Mngeomba msaada kwa CDF, angewapa makomando, wangeonyesha uwezo wao na kuokoa wahanga wa ajali ya ndege

Mngeomba msaada kwa CDF, angewapa makomando, wangeonyesha uwezo wao na kuokoa wahanga wa ajali ya ndege

Mwl Athumani Ramadhani

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2022
Posts
1,280
Reaction score
2,522
Nampa pole Waziri MKUU na Rais

KWA fedheha na aibu tulioipata kama Taifa kwenye hii ajali ya ndege, mengi yameandikwa lakini NIMEONA niwape mbadala kwa siku za mbeleni kama yakitokea kama Hayo tulioyaona!

Naamini kama Waziri MKUU angemuomba CDF amsaidie kwenye hili nadhani tungeshuhudia tukio la kujivunia kama Taifa na historia kuandikwa, CDF angetoa order KWA special force kikosi cha dharura na kingejitosa ipasavyo na leo hii wahanga wangeokolewa na sio wavuvi na wasamaria ambao wamejitosa na kuhatarisha Maisha yao kwa ajili ya kuokoa wapendwa wao na kuleta aibu KWA Taifa kwamba hatukujiandaa na majanga ya kitaifa kama haya!

Tumeonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye hili na tunapaswa kuchutama na kuja na Mpango kazi kabambe ambao ungetusaisaidia kama Taifa!

Makomando kwa uwezo wao ambao tumeushuhudia kwenye maadhimisho ya KILA mwaka ya muungano nadhani wangeweza kuokoa wahanga ndani ya Muda mfupi kuliko sintofahamu ambayo imejitokeza!

Jeshi la wananchi ndio tumaini pekee la mwisho pale mambo yanapokuwa nje ya uwezo wetu!!

Mungu ibariki nchi YANGU TANZANIA
 
Sio kila mtu anapaswa kuanzisha thread humu. Pelekeni upuuzi wenu huko mbele nimechoka na kelele zenu za kijinga!
KELELE ZETU zinachangia uchumi KWA kununua bando na kujenga Taifa letu!Lazima tuandike Sana zile sio mbuzi ni watu tena wajenzi wa Taifa tumepoteza!

Lazima tuishauri Serikali pale tunapoona nyufa za kimawasiliano zinazozaa majanga kama hizi!!
 
ni kweli makomando wanaweza hii shughuli! tunao special force wako njema sana!

tatizo lipo kwenye siku ya kufa nyani! Africa bado sana kwenye kujiandaa na majanga! bado sana sana
 
Hawana msaada wowote hapa Tanzania!! Kwamba wao ni mpaka waombwe ndo wakaokoe!! Inashangaza sana!!

Basi hawana msaada kwa nchi kama hawajui dharura!!
 
Lingewashwa lindenge lile Rais anapenda kutembelea, dakika sufuri sema hatujawa na task force ya Kitaifa KWENYE Mambo ya dharula
Yet wangechelewa aisee na uhakika Bukoba kuna vikosi vya jeshi na zimamoto ila pengine not specialized kwenye maji
 
Bora hawakwenda hao makomandoo maana ingekuwa aibu. Tunajua udhaifu wa taasisi zetu za umma. Hao wako vizuri kwenye kupambana na raia wasio na silaha. Matukio halisi ni aibu tupu.
 
Wakati huo huyo Waziri mkuu anamtafuta CDF, maji yaliyokuwa yanaingiia kwenye Ndege yanasubiri tu.. Wakati mwingine lazima tukumbuke kuwa Desperate times needs Desperate measures.

Kilichofanyika ndio kilikuwa the best option kwa wakati huo... Hakuna solution nyingine yoyote ambayo ingezidi solution ya Dogo Majaliwa kutokana na mazingira na uharaka wa tukio lenyewe..
 
Back
Top Bottom