Mnawafahamu waliompachika Dkt. Salim Ahmed Salim jina la Hezbollah katika kugombea Madaraka?

Huo ndio ukweli, mtu dhaifu katika siasa anabaki kulalamika anapigwa fitna na majungu. Siasa kupambana kweli.
 
Vijiji vya Ujamaa vilikuwa 1972 wakati huo Kambona kishavurugana na Nyerere miaka kadhaa, nadhan umechanganya na Azimio la Arusha

Kawawa alikuwa Yes Sir baada ya makubaliano sio kuwa hakuwa na mawazo binafsi kwny mijadala
ahaa
 
Hapana kura zilipigwa kwenye halmashauri kuu mwinyi akashinda
Hawakupiga kura

Halmashauri kuu iliweka vigezo 13 ili kumpata mrithi wa Mwalimu.

Wagombea walikuwa 3
1.Ally Hassan Mwinyi(Rais wa SMZ)
2.Rashid Mfaume Kawawa
3.Dr Salim Ahmed Salim

Mzee kawawa alijitoa mwanzoni kabisa na akasema jina lake lisijadiliwe ana akajenga hoja 2 kuu
1.Yeye na Mwalimu walionekana kama mapacha hivyo kama angelirithi mikoba ya Mwalimu watu wasingelihisi mabadiliko yoyote akapendekeza aje mtu mpya na fikra mpya.
2. Sababu za kiafya
Halmashauri kuu ikamkubalia na kuondoa jina lake.
Majina yakabaki mawili.

Aliyefuatwa kujadiliwa ni Ally Hassan mwinyi ambaye wajumbe walionekana kumtaka sana wakiongozwa na wahafidhin( Liberators wakombozi) kutoka Zanzibar kazi yao kuu ilikuwa ni kuhakikisha mu hizbu Dr. Salim ambaye ni chaguo la Mwalimu kuwa hawi Rais wa Jamhuri.
Hii ilipelekea Mzee Mwinyi kupata vigezo karibia vyote 13.
Na hapa Mwalimu akasimama akasema "Kama ni hivyo haya...hakuna haja ya kujadili jina la tatu, mgombea wetu ni Ally Hassan Mwinyi Rais wa SMZ..."

NB
Kwahiyo Dr. Salim hakujadiliwa kwenye kikao wala hakukupigwa kura.
 
Sheikh adui wetu ni wanafiq waislamu wenzetu...tusijidanganye
Mzee mwinyi kwenye kitabu chake kaandika kuwa kwa kuwa yeye Muislam eti walikuwa wanamtuhum kuwa alikuwa anateua viongoz kwa upendeleo wa kidini,kumbe wagalatia drama hizi za fitna za udini hawakuanza leo hawa jamaa
 
Kwa sasa inaonekana kana masikhara, lakini tusisahahu hii SMZ ni serkali ya mapinduzi (mapindizi ya kikwelikweli, yale ya chama cha mapinduzi). Ni watu walimwaga damu kujikomboa. Mwaka huu viongozi wa mapinduzi at least 6 walikuwa hai, wakiwamo Saidi Natepe, Ramadhani Haji, Seif Bakari na Ali Anmeir. There is no way wangemwachia Mwarabu atawale tena, no way. Watakuwa walikumbuka mwenzao Karume alivyouliwa 1972. Iwapo utafikiria vinginevyo hujui maana ya mapinduzi,
 
Wanasema Nyerere aliwahi kuwapenda viongozi 2 tu, Sokoine na Salim. Mliokuwepo kipindi hicho tuambieni ukweli kuhusiana na hili.
Nyerere aliwaamini ndio mawaziri wakuu vijana zaidi kutokea kwa kifupi Nyerere aliandaa viongozi wazuri kiasi walipoenda kimataifa walifanya vizuri sana kama Salim, Mahiga, Mwakawago
 
Halafu kwa nini Karume huwa anazomewa kila akiwa kwenye haraiki ya wazanzibar
 
So Salim was the best president we never had?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Salim alikuwa kijana Sana wakati anaanza siasa..
Kumbuka anaenda kuwa Balozi Misri ana miaka 18 Tu ndo akaenda kusoma huko huko..

Alipaswa kuandika historia yake..
Alikuwa anapigwa vita na wengi
Duuuh 18 yrs anakuwa balozi wa nchi? Heeeeh mbna ilikua hatareeeh.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Aiseeeeeh hii nchi ina historia ndefu hivi kumbe? Duuuuh

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hatareeeeh sana.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Maskini baba wa watu sijui alikosa nn huyo SALIM.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Ambalo liko dhahiri ni hili, Mwinyi hakuwa chaguo la Mwalimu hata kidogo na haya yalikuwa wazi kabisa. Mwinyi ni kati ya marais ambao hawakuwahi kufurahia uraisi wao, Mwalimu kila alichofanya mwinyi alipinga ama kumsakama. Kuna za chini chini kwamba kuna kipindi Mwinyi alichoka na kashfa za Mwalimu akataka kumweka detention ama kumuua. Ni bahati mbaya kwamba mpango ulivuja na mwalimu akamuendea Mwinyi na kumuabia 'nasikia unataka kuniua, haya nimalize hapa hapa'
 
Kundi la watu wa siasa chafu za maji taka, kundi la 'do whatever it takes'. Mkwere ni mahiri sana kwenye siasa hizi, Karume(mtu wa bapa) yeye alikuwa analipa 'fadhila' kwa kuwa anakumbuka bila ya Mkwere asingeukwaa urias wa Zenji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…