'Mnyalu' wa UDSM: Muuza karatasi aliyetumia fursa

Hongera mleta thread na wote waliochangia ..matukio ya mnyalu Kama series vile ..nasubiria episode nyingine ,hongera kwa mnyalu pia
 
Mnyalu ana business plan, na hiyo ndo inatakiwa kwa ma-graduants
 
Dah na atakua kawala sana aisee mana wale ni easy target. Ila kama kaanzisha kariakoo yake kwenye hayo ma hall ni vzuri atakua anakula vichwa hadi kule kariakoo kutakua kumedoda.

Nilikuwa najifunza kimyakimya mara nimevutiwa na hili ikabidi nivunje ukimya......naomba ufafanuzi kidogo hapo kwenye red
 

Miaka ya nyuma ipi? Au tangu chuo kilipoanzishwa? Mimi nilipokuwepo mlimani sikuwahi kumwona huyo unayemsema mbali na wauza matunda hata kabla ya masoko kujengwa hall 5.
 
Miaka ya nyuma ipi? Au tangu chuo kilipoanzishwa? Mimi nilipokuwepo mlimani sikuwahi kumwona huyo unayemsema mbali na wauza matunda hata kabla ya masoko kujengwa hall 5.

Ukishajua ni mwaka fulani inakusaidia nini?yani kwenye content yote ulichojifunza ni hiki tu? Au unataka kutuaminisha kuwa na wewe umesoma zamani zaidi?..it doesnt matter, halafu jua kuwa si kila aliesoma mlimani kwa kipindi hicho ambacho mnyalu yupo ni mtoto mdogo, au alianza undergraduate nk. Wengine walisoma masters na/ phd tu kwa hiyo si vijana wadogo wa umri pengine hata wewe unaejiona "mzee wa enzi hizo" ukawa ni mdogo kwao.

Wapo waliopita hapo katika zaidi ya mara moja katika vipindi tofauti zamani za enzi za yombo 1 na 2 kuwa cafteria mpaka leo kuna yombo 5 lecture theaters.
By the way turudi kwenye mada ,tujadili tunachojifunza kwake
 
Dah na atakua kawala sana aisee mana wale ni easy target. Ila kama kaanzisha kariakoo yake kwenye hayo ma hall ni vzuri atakua anakula vichwa hadi kule kariakoo kutakua kumedoda.
hahha nkajua utanipa na ushuhuda kabisa walioliwa...
 

Kwanza elimu haina umri - kuna watu wanafanya undergraduate na umri mkubwa na wengine wenye umri mdogo wanafanya doctorate.

Nilichojifunza kwenye content yako ni kuwa wateja wa huyo Mnyalu walikuwa ni wajinga (yawezekana nawe pia ulikuwa mteja wake) kwa sababu walikuwa wananunua ream ya karatasi mara mbili ya bei ya dukani. Kuuliza ni kipindi gani nilitaka kupata context kamili ya story yako; na wala sijataka kujua umri wa mtu.

Halafu hizo biashara ambazo unashauri graduates wafanye sio za viwango vyao; ni vyema ufanye wewe mwenyewe ili uwe kama Bakhresa kwani naye inadaiwa alianzia huko unakosema.
 

ndio uwezo wako wa kufikiri ulipoishia. Kwa hiyo wewe ulitaka wafanye kazi zipi za VIWANGO VYAO ikiwa wamemaliza chuo na ajira ya kile walichokisomea hakuna?
Unataka wachague kazi wakati hicho cha kuchagua hakipo?
Au waendelee kukaa nyumbani kula kwa shemeji ?
hivi njaa inaangalia KIWANGO cha mtu? Unajua namna vijana wanavyoteseka mtaani kuzungusha bahasha huku hawaijui hata kula yao?? Should they keep on waiting "KAZI YA VIWANGO"?
 
Mnyalu anakula watoto wazuri sana pale UDSM kuna wakati tuligongana kwa demu fulani mitaa ya kati SURVEY MOTEL, jamaa linahonga hatari, sema enzi hizo mimi ndo nilikuwa bado dent kwa hiyo hela yenyewe ya mawazo full UBAHILI
 
huwa namfananisha na yule msanii Suma G

hata mi nlikua namfananisha na Suma G...he was friendly kwa kweli na nlikua mteja wake mzuri.Mbali na Mnyalu kulikua na dada Ubuyu huyu nae alikua na wateja sana kwa biashara ya ubuyu na karanga.Waliona fursa wakaitumia naamini ilikua inawafaidisha sana.
 
Perfect..... ni kweli kabisa na mimi nimeleta mfano wa mnyalu ili jamii ifunguke macho si tu wafanye biashara hii ila wajifunze kufumbua macho kuangalia fursa katika mazingira yanayowazunguka.

swali la kizushi:Hivi bado mnyalu yupo hadi Leo UDSM ?

Bado yupo , mimi nilitoka mwaka jana pale nilimuacha , tena amepanua biashara yake kweli , , ameweka meza kila ukumbi wa lecture.. Kwanzia theatre kule , yombe , maeneo ya sr na kadhalika... Jamaa nina ukakika kwa sasa anaigusa 50 per day
 
mwaka jana mwanzoni nilienda pale nikakuta anauza soda na ana mafriji pale daruso sijui mpaka sasa

Ni kweli mpaka sasa hvi anauza soda na ana mafriji na biashara zake zimezidi kukua...

Hivi wewe masai dada ni mtu wa aina gani?? Mbna unajua mambo mengi na sehemu nyingi pia ushafika na kupita??? Natamani kukujua zaidi.. Labda tunafahamiana
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli mpaka sasa hvi anauza soda na ana mafriji na biashara zake zimezidi kukua...

Hivi wewe masai dada ni mtu wa aina gani?? Mbna unajua mambo mengi na sehemu nyingi pia ushafika na kupita??? Natamani kukujua zaidi.. Labda tunafahamiana
kawaida tu mkuu

uwenda ukanifahamu
 
Last edited by a moderator:
The Lion does not eat Grass no matter the economy of the jungle. Its not Pride its just what it is
 

mie mwenyewe nilikua mteja wake, alikua charming saana , Haaa jamani umenikumbusha yule dada wa ubuyu na karanga ... alikua anauza nae si haba... muda mmkeaa discussion akipita mwebyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…