Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
MNEC TOUFIQ TURKY AAHIDI KUENDELEZA UFADHILI WA WALIMU WA MADRASA
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Ndugu Toufiq Salim Turky amekutana na viongozi mbalimbali wa Misikiti na Walimu wa Madrasa katika Jimbo la Mpendae ambapo amewatoa wasiwasi kwa kuahidi kuwa ataendelea kuwa pamoja nao katika kuwawezesha shughuli za mafunzo kama alivyokuwa akifanya hapo awali
Itakumbukwa kuwa, Ndugu Toufiq Salim Turky wakati wa Uhai wa Bunge la 12 (2020-2025), Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Mpendae na wakati wote huo alikuwa akifanya ufadhili kwa kuwalipa mishahara walimu wa Madrasa katika Misikiti 27 na Vyuo 42 ambapo alijitolea kuwalipa Shilingi 50,000 mpaka Shilingi 200,000 kutegemea na ukubwa wa Msikiti na Chuo.
MNEC Toufiq Salim Turky amesema kuwa ataendelea kutoa huduma kwa wananchi kwani kufanya hivyo kwake ni kitu anachokipenda ana amerithishwa na baba yake mzazi na pia anatamani kuwarithisha watoto wake wawe na wito huo wa kuendelea kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Mpendae.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya Walimu wa Madrasa na viongozi wa Misikiti wameonyesha kufurahishwa sana na Kitendo cha Ndugu Toufiq Salim Turky kuendelea kutoa ufadhili kwenye Misikiti na Madrasa.

Attachments
-
VID-20250817-WA0008.mp417 MB
-
IMG-20250818-WA0002.jpg64.9 KB · Views: 37 -
IMG-20250818-WA0001.jpg96.9 KB · Views: 36 -
IMG-20250817-WA0011.jpg64.9 KB · Views: 35 -
IMG-20250817-WA0009.jpg79.1 KB · Views: 27 -
VID-20250817-WA0007.mp46.2 MB
-
VID-20250817-WA0006.mp48.6 MB
-
VID-20250817-WA0005.mp45.5 MB
-
VID-20250817-WA0004.mp44 MB