wakati inasimuliwa historia ya maisha ya Mzee Ali Hassan Mwinyi kwenye maisha yake ya uongozi na Professor Mukandala kipengele hiki alikizungumzia,ni kinani hao tuwafahamu kwa mlio na kumbukumbu mpaka ilipelekea Mzee Mwinyi atengeneze nafasi ya naibu waziri mkuu na nafasi hizo na ile ya wizara ya ulinzi kukabidhiwa Dr Salim?

Kwangu mimi nakumbuka nikiwa na utimamu wa kufuatilia siasa nchini hali hii ilijitokeza pia wakati hayati Mzee Mkapa anamaliza muda wake ,fimbo hii pia ilitumika kumchapiaDr Salim tena kwenye kinyang'anyiro cha awamu ya nne
Cha kustaajabisha Dr Salim sikuwahi kwenye maisha yangu kumskia akilalamika sehemu yoyote ile ,bali alibaki kimya kwenye kigoda cha Mwalimu,bila ya kuwa na nongwa .nionavyo Maisha ya Mzee Mwinyi na Dr Salim ni kama yanashabihiana kwa namna moja ama nyingine
Kuweka rekodi sawa! Mzee Salim aliwahi kuhoji suala hili na alionyeshwa kwenye TV. Hii ni alipojaribu nafasi ya urais kwa mara ya pili wakati awamu aliyoshinda JK.
 
Uko sahihi

Moja ya udhaifu wa Mzee Mwinyi ni kutopenda kuingia kwenye malumbano na Mtu ndio sababu hata Waziri aliemdhulumu Vifaa vyake vya Ujenzi miaka zaidu ya 38 kaona amsitiri maana akimtaja itakuwa zogo na nongwa kwake na watu wake
Ukiandika kitabu kilichoficha, kilichopendelea au kilichopindisha ukweli; kinabaki kuwa simulizi.
 
Salim Ahmed Salem kwa bahati mbaya amekuwa anaumwa muda mrefu, natamani angeandika kitabu maana na uhakika ana mengi sana ya kusema na watu wangejifunza. Mimi simjui binafsi lakini anaonekana alikuwa mtu mzuri maana waswahili wanasema mti mzuri ndio hupigwa mawe na kapigwa sana maishani mwake.
 
Salim alipewa ubalozi na Nyerere wakati ana miaka 18 tu..
Alilelewa na Nyerere..
Alijongezea sifa alipokuwa balozi wa Tz UN
Aliiongoza wajumbe wa UN kuipa China
Permanent membership..
USA walimchukia milele..
Wachina hadi wakasema Nyerere nabii wa Africa...Salim alimfanya Nyerere awe so proud..
Usisahau pia Salim katika nyazifa zote hakuwahi kupata kashfa ya kupiga hela yeyote na alikuwa na nafasi ya kujitajirisha.
Hata Bakhresa inasemekana alisaidiwa na Salim kuweza kupata nafasi ya biashara
Enzi hizo kuagiza kitu Ulaya sio kitu rahisi..
Alikuwa na miaka 23 sio 18

Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
 
Niliwahi mjibu mtu humu 19/12/2017

Mwinyi hakumgeuka Dr salim
Inaelezwa kuwa mwaka 1985 wakati wa kumtafuta mrithi wa mwalimu.

Inasemekena mwalimu nyerere alikuwa akimtaka sana Dr.salim ila mwalimu aliogopa fitna za makundi hasimu ya wanamstari(frontliners) na wale wagombozi (linerators) hii ilipelekea mwalimu nyerere kusuka njama.

Mwalimu nyerere alimfuata Rais Mwinyi wakati huo alikuwa ni Rais wa Zanzibar akamwambia Ali ntakupendekeza kuwa mrithi wangu kwa urais wa bara ila wewe ukatae..inasemekana Ali (Mwinyi) alikubali lakini kabla ya kikao kuanza Ali(Mwinyi) alimfuata sheikh Thabit Kombo(mshauri mkuu wa mwalimu Nyerere kuhusu maswala ya Zanzibar na huyu ndo alimpendekeza Mwinyi kuwa rais wa Zanzibar)

Akamwambia sheikh Thabit mwalimu kanambia "anipendekeze kuwa mrithi wake lakini akasema niikatae nafasi".
Sheikh Thabit akamwambia "ataka kukufanya punda wa dobi eeee, usikubali yeye akishakupendekeza kwenye mkutano wewe kubali"

Basi baadae kikao kikaanza huku mwalimu hajui hili wala lile, ana confidence kuwa atampendekeza Ali(Mwinyi) kuwa mrithi wake alafu Mwinyi atakaa basi kwake itakuwa rahisi kupendekeza jina la Dr. Salim.

Basi ghafla mwalimu akapendekeza jina la Rais wa Zanzibar Mwinyi kuwa mrithi wake JMT kwa kujiamini kabisa.
Ilipofika zamu ya kuzungumza Mwinyi AKAKUBALI dah mwalimu akatahayari hakuamini macho yake aliona kama Mwinyi kamgeuka.

Kwa hiyo mchezo ukaisha pale pale

Mwalimu 0-3 Mwinyi na makundi hasimu ya Dr. Salim.
 
Wakati wa kumtafuta mrithi wa Rais Jumbe kulikuwa na makundi mawili mahasimu.

Kundi la kwanza wakijiita Frontliners(Wanamstari) hili lilikuwa kundi la vijana wa wakati huo linalotaka mabadiliko na nafasi ya Uongozi kushikwa na vijana kundi hili likijumuisha vijana wa wakati huo Dr. Salmin Amour, Maalim Seif Sharif Hamad, Seif Khatib na wengineo lilikuwa linapinga wahafidhina waasisi wa mapinduzi.

Kundi la pili likiitwa Liberators(Wakombozi wa Mapinduzi) lilikuwa kundi la kihafidhina(Conservative) lilikuwa na wajumbe wazee wa makamo wakati huo Wakina kanali Seif Bakari,Meja Gen Abdallah Natepe,Brig Gen Ramadhan Fakhi nk
Kundi hili ndio lilikuwa halimtaki Dr. Salim licha ya mwalimu kulisihi sana
Ilibidi Mwalimu akutane na wajumbe kutoka Zanzibar mchana ule ili kuwashinikiza wamkubali Dr. Salim, wakakataa kata kata wakawa wanasimamia hoja kuu tatu

1.Dr. Salim hatokani na kizazi cha kimapinduzi, hana damu ya kimapinduzi

2.Asili ya Dr. Salim ni mwarabu na wao wakombozi waliikomboa nchi toka kwa waarabu kwa hiyo hawawezi mkabidhi tena mtu mwenye asili ya kiarabu.

3.Dr. Salim ni hizbu(Nationalistic Party)
Kwa kuwa Dr Salim aliwahi kuwa hizbu kabla ya kujiunga na ASP
Hizbu ndio chama kilichotolewa na kupinduliwa kikiongozwa na Sheikh Mohammed Shamte.

Dr. Salim alisakamwa sana. Nyakati za mapumziko ya kikao alimfuata Mwalimu huku akilia na kutokwa na machozi akamuuliza Mwalimu ".. Tatizo ni Asili yangu, ndio maana napewa shutuma zote hizi???... "

Kumbuka huyu ndiye aliyekuwa chaguo la Mwalimu ilibidi ampooze na Mwalimu akashindwa na kundi la Wakombozi kumfanya Dr. Salim kuwa rais wa zanzibar ile January 1984.
 
Mzee Mwinyi jana kuna sehemu pia alizungumzia Fitna alizopigwa Dr Salim japo hakumtaja Jina

Anasema 1985 wakati wanajadili jina la Mgombea Urais wa Jamhuri kutokea Upande wa Znz kulikuwa na Majina mawili;
1) Jina lake Ally Hasan Mwinyi akiwa Rais wa Znz wakati huo
2) Jina la pili ambalo amestahi kwa kutolitaja alikuwa Dr Salim Ahmed Salim ( wakati huo alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri) ambae anakiri alipigwa Jungu kuwa kila akiongea huwa hatumii ile kauli mbiu ya 'Mapinduziiii Daimaaaa' kwa hiyo ikaonekana alikuwa mpinga Mapinduzi

Fitna zimeanza kitambo
Hapana hujui, huyo alikuwa ni Maalim Seif
 
Mzee mwinyi kwenye kitabu chake kaandika kuwa kwa kuwa yeye Muislam eti walikuwa wanamtuhum kuwa alikuwa anateua viongoz kwa upendeleo wa kidini,kumbe wagalatia drama hizi za fitna za udini hawakuanza leo hawa jamaa
Mkuu umetoka kushindilia na kubughia msosi usiku kucha kama fisi mlafi. Itakuwaje njaa imekubamba asubuhi hii uanaanza kuleta porojo jamvini?
 
Mtandao wa Jakaya ulitumika kumuangusha Dr Gharib Bilal mwaka 2000 kwny NEC ya Bara na kumuibua Karume aliekuwa wa pili kutoka mwisho kwny kura za NEC ya Znz

Jk akajigeuza akiwa Waziri wa Mambo ya nje nakumbuka akajigeuza Kampen Manager wa Aman Karume hadi nakumbuka alionekana kwny Magazeti akimfungulia Mlango wa Gari Karume wakati anaingia Dodoma Chimwaga kwny kura kuashiria ndio Mgombea wake hivyo Wanamtandao wote wampe kura na ndicho kilichotokea

Ilipofika 2005 ikawa sasa zamu ya Karume kulipa fadhila kwa kuhakikisha Salim kwanza hapati kura za Wa Znz wenzie lakin pia aoneshwe yeye ni Hizbu na Mpinga Mapinduzi na baya zaid akapakaziwa alikuwa kwny mpango uliofanikiwa wa April 7,1972 pale Kisiwandui
Halafu JK Jana nilimuona Kama hakuwa sawa kifikra [emoji1]

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom