'Mnyalu' wa UDSM: Muuza karatasi aliyetumia fursa

'Mnyalu' wa UDSM: Muuza karatasi aliyetumia fursa

Ni kweli mpaka sasa hvi anauza soda na ana mafriji na biashara zake zimezidi kukua...

Hivi wewe masai dada ni mtu wa aina gani?? Mbna unajua mambo mengi na sehemu nyingi pia ushafika na kupita??? Natamani kukujua zaidi.. Labda tunafahamiana

pale daruso hayupo nw japo kuna friji moja chakavu tu;sijui unazungumzia daruso ipi???
 
Last edited by a moderator:
Kumbe watu wengi mmesoma UDSM huku.... Ndio maana vilaza... Wengine degree zetu tumezipatia Havard University kama Obama.
.
 
Habari!
Kwa wale waliowahi kusoma UDSM(Mlimani) miaka ya nyuma huenda wanamkumbuka huyu kijana "sharobaro" muuza karatasi ambaye inadaiwa ni "mnyalu" kutoka kule Iringa.

Alichokuwa anafanya ni kununua rimu kisha anabana karatasi 4 au 5 na kisha anauza kwa sh 100(kwa wakati huo,sijui sasa kama bado anauza).

Wengi walimchukulia kama "muhuni" flani mganga njaa lakini mimi namtazama kama mjasiriamali alieiona fursa na kuitumia tena katika jumuia ya wasomi ambao wengi wao hawakuiona kama ni fursa au kama waliiona basi waliidharau na kuona kuwa wao ni wasomi hawawezi kufanya biashara "kichaa" kama ile.
Tumfanyie makadirio madogo:
Bei ya Rimu 1aina ya MONDI = 6000
rimu ina karatasi 500
yeye anabana karatasi 4
Hivyo 500÷4=125 bundles
1 bundle=100Tsh
125 bundlesX100=12500 Tsh (mauzo)

Faida; 12500-6000=6500TSH(faida ya rimu moja tu)

Je akiuza rimu mbili kila siku kwa mwezi atakuwa na faida ya sh ngapi?
6500tsh X2 X5(working days) X4 Weeks=260,000Tsh

Tunajifunza nini kutoka kwa bwana "mnyalu"?? Mnyalu hana degree kama walivyo wengi wa wateja wake, wengine wana masters na hata Phd lakini mnyalu ameona fursa ndogo na kuitumia.

Je ni graduates wangapi wako mtaani wanashinda kuangalia TV kwa kisingizio cha kukosa ajira na hawaingizi hata alfu 10 kwa mwezi? jibu ni rahisi: HAWAWEZI KUFANYA KAZI HIYO kwa sababu si status yao, wao wana degree!!

Graduates wakiacha superiority complex waliyonayo basi nina hakika Macho yao YATAFUNGUKA na kuona Fursa nyingi zinazowazunguka ambazo nyingine hazihitaji mtaji mkubwa. Huu ni mfano tu mdogo kutoka kwa bwana "mnyalu" vipo vingi ambavyo graduates wanaweza kuvifanya individually au in groups

Ukiwa gradute unaweza kuiboresha wazo la biashara anayoifanya "mnyalu" na kulifanya kuwa ni wazo bora likakuingizia kipato zaidi. Mfano:

1.Chukua begi lako la mgongoni ulilokuwa unatumia chuo
2.chukua kiwi na brash unayoitumia kung'arisha viatu vyako
3.Nunua rimu mbili
4.Nunua staple machine ndogo
5.Nunua box la kalamu ya blue na nyeusi
6.nunua karanga kg1,kaanga na funga kwenye vipakiti
7.Nunua BIG G/PK
8. Nenda ofisi za tigo na ungainishi line yako na huduma ya kuuza tigo rusha(kuunganishwa ni bure)....uza tigo rusha

Weka vitu vyote kwenye begi na zunguka maeneo ya chuo na anza kutoa huduma.

Mtaji ukikua nunua mashine ya KUPIMA UZITO, weka kwenye bag na anza kutoa huduma....believe me wadada wanapenda sana kupima uzito ili kudhibiti miili yao isinenepe hovyo.

Kwa kifupi utakuwa unauza vocha,kung'arisha viatu vya wanafunzi,kuuza bites,kuuza kalamu na karatasi, kupima uzito nk
Je kwa mwezi utakuwa unaingiza kiasi gani??

Jitahidi kujenga uhusiano mzuri nnna wateja wako, ikiwezekana tengeneza business card ioneshe kiwango chako cha elimu, believe me utapata connection humo humo kutoka kwa wateja wako mana wengine wana makampuni yao na watavutika tu na uthubutu wako na wangependa ufanye nao kazi.

. Biashara hii mtaji wake ni MDOGO SANA. Ondoa aibu,superiority complex na acha kukaa nyumbani bila kazi

Kuna wanachuo wengine wajanja waliotea mchongo wakaudandia.

Kuna jamaa anajiita "Mtoto wa Nguchiro" (Kamaliza mwaka huu),
Huyu jamaa alikuwa anauza
-karatasi,
-kalamu,
-karanga,
-madesa,
-embe,
-M-PESA,
-machungwa,
-ubuyu,
-nguo za mtumba,
-tikiti maji,
-mafuta ya kuosha PC,
-kusuka nywele wasichana &
-kupaka rangi ya kucha.
 
ndio uwezo wako wa kufikiri ulipoishia. Kwa hiyo wewe ulitaka wafanye kazi zipi za VIWANGO VYAO ikiwa wamemaliza chuo na ajira ya kile walichokisomea hakuna?
Unataka wachague kazi wakati hicho cha kuchagua hakipo?
Au waendelee kukaa nyumbani kula kwa shemeji ?
hivi njaa inaangalia KIWANGO cha mtu? Unajua namna vijana wanavyoteseka mtaani kuzungusha bahasha huku hawaijui hata kula yao?? Should they keep on waiting "KAZI YA VIWANGO"?

Yawezekana ndio uwezo wangu wa kufikiri umeishia hapo kutokana na mtazamo wako. Je, wewe una kazi ya kuajiriwa? Kama ndio uliipataje hiyo kazi? Kwa kupata favour i.e. kujuana au rushwa au kihalali? Kama ni kwa kubebwa basi hauna right kabisa ya kutoa ushauri ulioweka hapa! Je unaonaye ukaacha hiyo kazi ulionayo na kufanya biashara uliopendekeza hapo juu? Hivi vijana wote ambao unasema wafanye biashara hiyo, na wote wakaaitikia ushauri wako soko litakuwa zuri kweli kwao?

Kwanza hata uelewi kama huyo mnyalu bado ana hiyo biashara au la.
 
Mkuu, nitakuwa sahihi nikisema HUJASOMA nilichoandika UKAKIELEWA(You didn't read between lines). Hebu angalia hizi sehemu hapa chini:
..............

Tunajifunza nini kutoka kwa bwana "mnyalu"?? ...... lakini mnyalu ameona fursa ndogo na kuitumia.

Graduates wakiacha superiority complex waliyonayo basi nina hakika Macho yao YATAFUNGUKA na kuona Fursa nyingi zinazowazunguka ambazo nyingine hazihitaji mtaji mkubwa. Huu ni mfano tu mdogo kutoka kwa bwana "mnyalu" vipo vingi ambavyo graduates wanaweza kuvifanya individually au in groups.........

...... tengeneza business card ioneshe kiwango chako cha elimu, believe me utapata connection humo humo kutoka kwa wateja wako mana wengine wana makampuni yao na watavutika tu na uthubutu wako na wangependa ufanye nao kazi.

mkuu, ukisoma vizuri hizo nukuu hapo juu utaelewa LENGO la thread hii.

Wewe umejikita kwenye personal attack kuliko hoja.Kwanza hakuna mahala popote nimesema kuwa mimi nimeajiriwa, Na pia simuumini wa kuhonga/rushwa. Fuatilia nyuzi zangu humu utajua mimi ni muajiriwa au ni mfanyabiashara!na pia hakuna mahala Nimesema graduates wote wafanye hiyo biashara ila nimeonesha MFANO TU na nimesisitiza kuwa wanaweza kufanya vitu vingine nje ya nilichokieleza individually au kimakundi. Najua nadharia ya demand na supply na najua pia haiwezekani wote wakafanya kazi hiyo ila ninachohamasisha hapa ni kwamba WAHITIMU WETU WAYAANGALIE MAISHA KWA JICHO LA TATU!

Ama kuhusu mimi kutojua mnyalu yupo au hayupo udsm kwa sasa thats not a big deal. Na hapa hatumjadili yeye kama yeye ila tunataka tujifunze kupitia anacho/alichofanya. Nadhani umeona shuhuda zikitolewa jinsi alivyokuza biashara yake from scratch mpaka sasa yuko pazuri kiasi. Vijana wanatakiwa wajifunze kutoka kwake kwamba kuna wakati hali ikiwa nje ya matarajio basi vijana "wasione soo" kuanza level za chini. Kama wewe "mheshimiwa" ulipograduate tu ukapata kazi na mambo yakanyooka fahamu kuwa si kila mtu huwa hivyo. Wengine wamesoma ila wako mtaani zaidi ya mwaka hawajapata kazi ya kile walichokisomea. Hapo sasa ndipo hoja inakuja na lengo la uzi huu linapojitokeza.

Ikiwa una nia ya kuelewa naamini utakuwa umeelewa ama kama umeamua kuleta mnakasha tu , i am sorry, allow me to save my energy niwatumikie watanzania wengine wanaohitaji ushauri wangu.! I agree to disagree with you.
 
Hahaaaa COET halikua hapendi sana alikua anapenda wa Udbs na college ya soicial sciences wadada ndo walikua wamemzoea sana.
Mkuu naenda kusoma hapo UDBS mwaka huu... umenihamasisha sana kusema kuwa kuna totoz za ukweli.. ntafaulu sana inshaallah

Nikirudi kwenye mada ni kuwa vijana wa kibongo tuache ubishoo hauna faida. Binafsi nilikuwa na mtazamo wa kipuuzi sana kuona hadhi yangu ni kubwa kufanya baadhi ya kazi. Niliajiriwa mara baada ya chuo 2010 nà kijimshahara kisichofika hata 1m kwa mwezi ila mwaka 2013 nilijishtukia na kuanza process ya kuacha kazi kiusalama na kujiajiri. Na kwa bahati nzuri kufikia 2014 September nikawa tayari nimeacha kazi na kujikita rasmi kwenye biashara zangu ndogondogo tena ndogondogo kweli. Ila kutokana na ile nia ya dhati hadi sasa maisha yamebadilika na kipato kimekua sana. Na kwa sasa nafikiria kumalizia kusoma hapo UDBS bila changamoto za ada. Nimalizie kusema tafadhali vijana wenzangu tuamke ubishoo sio mpango.
 
Umemaliza vizuri ,japo umeanza VIBAYA.Hizo "totoz" zitakurudisha nyuma hatua 100 ukiziendekeza. By the way hongera kwa kuthubutu na kuwa mjasiriamali ulianzie chini kabisa!
 
Mkuu, nitakuwa sahihi nikisema HUJASOMA nilichoandika UKAKIELEWA(You didn't read between lines). Hebu angalia hizi sehemu hapa chini:

mkuu, ukisoma vizuri hizo nukuu hapo juu utaelewa LENGO la thread hii.

Wewe umejikita kwenye personal attack kuliko hoja.Kwanza hakuna mahala popote nimesema kuwa mimi nimeajiriwa, Na pia simuumini wa kuhonga/rushwa. Fuatilia nyuzi zangu humu utajua mimi ni muajiriwa au ni mfanyabiashara!na pia hakuna mahala Nimesema graduates wote wafanye hiyo biashara ila nimeonesha MFANO TU na nimesisitiza kuwa wanaweza kufanya vitu vingine nje ya nilichokieleza individually au kimakundi. Najua nadharia ya demand na supply na najua pia haiwezekani wote wakafanya kazi hiyo ila ninachohamasisha hapa ni kwamba WAHITIMU WETU WAYAANGALIE MAISHA KWA JICHO LA TATU!

Ama kuhusu mimi kutojua mnyalu yupo au hayupo udsm kwa sasa thats not a big deal. Na hapa hatumjadili yeye kama yeye ila tunataka tujifunze kupitia anacho/alichofanya. Nadhani umeona shuhuda zikitolewa jinsi alivyokuza biashara yake from scratch mpaka sasa yuko pazuri kiasi. Vijana wanatakiwa wajifunze kutoka kwake kwamba kuna wakati hali ikiwa nje ya matarajio basi vijana "wasione soo" kuanza level za chini. Kama wewe "mheshimiwa" ulipograduate tu ukapata kazi na mambo yakanyooka fahamu kuwa si kila mtu huwa hivyo. Wengine wamesoma ila wako mtaani zaidi ya mwaka hawajapata kazi ya kile walichokisomea. Hapo sasa ndipo hoja inakuja na lengo la uzi huu linapojitokeza.

Ikiwa una nia ya kuelewa naamini utakuwa umeelewa ama kama umeamua kuleta mnakasha tu , i am sorry, allow me to save my energy niwatumikie watanzania wengine wanaohitaji ushauri wangu.! I agree to disagree with you.

Kaka asante for your time and wisdom!Trust me,some people need such motivations to wake up and stop waiting for "graduate jobs". Wenye akili na watafutaji lazima hii thread itawapa changamoto ila wanaosubiri kuajiriwa ofcn na kupata ajira kwa vimemo ndio kama hao tunaoona wanacrush!!
Watu wanasahau education isn't a guarantee for being employed but with education you can create your own employment!!!
 
Umemaliza vizuri ,japo umeanza VIBAYA.Hizo "totoz" zitakurudisha nyuma hatua 100 ukiziendekeza. By the way hongera kwa kuthubutu na kuwa mjasiriamali ulianzie chini kabisa!
Mkuu nachangamsha baraza tu sio mtu wa totozz... kaka mimi naamini msemo wa THINK BIG AND START SMALL na ule wa COPY, IMPROVE AND PASTE. Hapo namaanisha tuwaze makubwa ila tuanze mdogomdogo na pia tukumbuke karibu kila biashara imeshafanyika kwa hiyo sio kujisikitikia ni kusoma tu jamii ina tatizo gani halafu unaisaidia huku na wao wakitia pesa mifukoni mwako.
 
Kaka asante for your time and wisdom!Trust me,some people need such motivations to wake up and stop waiting for "graduate jobs". Wenye akili na watafutaji lazima hii thread itawapa changamoto ila wanaosubiri kuajiriwa ofcn na kupata ajira kwa vimemo ndio kama hao tunaoona wanacrush!!
Watu wanasahau education isn't a guarantee for being employed but with education you can create your own employment!!!
Mkuu umenena vyema sana... tatizo kubwa ni vijana wengi kuelewa vibaya ujasiriamali. Baadhi hudhani ujasiriamali ni ujanjaujanja na utapeli kumbe ni jambo lenye maana nzito mno. Hiyo hupelekea watu kuwa wavivu, wenye tamaa na wasio waaminifu.
 
Ebana yule jamaa ni suma g kabisa aisee, aliwahi mzingua dada flani hivi class, "ebana daaah mtoto kachoooooonga huyuuuuu" hahahaha daaah yani hata kama uwe umeonana nae mara ya kwanza jamaa anaongea tafikiri mshawahi kutana kipindi kirefuu, sijawahi muona kakasirika yule jamaa aiseee...daaah...jamaa nadhani atakua na Mark X, Altezza au Brevis hahahahahaha...
 
TzPride naona anaingia na gia zile zile ambazo hapa hazitaisihia mbali . Ninapenda kuwa hakikishieni kwamba majereta hayo yameazimwa na si kununulia .Kwa hiyo we have spent so much kwa kitu cha muda maana serikali haina shida na ku solve shida ya umeme Tanzania kwa kuwa madukani yao yatakosa soko la vijenerata.Kwa hiyo tumeazima na hatujanunua .Mwendo mdundo kasi mpya

Asante mkuu, lets join hands together as unity is POWER. naamini wataelewa ,its a matter of time tu!
 
Kinachotakiwa kwa magraduate kuelewa ni kwamba, kujiajiri katika sekta binafsi na duni ni sehemu ya changamoto ambapo anapoitatua changamoto hii hujikuta akiwa anamiliki biashara inayompa kipato kizuri.
 
Yule mnyalu katumia fursa ipasavyo. Na naomba niongezee kitu hapo, yule mnyalu hauzi zile karatasi UD peke yake. Mm nilianza kumjua nikiwa o'level alikuwa anatuuzia hizo karatasi hapo shuleni.

Advance nikaenda shule ya Tambaza..napo nikakutana nae.Kuna tuition centre moja ilikuwa pale ubungo nilikuwa nasoma napo nilimuwa nikie da namkuta. Nikaja kusoma chuo UD napo nikamkuta yupo. Mpaka akawaga rafiki yangu mkubwa maana kila shule nikienda nakutana nae.Kwa maana hiyo hiyo faida izidishe kwa shule/vyuo zaidi ya kimoja. Anapata pesa sana yule mkaka!

Big up kwake!
 
Jamaa ni msanii pia, cheki songi lake hapa:

Last edited by a moderator:
Mkuu umenena vyema sana... tatizo kubwa ni vijana wengi kuelewa vibaya ujasiriamali. Baadhi hudhani ujasiriamali ni ujanjaujanja na utapeli kumbe ni jambo lenye maana nzito mno. Hiyo hupelekea watu kuwa wavivu, wenye tamaa na wasio waaminifu.

Af watu hawajui au tuseme ni uwoga wa kudhubutu ila kua mjasiriamali ni raha sana kuliko kuajiriwa.
 
yawezekana ndio uwezo wangu wa kufikiri umeishia hapo kutokana na mtazamo wako. Je, wewe una kazi ya kuajiriwa? Kama ndio uliipataje hiyo kazi? Kwa kupata favour i.e. Kujuana au rushwa au kihalali? Kama ni kwa kubebwa basi hauna right kabisa ya kutoa ushauri ulioweka hapa! Je unaonaye ukaacha hiyo kazi ulionayo na kufanya biashara uliopendekeza hapo juu? Hivi vijana wote ambao unasema wafanye biashara hiyo, na wote wakaaitikia ushauri wako soko litakuwa zuri kweli kwao?

Kwanza hata uelewi kama huyo mnyalu bado ana hiyo biashara au la.

we ni fwalaaaaaaa na waswas na hata kama unamaendeleo
 
Back
Top Bottom