Mnielimishe: Ni kitu gani haswa Nyerere alikitaka kwenye Muungano, maana nachoona tunapigwa wazi wazi

Mnielimishe: Ni kitu gani haswa Nyerere alikitaka kwenye Muungano, maana nachoona tunapigwa wazi wazi

Eneo lilibaki upande mashariki watakuwa na haki ya kumiliki eneo la ukubwa wa nm 12 ambazo zitakuwa eneo lao rasmi likijumuisha na anga, eneo lingine la nm 24 za ziada litakuwa la kwao lakini halitajumuisha anga. Eneo lingine lote la bahari linalobaki ni maji ya kimataifa ambapo halitamilikiwa na yeyote, hivyo ndivyo ilivyo kwetu na nchi nyingine zote kwa sehemu zisizopakana na visiwa.
Sawa
 
Zanzibar ikiwa huru itarudi kwa Mwaraabu fasta. Baadaye watataka mikoa yote ya Pwani. Utumwa kwa weusi utarudi, ikumbukwe Zanzibar ilikuwa Soko kuu la watumwa.

Usalama kwa Tanganyika utakuwa mgumu. Pia Nyerere alikuwa na maono ya kuiunganisha Afrika yote ukianzia na ukanda wako. Alitaka Kenya, Uganda, Tanzania ziwe kitu kimoja pamoja na Zanzibar.
Wacha ujinga, kaka. Utumwa hautarudi. Wakati ule ilienea kwa sababu watu wa bara walitaka kuuza wafungwa wao, walifurahi kupata wateja Zanzibar.
 
Kwanza fahamu sheria za kimataifa zinataka meli zote zisizo za kijeshi au kijasusi kuruhusiwa kupita bila bugdha hata katika nm 36 zilizo ndani ya umiliki wa taifa linalopakana na bahari halafu hizo km 58 kwa upande wetu hazitatutosha kupita katika hako kasehemu kadogo hadi twende kwenye hizo zao 58?

Eneo la bahari ya Tanzani ni kubwa sana na matumizi yake mpaka sasa ni kiduchu tu, umewahi kufikiria ncho kubwa kama Ethiopia, Congo na Uganda maisha yanaendaje bila bahari?!
Na eneo linalobaki nje ya hizo km?

KWANI ENEO LA BAHARI ALILONALO ZANZIBAR UNALIFAHAMU? KAMA NI NCHI IKISEMA MELI ZA NCHI YA TZ ZISIPITE ENEO LETU UNAFAHAMU TUTAATHIRIKA VIPI? MWISHO WAO WANA UWEZO WA KIJESHI KULINDA ENEO LAO LILILOUNGANA NA SISI NA MAHARAMIA NA WAUZA MADAWA?

Mkuu Yoda, Majibu yake wala usinipe wewe hitimisha tu kwa namna unavyopenda wewe.
 
Wacha ujinga, kaka. Utumwa hautarudi. Wakati ule ilienea kwa sababu watu wa bara walitaka kuuza wafungwa wao, walifurahi kupata wateja Zanzibar.

Vipi ndugu zetu, dada zetu wanapata treatment gani hapo Saudi Arabia. Mamilioni ya wanaume walihasiwa. Weusi hapo Zenji walikuwa second class citizens.

Kwanini unafikiri mapinduzi yalitokea? kwanini unafikiri Karume alilazimisha wanawake waarabu waolewe kwa nguvu na Weusi? Yeye mwenyewe alifanya hivyo. Unafikiri naye alikuwa mjinga.
 
View attachment 2029458

Naombeni wenye jicho la ziada mnitoe ujinga maana huu ujinga nilionao ndio unanifanya niwe napatwa na hasira kwa maono mafupi yanayonifanga nione Zanzibar inatunyonya

Kwa upeo wangu mfupi najionea mambo haya, Naombeni mnipe maarifa, huenda mtazamo wangu haupo sawa.

Mambo ya huku bara lazima yawe na mchanganyiko wa mtanganyika na mzanzibari kuanzia ajira, uongozi, jeshini, mahakama, n.k kwenye uongozi kukiwa na msaidizi wa bara basi mkuu inabidi awe wa Zanzibar, kwenye ajira nako katika kila ajira 100 basi 21 za wazanzibar, jeshini huko wapo wengi pia sana sana polisi na jwtz, ila sasa huko kwao mambo yao ni ya wao hawataki mchanganyiko, hapa Tanganyika tunanufaika kivipi????

Ukija kwenye ardhi, wazanzibari kibao wanamiliki mashamba makubwa na viwanja huku bara lakini mtanganyika harusiwi kufanya hivyo, Je tunanufaika kivipi??

Ukija kwenye Power, hakuna kabila wala kundi linalowafikia wala kuwasogelea wazanzibar, yani si mchaga wala msukuma wala kabila lolote unaloweza kulifikiria, hawa wenzetu wapo wachache lakini wamesambazwa si mchezo kwenye vyeo vizito. kuna mawaziri, wakuu wamikoa, wakuu wa wilaya, ma rpc, vyeo vikubwa jwtz, mabalozi wa nchi za nje, majaji wa mahakama, maprofesa vyuoni, waajiriwa kwenye mashirika yenye mishahara minono kama bandarini, Bot, Tanapa, Tra, Nssf, n.k hii ni kwasababu muungano unahitaji mchanganyiko wa pande mbili.

Mtanganyika hana nafasi kwenye serikali ya zanzibar kuanzia kwenye uongozi, ajira, mahakama, n.k Wana serikali yao kwajili yao kuanzia uraisi, makamu wa raisi, spika wa bunge, n.k hawa inabidi wawe wa zanzibar. pia wana taasisi zao kama Zff ambayo ni kama tff ya huku, Zrb ambayo ni kama Tra ya huku, Zssf ambayo ni kama Nssf ya huku, Jku ambayo ni kama jkt ya huku, yani taasisi zipo kibao kwakweli, hizo taasisi zinatoa ajira kwa wazanzibar tu, mtu wa Tanganyika huna sifa, lakini cha ajabu mzanzibar anaweza kupata ajira pande mbili za bara na huko kwao, vya bara ni vya wote ila vya zanzibar ni vya wao pekee, Patamu happ aisee [emoji848][emoji848]

Tukubali kwamba wazanzibar WALITUZIDI AKILI na sasa wanafaidi dili nono la muungano

Kwa upeo wangu nimegundua Karume alimzidi akili Nyerere, Alipoona kwamba Nyerere anambembeleza sana kuwe na muungano, Karume akatumia nafasi hii kumbana Nyerere aipe Zanzibar upendeleo kama huu tunaouona ama sivyo hakuna muungano, Pia akaongezea kipengere kwamba endapo kukiwa na muungano basi Zanzibar iwe kwajili ya Zanzibar lakini Tanganyika ibanwe iwe kwajili ya wote, Kwa lugha nyepesi "changu ni changu ila chako tutagawana" matokeo yake leo Tanganyika tunashuhudia inapigwa nje ndani na wazanzibar, na pia haya malalamiko ya wazanzibar kunyonywa yaliwekwa kimkakati ili iwe silaha kwa Zanzibar kutojitapa kwamba wametuzidi akili lakini pia haya malalamiko huwadanganya watanganyika wadhani kwamba Zanzibar ni kama mkoa wake kumbe kiukweli wanapigwa [emoji23][emoji23]
Wao ndo hujiona kuwa wanadhulumiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suala la maharamia na dawa za kulevya utalinda katika km zako 58 ulizopakana nao na huko kwengine kusipopakana na sehemu yoyote lakini pia kuna wakati hata sisi tuliomba ushirikiano kutoka Africa ya Kusini kupambana na uvuvi harama katika bahari kuu, suala la mataifa kusaidiwa, kusaidiana na kushirikiana katika ulinzi wa eneo la bahari ni la kawaida sana duniani kote.
Na eneo linalobaki nje ya hizo km?

KWANI ENEO LA BAHARI ALILONALO ZANZIBAR UNALIFAHAMU? KAMA NI NCHI IKISEMA MELI ZA NCHI YA TZ ZISIPITE ENEO LETU UNAFAHAMU TUTAATHIRIKA VIPI? MWISHO WAO WANA UWEZO WA KIJESHI KULINDA ENEO LAO LILILOUNGANA NA SISI NA MAHARAMIA NA WAUZA MADAWA?

Mkuu Yoda, Majibu yake wala usinipe wewe hitimisha tu kwa namna unavyopenda wewe.
 
watakata mikoa yote ya pwani ya wapi? wakati pwani yoote Mjerumani ndio alitawala, Mafia Mjerumani aliinunua toka kwa sulan, na wazanzibari hilo hawalijui kwasababu shule imeenda kushoto. soma historia ndio uje kujadili hapa. hakuna pwani yeyote itakayodondokea kwao, wala kisiwa chochote, vyote hivyo vilikuwa Germany EAst Africa. vile visiwa vyao viwili tu na twingine tudogo tusitoonekana around there, ndio vilikuwa vimebaki kwa sultani na ndivyo walivyovikomboa. manake ukitaka kusema hivyo wao wanaamini hadi dsm ni mali yao, hapa dsm watakuja kwa visa, au la watarudishwa kwa kutembea kwa mguu hadi nungwi.

sisemi hivi ili kuuvunja muungano, naupenda, ila nawaonya wanaotibua maji wajue wakitibua ukavunjika wao ndio watakula hasara.

Najua yote unayoyasema, lakini haiondoi ukweli hayo ndio yatakuwa madai yao. Hata mimi ni muumini wa muungano wenye tija, Serikali tatu. Ulinzi, usalama wa Wazanzibar wote na Watanganyika ni swala la Serikali kuu, maisha ya kuu kwa miaka 1000 ijayo.

Hatuwezi tena kukubali ,kurudia uhuni tuliofanyiwa kwa miaka zaidi ya 600 iliyopita.
 
Wacha ujinga, kaka. Utumwa hautarudi. Wakati ule ilienea kwa sababu watu wa bara walitaka kuuza wafungwa wao, walifurahi kupata wateja Zanzibar.

Of course utasema hivyo. Mamilioni waliuzwa utumwani, mamilioni kuuwawa, kubakwa,kulawitiwa, kuhasiwa, kuteswa.

Kwa maoni yako walitaka, walipenda na kufurahi kutendewa haya matendo.
 
Waafrika walihusika kukamata na waliuza Waafrika wenzao pia katika biashara ya utumwa.

Jaribu kusoma kabla ya kujibu. Hakuna aliyetaka kuwa mtumwa. Ila machifu wengi, pamoja na wajasiriamali huru walipenda kuuza watu ili wapate hela. Waarabu walifanya biashara ya watumwa, kweli. Ila kila biashara inahitaji mnunuzi na mwuzaji. Sivyo? Waarabu kutoka püwani walikuta wengi walikuwa tayari kukamata watu na kuwauzia.
 
Waafrika walihusika kukamata na waliuza Waafrika wenzao pia katika biashara ya utumwa.

Baadhi, ni sawa na kusema Red Indians in North and South Amerika, (wahindi wekundu Amerika ya Kusini na Kaskazini), Aborigines wa Australia, New Zealand walihusika na kukubali kuuliwa, kuteswa na kutokomezwa duniani.
 
Jaribu kusoma kabla ya kujibu. Hakuna aliyetaka kuwa mtumwa. Ila machifu wengi, pamoja na wajasiriamali huru walipenda kuuza watu ili wapate hela. Waarabu walifanya biashara ya watumwa, kweli. Ila kila biashara inahitaji mnunuzi na mwuzaji. Sivyo? Waarabu kutoka püwani walikuta wengi walikuwa tayari kukamata watu na kuwauzia.
Hata wakija leo kuna Watanzania wachache watakuwa tayari kufanya biashara ya kuwauxa wenzao. Hiyo haiondoi asili yao ukatili, unyama, uhuni uliopitiliza, kumuona mweusi kama mnyama.

Ni sawa na kusema Red Indians in North and South Amerika, (wahindi wekundu Amerika ya Kusini na Kaskazini), Aborigines wa Australia, New Zealand walihusika na kukubali kuuliwa, kuteswa na kutokomezwa duniani sababu baadhi yao waliwauzia watumwa.
 
Kwanza fahamu sheria za kimataifa zinataka meli zote zisizo za kijeshi au kijasusi kuruhusiwa kupita bila bugdha hata katika nm 36 zilizo ndani ya umiliki wa taifa linalopakana na bahari halafu hizo km 58 kwa upande wetu hazitatutosha kupita katika hako kasehemu kadogo hadi twende kwenye hizo zao 58?

Eneo la bahari ya Tanzani ni kubwa sana na matumizi yake mpaka sasa ni kiduchu tu, umewahi kufikiria ncho kubwa kama Ethiopia, Congo na Uganda maisha yanaendaje bila bahari?!
Aisee......
Sawa sawa.
 
Suala la maharamia na dawa za kulevya utalinda katika km zako 58 ulizopakana nao na huko kwengine kusipopakana na sehemu yoyote lakini pia kuna wakati hata sisi tuliomba ushirikiano kutoka Africa ya Kusini kupambana na uvuvi harama katika bahari kuu, suala la mataifa kusaidiwa, kusaidiana na kushirikiana katika ulinzi wa eneo la bahari ni la kawaida sana duniani kote.
Sawa...
Nimeshaelewa tuishie hapa tu boss.
 
kiukweli sioni umuhmu wa muungano,Kama nchi ni moja ,why wawe na ubalos nje .si tuwaache waendelee na maisha yao,wakiuzwa ughaibuni na watt wao ,Basi!!
Wana mabalozi nje?Yaani kwa mfano kuna Balozi wa Zanzibar nchini Ufaransa ?
 
Wana mabalozi nje?Yaani kwa mfano kuna Balozi wa Zanzibar nchini Ufaransa ?
Nadhani alichanganya kuelewa post, ishu ni kwamba wazanzibar kila sehem inabidi wawepo, kwa hio hata hizo nafasi za ubalozi wa Tanzania inabidi wapewe ili kuwe na muungano, kiufupi wazanzibar wana power kubwa sana kuzidi jamii / kabila lolote
 
Tatizo nyie vijan hamuelewi, nyerere aliona mbari sana for security reasons kwasababu hata leo hii zanzbar wakijitenga hawata survive coz watakua week kijeshi kitendo cha nyerere kuleta muungano ni kutaka ku access eneo kubwa la bahari ya hind
Ni hasara kubwa huu Muungano walahi kwa wabara
 
Hata wakija leo kuna Watanzania wachache watakuwa tayari kufanya biashara ya kuwauxa wenzao. Hiyo haiondoi asili yao ukatili, unyama, uhuni uliopitiliza, kumuona mweusi kama mnyama.

Ni sawa na kusema Red Indians in North and South Amerika, (wahindi wekundu Amerika ya Kusini na Kaskazini), Aborigines wa Australia, New Zealand walihusika na kukubali kuuliwa, kuteswa na kutokomezwa duniani sababu baadhi yao waliwauzia watumwa.
Wafanyabiashara Waarabu hawakubagua sana. Hujui habari za watumwa Wazungu waliopelekwa Unguja pia? Soma habari za Salme, mtoto wa Sultani aliyemzaa na mama mtumwa kutoka Kaukazi? Zamani zaidi walinunua watumwa huko Urusi, sababu moja kwamba lugha za Ulaya Mashariki zinaitwa "slavonic" (=kitumwa) hadi leo.
 
Kwa akili ya kawaida Nyerere aliangalia mbali sana... just imagine kisiwa kama Zanzibar, ilivyo
1. ki-geographically ni ndogo mno
2. kiusalama pia. sisi kama tanganyika tungepata wakati mgumu sana kiusalama kutokana na natural za watu, na imani waliyo nayo ya kiislamu..
Kwa maana nyingine ingekuwa kwenye jumuiya ya kiislam..
Kwa maana nyingine lengo lilikuwa kuunganisha east africa na visiwa vyake vyote ...
 
Tip Tippu alikuwa mfanyabiashara wa tembe za ndovu , pia alikuwa guide akiongoza misafara ya Wagunduzi kama Henry Morton Stanley.

Watu aliowatumia kwenye misafara yake alikuwa akiwalipa. Inashangaza kuwa amekuwa alama ya biashara katili ya utumwa.

Himaya ya Oman ilikuwa baada ya Sultan wa Oman kujitanua na kuhamishia makazi Zanzibar, kabla ya hapo walikuwepo Wareno na wenyeji ambao hasa walikuwa wametoka Uajemi kwa ajili ya biashara. Wabantu wengi walihamia Zanzibar kutoka bara wakati wa biashara ya Utumwa, hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaowapa Uenyeji wa visiwa hivyo.
Ni wenyeji hapo tangu karne ya 7 ,sijui, mwenyewe umesema wabantu walihamia huko toka kipindi cha utumwa,
Elewa zanzibar ilipata uhuru kamili jabla ya mapinduzi,,, so kulikua na hofu huko visiwani kuwa sultan atarudi, ndiposa wakafanya muungano faster, chama kilichofanya mapinduzi ni Afro shiraz party in collaboration na UMMA party , chama cha umma party kiliongozwa na Abdurahaman Babu alikua mkomunist , enzi hizo kulikuwa vita baridi, inasemwa hiyo ilifanya nchi za magharibi kubariki muungano chap ili kuzuia uwezekano wa zenj kuwa communists launching pad in east africa
 
Back
Top Bottom