Mnisahihishe kwa uhalisia lakini hadi sasa sijaona jamii yenye watu wenye mafanikio kuwazidi wazanzibari, wapo mbali sana na huu ni mwanzo tu

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Waznzibar wapo milioni na nusu hivi lakini mziki wao haukamatiki kwa % ya waliofanikiwa. Percentagewise ukiwaweka wazanzibari waliofanikiwa kwenye idadi ya wazanzibari wote, unapata asilimia kubwa kuzidi kabila au jamii yoyote hapa Tanzania bara.

- Kibiashara wapo juu, pesa wanazichapisha aisee, pale kariakoo wapemba wana mgao wao si haba, ukija kwa Don wao Bakhresa huyu ni habari nyingine,,,, vingamuzi vyake vimesambaa kila kona ya nchi, bidhaa zake za vyakula na vinywaji zimesambaa si mchezo, boti zake za usafiri majini hazina mpinzani, n.k.

- Vyeo vya juu vya Serikali ya Zanzibar kuanzia Raisi, makamu wa raisi, wabunge, wakuu wa mashirika ya zanzibar n.k inabidi uwe mzanzibar.

-Ajira za Zanzibar kuanzia ajira za kwenye ikulu, ajira za kwenye wizara za zanzibar, ajira za kwenye mashirika, n.k inabidi uwe mzanzibari.

- Vyeo vya juu vya Tanzania bara huku wamevikwida vya kutosha tu, mawaziri, vyeo vya juu jeshini, wakuu wa mashirika, wakuu wa taasisi, mabalozi, n.k

- Ajira za huku Tanzania bara sehemu kama Jeshini, bandarini, Tra, bot, nssf, n.k wamo wengi tu.

-Ajira ama teuzi kwa mzanzibari haijali sana elimu yake au uzoefu, uzanzibari wake pekee ni sifa kubwa kupata ajira ama kulamba teuzi tofauti na mtu wa bara watacheki ufaulu wako kwenye elimu, uzoefu wako, umesoma chuo kipi, n.k. kumkuta mzenji aliekuwa na uwezo mdogo darasani kapata kazi nzuri au kalamba teuzi ni jambo la kawaida.

-Jkt nako ukiwa mzanzibari hesabia ushapenya kwenye jeshi moja wapo iwe ni jwtz, polisi, n.k, kwa watu wa bara unaweza kujitolea jkt hapo miaka lakini mwisho wa siku unaambiwa urudi kijijini kwenu ukalime.

- Kwenye kilimo wapo wapo pia, wanamega maelfu ya hekari kwenye mapori ya huku bara kwajili ya kilimo cha biashara, bakhresa nahisi kamega ekari za kutosha sana bagamoyo analima sukari
 
Na usije kuropoka kusema ni kipindi hiki cha mama, La hasha!! ni tangu zamani
 
Wakuja ndo mkurugenz mwenyej mvuv wa ngalawa ameket kit cha enz pembeni kombe la kahawa...muungano ni kama koti likikubana unavua
 
leo kuna mtu alikuwa ananambia kuwa kitengo wamejaaa hao jamaa sasa naanza kuamini
 
leo kuna mtu alikuwa ananambia kuwa kitengo wamejaaa hao jamaa sasa naanza kuamini
wakishika nafasi za uongozi mambo ya elimu kwao hayanaga muda, mfano moja wao akiwa kiongozi wa shirika basi atamweka mzenji mwenzake mwenye diploma awe nafasi za juu, mtu wa bara mwenye masters yake hawezi fungua mdomo kwa bosi hapo kwamba yeye ana master, bosi hapangiwi, power ni kitu muhimu sana aisee.
 
Ila mtu wa bara atakuambia tunaitawala Zanzibar ila kiuhalisia Zanzibar ndio anaitawala Tanzania
Ni kipimo tosha kwamba watu wa bara wana matatizo ya pride .... ni sawa na tembo mwenye mwili mkubwa anatumwa na sungura kuchota maji mtoni halafu anajisifu kwamba yeye ana mkonga wa kubeba maji anamcheka sungura.
 
Vipi nduguzetu wachaga wanaojinasibu kila uchwao
 
Sample yako umechuku kwa viongozi au watu wa kawaida umefika pemba mkuu ukaona maisha ya watu wa kawaida kwa kuanzia na makazi yao.
 
Vipi nduguzetu wachaga wanaojinasibu kila uchwao
hao ni kweli wamefanikiwa kwa watu wa bara lakini hawagusi kwa wazazibari. labda ni wingi tu wa kuwa na idadi ya watu wengi ndio unawabeba lakini tukija kwa asilimia % ya waliofanikiwa kwenye hio idadi hawawezi kuwafikia wazenji.

Mzenji anashinda kibarazani hakosi kuwa na dada / kaka / dogo, n.k ambae yupo kakitengo flani huko kwao au huku bara wa kumtumia pesa za matunzo,,,
 
Sample yako umechuku kwa viongozi au watu wa kawaida umefika pemba mkuu ukaona maisha ya watu wa kawaida kwa kuanzia na makazi yao.
Hata marekani wapo watu hawana hata sehemu ya kulala, Tunapozungumzia watu flani wamefanikiwa haina maana kwamba kila moja wao kafanikiwa.... Kuna wapemba wengi tu kwa hapa Tz wanaishi poa tu wamemega mapande makubwa ya ardhi wanalima mazao na kuyauza, wana maduka ya jumla ya spea, wana baashara zao kiabo tu kariakoo, n.k. ukicheki asilimia ya hawa wapemba ukaiweka kwenye population yao, hata wachaga hawafikii robo percentage wise
 
Kwasababu hawalipi kodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…