Mnawafahamu waliompachika Dkt. Salim Ahmed Salim jina la Hezbollah katika kugombea Madaraka?

CCM ndani ya chama chao wanashindana kwa fitna, majungu, ulozi na fedha nje ya chama chao wanashindana kwa bunduki, marungu, visu, mapanga na mabomu ya machozi.

Politics beyond humanity.
 
Taifa limekosa huduma ya Kichwa Muhimu sana.

Salim ni Kiongozi Mzuri sana Mwenye Maono makubwa na asiye na Makuu kabisa.
 
Ukiandika kitabu kilichoficha, kilichopendelea au kilichopindisha ukweli; kinabaki kuwa simulizi.
 
Mzee mwinyi kwenye kitabu chake kaandika kuwa kwa kuwa yeye Muislam eti walikuwa wanamtuhum kuwa alikuwa anateua viongoz kwa upendeleo wa kidini,kumbe wagalatia drama hizi za fitna za udini hawakuanza leo hawa jamaa
Cha ajabu na kushangaza wao wanajifanya sio wadini na wala hawalalamikii udini.

Ni hatari sana hawa wanafki.
 
Kuweka rekodi sawa! Mzee Salim aliwahi kuhoji suala hili na alionyeshwa kwenye TV. Hii ni alipojaribu nafasi ya urais kwa mara ya pili wakati awamu aliyoshinda JK.
 
Uko sahihi

Moja ya udhaifu wa Mzee Mwinyi ni kutopenda kuingia kwenye malumbano na Mtu ndio sababu hata Waziri aliemdhulumu Vifaa vyake vya Ujenzi miaka zaidu ya 38 kaona amsitiri maana akimtaja itakuwa zogo na nongwa kwake na watu wake
Ukiandika kitabu kilichoficha, kilichopendelea au kilichopindisha ukweli; kinabaki kuwa simulizi.
 
Kuweka rekodi sawa! Mzee Salim aliwahi kuhoji suala hili na alionyeshwa kwenye TV. Hii ni alipojaribu nafasi ya uraisi kwa mara ya pili wakati awamu aliyoshinda JK.
Nakumbuka bwashee!
 
Salim Ahmed Salem kwa bahati mbaya amekuwa anaumwa muda mrefu, natamani angeandika kitabu maana na uhakika ana mengi sana ya kusema na watu wangejifunza. Mimi simjui binafsi lakini anaonekana alikuwa mtu mzuri maana waswahili wanasema mti mzuri ndio hupigwa mawe na kapigwa sana maishani mwake.
 
Alikuwa na miaka 23 sio 18

Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
 
Niliwahi mjibu mtu humu 19/12/2017


Mwinyi hakumgeuka Dr salim
Inaelezwa kuwa mwaka 1985 wakati wa kumtafuta mrithi wa mwalimu.

Inasemekena mwalimu nyerere alikuwa akimtaka sana Dr.salim ila mwalimu aliogopa fitna za makundi hasimu ya wanamstari(frontliners) na wale wagombozi (linerators) hii ilipelekea mwalimu nyerere kusuka njama.

Mwalimu nyerere alimfuata Rais Mwinyi wakati huo alikuwa ni Rais wa Zanzibar akamwambia Ali ntakupendekeza kuwa mrithi wangu kwa urais wa bara ila wewe ukatae..inasemekana Ali (Mwinyi) alikubali lakini kabla ya kikao kuanza Ali(Mwinyi) alimfuata sheikh Thabit Kombo(mshauri mkuu wa mwalimu Nyerere kuhusu maswala ya Zanzibar na huyu ndo alimpendekeza Mwinyi kuwa rais wa Zanzibar)

Akamwambia sheikh Thabit mwalimu kanambia "anipendekeze kuwa mrithi wake lakini akasema niikatae nafasi".
Sheikh Thabit akamwambia "ataka kukufanya punda wa dobi eeee, usikubali yeye akishakupendekeza kwenye mkutano wewe kubali"

Basi baadae kikao kikaanza huku mwalimu hajui hili wala lile, ana confidence kuwa atampendekeza Ali(Mwinyi) kuwa mrithi wake alafu Mwinyi atakaa basi kwake itakuwa rahisi kupendekeza jina la Dr. Salim.

Basi ghafla mwalimu akapendekeza jina la Rais wa Zanzibar Mwinyi kuwa mrithi wake JMT kwa kujiamini kabisa.
Ilipofika zamu ya kuzungumza Mwinyi AKAKUBALI dah mwalimu akatahayari hakuamini macho yake aliona kama Mwinyi kamgeuka.

Kwa hiyo mchezo ukaisha pale pale

Mwalimu 0-3 Mwinyi na makundi hasimu ya Dr. Salim.
 
Wakati wa kumtafuta mrithi wa Rais Jumbe kulikuwa na makundi mawili mahasimu.

Kundi la kwanza wakijiita Frontliners(Wanamstari) hili lilikuwa kundi la vijana wa wakati huo linalotaka mabadiliko na nafasi ya Uongozi kushikwa na vijana kundi hili likijumuisha vijana wa wakati huo Dr. Salmin Amour, Maalim Seif Sharif Hamad, Seif Khatib na wengineo lilikuwa linapinga wahafidhina waasisi wa mapinduzi.

Kundi la pili likiitwa Liberators(Wakombozi wa Mapinduzi) lilikuwa kundi la kihafidhina(Conservative) lilikuwa na wajumbe wazee wa makamo wakati huo Wakina kanali Seif Bakari,Meja Gen Abdallah Natepe,Brig Gen Ramadhan Fakhi nk
Kundi hili ndio lilikuwa halimtaki Dr. Salim licha ya mwalimu kulisihi sana
Ilibidi Mwalimu akutane na wajumbe kutoka Zanzibar mchana ule ili kuwashinikiza wamkubali Dr. Salim, wakakataa kata kata wakawa wanasimamia hoja kuu tatu

1.Dr. Salim hatokani na kizazi cha kimapinduzi, hana damu ya kimapinduzi

2.Asili ya Dr. Salim ni mwarabu na wao wakombozi waliikomboa nchi toka kwa waarabu kwa hiyo hawawezi mkabidhi tena mtu mwenye asili ya kiarabu.

3.Dr. Salim ni hizbu(Nationalistic Party)
Kwa kuwa Dr Salim aliwahi kuwa hizbu kabla ya kujiunga na ASP
Hizbu ndio chama kilichotolewa na kupinduliwa kikiongozwa na Sheikh Mohammed Shamte.

Dr. Salim alisakamwa sana. Nyakati za mapumziko ya kikao alimfuata Mwalimu huku akilia na kutokwa na machozi akamuuliza Mwalimu ".. Tatizo ni Asili yangu, ndio maana napewa shutuma zote hizi???... "

Kumbuka huyu ndiye aliyekuwa chaguo la Mwalimu ilibidi ampooze na Mwalimu akashindwa na kundi la Wakombozi kumfanya Dr. Salim kuwa rais wa zanzibar ile January 1984.
 
Hapana hujui, huyo alikuwa ni Maalim Seif
 
Mzee mwinyi kwenye kitabu chake kaandika kuwa kwa kuwa yeye Muislam eti walikuwa wanamtuhum kuwa alikuwa anateua viongoz kwa upendeleo wa kidini,kumbe wagalatia drama hizi za fitna za udini hawakuanza leo hawa jamaa
Mkuu umetoka kushindilia na kubughia msosi usiku kucha kama fisi mlafi. Itakuwaje njaa imekubamba asubuhi hii uanaanza kuleta porojo jamvini?
 
Halafu JK Jana nilimuona Kama hakuwa sawa kifikra [emoji1]

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…