Mnielimishe: Ni kitu gani haswa Nyerere alikitaka kwenye Muungano, maana nachoona tunapigwa wazi wazi

Mnielimishe: Ni kitu gani haswa Nyerere alikitaka kwenye Muungano, maana nachoona tunapigwa wazi wazi

Wafanyabiashara Waarabu hawakubagua sana. Hujui habari za watumwa Wazungu waliopelekwa Unguja pia? Soma habari za Salme, mtoto wa Sultani aliyemzaa na mama mtumwa kutoka Kaukazi? Zamani zaidi walinunua watumwa huko Urusi, sababu moja kwamba lugha za Ulaya Mashariki zinaitwa "slavonic" (=kitumwa) hadi leo.

Nayajua yote hayo. Wazungu waliwachukua wengi, kama Wareno walinunua wengi tu kutoka kwa Waarabu wengi walipelekwa Brazil, Carribean. Lakini ni wengi zaidi walipelekwa Uarabuni, upande wa pili wa jangwa la sahara.

Kwa zaidi ya miaka 600 Waarabu walikuwa wakiwauza Watanganyika na weusi wengine. Ukiangalia hata sasa unaona kuna mchanganyiko South America, North America, Ulaya kidogo weusi wanapewa nafasi japo kiduchu.

Umeshawahi kuona wapi kiongozi mweusi Uarabuni, japo mamilioni walitumika kule kwa zaidi ya miaka mia sita. Pembe za ndovu, rasilimali na bara hili.

Kiuhalisia hakuna watu wabaguzi kama Waarabu hasa kwa mtu mweusi.
 
unapotezaje sehemu ya eneo la bahari wewe? yaani toka mtwara hadi Tanga, wenyewe kaeneo kao mbona kadogo tu, au unafikiri kwasababu ni kisiwa basi bahari yote wanamiliki, wanamiliki sehemu ndogo sana ya bahari hao urojo. utaanza kuhesabu nautical miles ngapi toka mafia hadi uwafikie, upande wa chini hawatashuka kwasababu hawana kisiwa chochote chini ya unguja, tanga kidogo itagawana kwasababu ya pemba. enda kwenye ramani angalia ramani yao, kuna,chukia kisiwa chao kimataifa kuna nautical miles kadhaa tu ndizo watamiliki. kwengine kote bara tutasambaa sana, tuna eneo kubwa la bahari kuliko na hawatuathiri chochote. ila kiukweli hawana faida kwetu zaidi ya undugu tu ambao wao hawaapreciate.
Kasome tena history
 
Yote yalifanywa kuisecure BARA zanzibar isingeungana na Mainland ilikua iwe taifa la dola ya kiislamu, afu intellejensia ya America(Ama uingereza kama sijakosea) ilimtonya mchonga kwamba kingekua kitovu cha mafunzo ya.....automatically bara isingetawalika.....sababu ya pili ilikua influence ya Vatican kwa mwl hapa sielezi sana ila it is what it is
Dhana potovu, mwaka 64 ugaidi ulikuwepo?
 
Huu ni muungano wa hovyo kuwahi kutokea duniani uvunjwe mara 1 waznz ndo wana nufaika na sio watu wa bara pia nawasifu wako vizur viongozi na wananchi wake wako makini na nchi yao sio sisi wa bara tuko kisiasa zaidi kiccm zaidi
 
Sisi wa bara hatutaki huuu muungano wa mchongo una tunyonya badala ya kutufadisisha sasa tuna marais Wawili wote wa zanzibar sa itakuwaje
 
Ni hasara kubwa huu Muungano walahi kwa wabara
hapana mkuu..........nyerere alipiga hesabu kali sana muungao una faida kubwakiulinzi.........imagine zanzibar ni free ste alafu ikulu yetu ipo pemben mwa bahari
 
Tatizo nyie vijan hamuelewi, nyerere aliona mbari sana for security reasons kwasababu hata leo hii zanzbar wakijitenga hawata survive coz watakua week kijeshi kitendo cha nyerere kuleta muungano ni kutaka ku access eneo kubwa la bahari ya hind
Security reason ilikua miaka hiyo.sasa hivi sidhani kama hiyo ni sababu.sababu iliyobaki ni yakisiasa tu.
 
Huu muungano siupendi
Naomba atokee Rais chizi auvunje tu.
Kwa akili za kawaida tu utaona hauwezi kudumu miaka mingi.maana maswali yasiyo na majibu ni mengi na kile kizazi cha zidumu fikra za mwenyekiti kinapukutika kwa kasi.kwahiyo uko mbele lazima waje watu wenye kuhoji zaidi kuliko kukaririshwa.
 
Wacha ujinga, kaka. Utumwa hautarudi. Wakati ule ilienea kwa sababu watu wa bara walitaka kuuza wafungwa wao, walifurahi kupata wateja Zanzibar.

Soko kubwa kabisa duniani ukanda wa Mashariki, bidhaa muhimu kabisa ilikuwa wewe na mababu na mabibi zako. Kaskazini ilikuwa Ghana. Soko dogo lilikuwa Bagamoyo la kuuza Watanganyika, weusi.

Dr John Alembllah book, milioni 80 walikufa safarini. Walifanya hivi walikata balls na penis, kwa waliowataka welipenda miaka 8 handi 12, asilimia 60% walikufa kwenye huu ukatili, ila waliobaki walinunuliwa kwa bei kubwa, nzuri sana kuwapa faida kubwa. Msome pia Ronald Seagal book 2001.

Amilikie Zanzibar; anamiliki usalama wa Afrika
 
Angefosi kuwe na serikali moja hizi drama zote zisengekuwepo.
Jambo wanalosahau wengi ni kwamba muungano ulipoanzishwa haukuwa ndio uwe umekamilika. Huo mwanzo ilikuwa ni kama 'process' ya kuanzia na kuendelea mbele.
Lengo likiwa kwamba ingefika wakati sehemu zote mbili zikawa zimechanganyika (integrated' kiasi cha kutojali tena u-Zanzibar' au u-Tanganyika. Mchakato ulilenga iwe hivyo. Lakini ili iwe hivyo ilitakiwa kazi endelevu, kila mara kuupeleka muungano kwenye lengo hilo.

Badala yake, na hasa baada ya waasisi kutokuwepo, matendo mengi yaliyofanyika, hasa kutoka upande wa Zanzibar ikawa ni kinyume na kuelekea kwenye lengo la mwanzo. Watu wakajitengenezea katiba yao, hata nyimbo ya taifa nadhani iliandaliwa, na kukawa na bendera ya NCHI ya Zanzibar. Hapakuwepo na jibu lolote la maana katika kuyakabili haya ya kuifanya Zanzibar kuwa nchi na mambo mengi mengine ya kudhoofisha muungano.

KERO za Muungano zikapamba moto toka upande mmoja wa muungano na kila mara zikawa zinalegeza nati za muungano, na waliokuwa viongozi kwenye serikali ya muungano wakawa hawatoi jibu la kuimalisha muungano, bali ikawa kama wanawapa waZanzibari RUHWA waendelee kuwepo kwenye muungano.

Sasa mambo yameanza kubadilika. Inaonekana sasa pawepo na utaratibu wa kuwasilisha "KERO ZA MUUNGANO" toka Bara, ili nazo zipatiwe ufumbuzi kama zile zinazoibuka kutoka Zanzibar.
 
Mbona Nyerere alikuwepo kwa miaka mingi sana baada ya Karume kuuwawa?

Hata issue ya Zanzibar kujiunga na OIC ni Nyerere ndiye alikemea Zanzibar ikalazimika kujitowa.

Kwa swala la muungano huu Nyerere anabeba lawama zote, alikuwepo na alikuwa na fursa ya kuweka mambo sawa kabla hajafa.

Malengo ya huu muungano ni kuimeza Zanzibar, sasa lengo limeshindikana na Wazanzibar ndio wananufaika Zaidi Watanganyika tumebaki tumepigwa na butwaa.

Ila adui wa yote haya ni ccm, kama Wazanzibar wangeachiwa waongozwe na Rais waliokuwa wakimpigia kura miaka yote Maalim Seif Sharrif Hamad hizi kero zisingekuwepo leo.
 
Muungano wa hovyo kabisa uvunjwe, upo sahihi mkuu
Watu wenye akili na wakiendelea kiuchumi na kijeshi wanaunganga wewe unataka matengano na makasiriko?
Umeshasikia kitu kinaitwa NATO?
Umeshasikia kitu kinaitwa EU
Je hii € unajua Ina nguvu kiasi gani?
 
Watu wenye akili na wakiendelea kiuchumi na kijeshi wanaunganga wewe unataka matengano na makasiriko?
Umeshasikia kitu kinaitwa NATO?
Umeshasikia kitu kinaitwa EU
Je hii € unajua Ina nguvu kiasi gani?
Huu ni muungano au unyonyaji tupu, Wabara haturuhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar lakini wazanzibar wamejaa huku na wanamiliki kila kitu wanachotaka, aibu kubwa sn uvunjwe hauna manufaa kwetu
 
Back
Top Bottom