'Mnyalu' wa UDSM: Muuza karatasi aliyetumia fursa

'Mnyalu' wa UDSM: Muuza karatasi aliyetumia fursa

Hongera mleta thread na wote waliochangia ..matukio ya mnyalu Kama series vile ..nasubiria episode nyingine ,hongera kwa mnyalu pia
 
Mnyalu ana business plan, na hiyo ndo inatakiwa kwa ma-graduants
 
Dah na atakua kawala sana aisee mana wale ni easy target. Ila kama kaanzisha kariakoo yake kwenye hayo ma hall ni vzuri atakua anakula vichwa hadi kule kariakoo kutakua kumedoda.

Nilikuwa najifunza kimyakimya mara nimevutiwa na hili ikabidi nivunje ukimya......naomba ufafanuzi kidogo hapo kwenye red
 
Habari!
Kwa wale waliowahi kusoma UDSM(Mlimani) miaka ya nyuma huenda wanamkumbuka huyu kijana "sharobaro" muuza karatasi ambaye inadaiwa ni "mnyalu" kutoka kule Iringa.

Alichokuwa anafanya ni kununua rimu kisha anabana karatasi 4 au 5 na kisha anauza kwa sh 100(kwa wakati huo,sijui sasa kama bado anauza).

Wengi walimchukulia kama "muhuni" flani mganga njaa lakini mimi namtazama kama mjasiriamali alieiona fursa na kuitumia tena katika jumuia ya wasomi ambao wengi wao hawakuiona kama ni fursa au kama waliiona basi waliidharau na kuona kuwa wao ni wasomi hawawezi kufanya biashara "kichaa" kama ile.
Tumfanyie makadirio madogo:
Bei ya Rimu 1aina ya MONDI = 6000
rimu ina karatasi 500
yeye anabana karatasi 4
Hivyo 500÷4=125 bundles
1 bundle=100Tsh
125 bundlesX100=12500 Tsh (mauzo)

Faida; 12500-6000=6500TSH(faida ya rimu moja tu)

Je akiuza rimu mbili kila siku kwa mwezi atakuwa na faida ya sh ngapi?
6500tsh X2 X5(working days) X4 Weeks=260,000Tsh

Tunajifunza nini kutoka kwa bwana "mnyalu"?? Mnyalu hana degree kama walivyo wengi wa wateja wake, wengine wana masters na hata Phd lakini mnyalu ameona fursa ndogo na kuitumia.

Je ni graduates wangapi wako mtaani wanashinda kuangalia TV kwa kisingizio cha kukosa ajira na hawaingizi hata alfu 10 kwa mwezi? jibu ni rahisi: HAWAWEZI KUFANYA KAZI HIYO kwa sababu si status yao, wao wana degree!!

Graduates wakiacha superiority complex waliyonayo basi nina hakika Macho yao YATAFUNGUKA na kuona Fursa nyingi zinazowazunguka ambazo nyingine hazihitaji mtaji mkubwa. Huu ni mfano tu mdogo kutoka kwa bwana "mnyalu" vipo vingi ambavyo graduates wanaweza kuvifanya individually au in groups

Ukiwa gradute unaweza kuiboresha wazo la biashara anayoifanya "mnyalu" na kulifanya kuwa ni wazo bora likakuingizia kipato zaidi. Mfano:

1.Chukua begi lako la mgongoni ulilokuwa unatumia chuo
2.chukua kiwi na brash unayoitumia kung'arisha viatu vyako
3.Nunua rimu mbili
4.Nunua staple machine ndogo
5.Nunua box la kalamu ya blue na nyeusi
6.nunua karanga kg1,kaanga na funga kwenye vipakiti
7.Nunua BIG G/PK
8. Nenda ofisi za tigo na ungainishi line yako na huduma ya kuuza tigo rusha(kuunganishwa ni bure)....uza tigo rusha

Weka vitu vyote kwenye begi na zunguka maeneo ya chuo na anza kutoa huduma.

Mtaji ukikua nunua mashine ya KUPIMA UZITO, weka kwenye bag na anza kutoa huduma....believe me wadada wanapenda sana kupima uzito ili kudhibiti miili yao isinenepe hovyo.

Kwa kifupi utakuwa unauza vocha,kung'arisha viatu vya wanafunzi,kuuza bites,kuuza kalamu na karatasi, kupima uzito nk
Je kwa mwezi utakuwa unaingiza kiasi gani??

Jitahidi kujenga uhusiano mzuri nnna wateja wako, ikiwezekana tengeneza business card ioneshe kiwango chako cha elimu, believe me utapata connection humo humo kutoka kwa wateja wako mana wengine wana makampuni yao na watavutika tu na uthubutu wako na wangependa ufanye nao kazi.

. Biashara hii mtaji wake ni MDOGO SANA. Ondoa aibu,superiority complex na acha kukaa nyumbani bila kazi

Miaka ya nyuma ipi? Au tangu chuo kilipoanzishwa? Mimi nilipokuwepo mlimani sikuwahi kumwona huyo unayemsema mbali na wauza matunda hata kabla ya masoko kujengwa hall 5.
 
Miaka ya nyuma ipi? Au tangu chuo kilipoanzishwa? Mimi nilipokuwepo mlimani sikuwahi kumwona huyo unayemsema mbali na wauza matunda hata kabla ya masoko kujengwa hall 5.

Ukishajua ni mwaka fulani inakusaidia nini?yani kwenye content yote ulichojifunza ni hiki tu? Au unataka kutuaminisha kuwa na wewe umesoma zamani zaidi?..it doesnt matter, halafu jua kuwa si kila aliesoma mlimani kwa kipindi hicho ambacho mnyalu yupo ni mtoto mdogo, au alianza undergraduate nk. Wengine walisoma masters na/ phd tu kwa hiyo si vijana wadogo wa umri pengine hata wewe unaejiona "mzee wa enzi hizo" ukawa ni mdogo kwao.

Wapo waliopita hapo katika zaidi ya mara moja katika vipindi tofauti zamani za enzi za yombo 1 na 2 kuwa cafteria mpaka leo kuna yombo 5 lecture theaters.
By the way turudi kwenye mada ,tujadili tunachojifunza kwake
 
Dah na atakua kawala sana aisee mana wale ni easy target. Ila kama kaanzisha kariakoo yake kwenye hayo ma hall ni vzuri atakua anakula vichwa hadi kule kariakoo kutakua kumedoda.
hahha nkajua utanipa na ushuhuda kabisa walioliwa...
 
Ukishajua ni mwaka fulani inakusaidia nini?yani kwenye content yote ulichojifunza ni hiki tu? Au unataka kutuaminisha kuwa na wewe umesoma zamani zaidi?..it doesnt matter, halafu jua kuwa si kila aliesoma mlimani kwa kipindi hicho ambacho mnyalu yupo ni mtoto mdogo, au alianza undergraduate nk. Wengine walisoma masters na/ phd tu kwa hiyo si vijana wadogo wa umri pengine hata wewe unaejiona "mzee wa enzi hizo" ukawa ni mdogo kwao.

Wapo waliopita hapo katika zaidi ya mara moja katika vipindi tofauti zamani za enzi za yombo 1 na 2 kuwa cafteria mpaka leo kuna yombo 5 lecture theaters.
By the way turudi kwenye mada ,tujadili tunachojifunza kwake

Kwanza elimu haina umri - kuna watu wanafanya undergraduate na umri mkubwa na wengine wenye umri mdogo wanafanya doctorate.

Nilichojifunza kwenye content yako ni kuwa wateja wa huyo Mnyalu walikuwa ni wajinga (yawezekana nawe pia ulikuwa mteja wake) kwa sababu walikuwa wananunua ream ya karatasi mara mbili ya bei ya dukani. Kuuliza ni kipindi gani nilitaka kupata context kamili ya story yako; na wala sijataka kujua umri wa mtu.

Halafu hizo biashara ambazo unashauri graduates wafanye sio za viwango vyao; ni vyema ufanye wewe mwenyewe ili uwe kama Bakhresa kwani naye inadaiwa alianzia huko unakosema.
 
ndio uwezo wako wa kufikiri ulipoishia. Kwa hiyo wewe ulitaka wafanye kazi zipi za VIWANGO VYAO ikiwa wamemaliza chuo na ajira ya kile walichokisomea hakuna?
Unataka wachague kazi wakati hicho cha kuchagua hakipo?
Au waendelee kukaa nyumbani kula kwa shemeji ?
hivi njaa inaangalia KIWANGO cha mtu? Unajua namna vijana wanavyoteseka mtaani kuzungusha bahasha huku hawaijui hata kula yao?? Should they keep on waiting "KAZI YA VIWANGO"?
 
Mnyalu anakula watoto wazuri sana pale UDSM kuna wakati tuligongana kwa demu fulani mitaa ya kati SURVEY MOTEL, jamaa linahonga hatari, sema enzi hizo mimi ndo nilikuwa bado dent kwa hiyo hela yenyewe ya mawazo full UBAHILI
 
huwa namfananisha na yule msanii Suma G

hata mi nlikua namfananisha na Suma G...he was friendly kwa kweli na nlikua mteja wake mzuri.Mbali na Mnyalu kulikua na dada Ubuyu huyu nae alikua na wateja sana kwa biashara ya ubuyu na karanga.Waliona fursa wakaitumia naamini ilikua inawafaidisha sana.
 
Perfect..... ni kweli kabisa na mimi nimeleta mfano wa mnyalu ili jamii ifunguke macho si tu wafanye biashara hii ila wajifunze kufumbua macho kuangalia fursa katika mazingira yanayowazunguka.

swali la kizushi:Hivi bado mnyalu yupo hadi Leo UDSM ?

Bado yupo , mimi nilitoka mwaka jana pale nilimuacha , tena amepanua biashara yake kweli , , ameweka meza kila ukumbi wa lecture.. Kwanzia theatre kule , yombe , maeneo ya sr na kadhalika... Jamaa nina ukakika kwa sasa anaigusa 50 per day
 
mwaka jana mwanzoni nilienda pale nikakuta anauza soda na ana mafriji pale daruso sijui mpaka sasa

Ni kweli mpaka sasa hvi anauza soda na ana mafriji na biashara zake zimezidi kukua...

Hivi wewe masai dada ni mtu wa aina gani?? Mbna unajua mambo mengi na sehemu nyingi pia ushafika na kupita??? Natamani kukujua zaidi.. Labda tunafahamiana
 
Last edited by a moderator:

kawaida tu mkuu

uwenda ukanifahamu
 
Last edited by a moderator:
The Lion does not eat Grass no matter the economy of the jungle. Its not Pride its just what it is
 
hata mi nlikua namfananisha na Suma G...he was friendly kwa kweli na nlikua mteja wake mzuri.Mbali na Mnyalu kulikua na dada Ubuyu huyu nae alikua na wateja sana kwa biashara ya ubuyu na karanga.Waliona fursa wakaitumia naamini ilikua inawafaidisha sana.

mie mwenyewe nilikua mteja wake, alikua charming saana , Haaa jamani umenikumbusha yule dada wa ubuyu na karanga ... alikua anauza nae si haba... muda mmkeaa discussion akipita mwebyewe
 
Back
Top Bottom