Mnyama aliyeishi miaka milioni 240 iliyopita agundulika Tanzania

Mnyama aliyeishi miaka milioni 240 iliyopita agundulika Tanzania

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
NB: Translation ya baadhi ya maneno ya Kiswahili yaliyotumika
  • Dinosaria- Dinasours 🦕
  • Visukuku- Fossils 🦴
Screenshot_20260923-180634.png

Wanasayansi wamegundua spishi mpya ya mnyama wa kale aliyeishi takribani miaka milioni 240 iliyopita.

Kiumbe huyo aliyekula mimea, aliyepewa jina la Dinodontosaurus isiyavamanda, aligunduliwa katika eneo ambalo sasa ni Tanzania, Afrika Mashariki.

Kilichowashangaza watafiti ni kwamba hapo awali mabaki ya visukuku vya Dinodontosaurus yalikuwa yamepatikana Amerika Kusini pekee.

Wataalamu wanasema ugunduzi huo unaweza kuwasaidia kuelewa vizuri zaidi ni lini na wapi dinosaria walitokea kwa mara ya kwanza duniani.

Wanasayansi waligundua nini?
Screenshot_20260923-181008.png

Utafiti huo uliongozwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Bristol, ambao walichunguza kwa undani zaidi visukuku vilivyokusanywa nchini Tanzania zaidi ya miaka 60 iliyopita.

Wanasayansi walichunguza mabaki hayo, yaliyohifadhiwa katika Jumba la Makumbusho la Historia ya Asili huko London, na kugundua kwamba yalikuwa ya aina ya kiumbe aliyekula mimea aitwaye dicynodont.

Kwa usahihi zaidi, mabaki hayo yalikuwa ya Dinodontosaurus, aina ya kiumbe wa kabla ya historia ambaye hapo awali alikuwa amepatikana Amerika Kusini pekee.

Uchunguzi zaidi ulionesha kwamba visukuku vya Tanzania vilikuwa vya spishi ambayo haikuwahi kujulikana hapo awali, ambayo watafiti waliipa jina Dinodontosaurus isiyavamanda.

Wataalamu wanasema ugunduzi huo ni muhimu kwa sababu miamba ambako Dinodontosaurus alipatikana pia imetoa baadhi ya visukuku vya kale zaidi vinavyodhaniwa kuwa vya dinosaria.

Kwa kuwa sasa Dinodontosaurus amepatikana Tanzania na Amerika Kusini, wanasayansi waliweza kubaini kwamba miamba yenye visukuku hivyo ina takribani umri sawa.

Mwandishi mkuu wa utafiti huo, Hady George, kutoka Chuo Kikuu cha Bristol, alieleza: "Hili linasaidia kuthibitisha kwamba visukuku vya kale zaidi vinavyodhaniwa kuwa vya dinosaria kutoka Tanzania huenda si vya zamani zaidi kuliko vile vya Amerika Kusini, hivyo kuboresha uelewa wetu wa ratiba ya asili ya dinosaria."

Timu hiyo iliongeza kwamba, kutokana na ugunduzi huo, huenda wanasayansi wakahitaji kutathmini upya ni lini na wapi dinosaria walianza kutokea.
 
Kuna watu niliwahi kuwaeleza kuwa; huenda ile bustani ya Eden ya kwenye simulizi za kale ndiyo sasa hivi inajulikana kama nchi Tanzania.

Wanatheolojia wakiacha uvivu wa kufanya utafiti wa kina, naamini miaka ya mbele watakuja kukubaliana na hoja yangu.
 
Hii habari Nzuri lakini Bado haijitoshelezi
 
Hivyo visukuku vya miaka 240 millioni mbona havifikii visukuu vya Hamis kigwangwalai vyenye miaka 590 millioni tulivyogundua sisi na watafiti kutoka Oxford mwaka wa 2018?
 
Huu ni Uongo, hakuna Skull inaweza kuwepo kwa miaka 240Million years...hata ingetengenezwa kwa material ya brass au aluminium sembuse mifupa inayooza na kuisha
Hivi wanajua miaka Laki 1 iliyopita ina umbali upi? Je miaka Million 1? Je Mil 240 Sheikh?
 
Huu ni Uongo, hakuna Skull inaweza kuwepo kwa miaka 240Million years...hata ingetengenezwa kwa material ya brass au aluminium sembuse mifupa inayozza na kuisha
Hivi wanajua miaka Laki 1 iliyopita ina umbali upi? Je miaka Million 1? Je Mil 240 Sheikh?
Acha tunywe tu hii kahawa japo imewekewa sukari
 
Huu ni Uongo, hakuna Skull inaweza kuwepo kwa miaka 240Million years...hata ingetengenezwa kwa material ya brass au aluminium sembuse mifupa inayozza na kuisha
Hivi wanajua miaka Laki 1 iliyopita ina umbali upi? Je miaka Million 1? Je Mil 240 Sheikh?
Inawezekana. Kama conditions za Fossil preservation zikiwa met.
 
Inawezekana. Kama conditions za Fossil preservation zikiwa met.
I trust in science, bt for 240 Million years ago events, nahisi nitakuwa wa mwisho kuamini
Hivi ujue hata existance tu ya Dinosaurs ni mjadala? Walikuwa wanaishinkwa kula Tembo, faru n.k na ni mamilioni ya miaka kabla ya Binadamu kuwapo Duniani....kwmb ni mazingira tu yaliyowaondoa? Ni njaa? Tembo na wanyama wengine wakubwa waliisha? 🤣
 
Huu ni Uongo, hakuna Skull inaweza kuwepo kwa miaka 240Million years...hata ingetengenezwa kwa material ya brass au aluminium sembuse mifupa inayozza na kuisha
Hivi wanajua miaka Laki 1 iliyopita ina umbali upi? Je miaka Million 1? Je Mil 240 Sheikh?
Sasa si wamefanya utafiti wa Kisayansi wamegundua ni miaka milioni 240 iliyopita, kwani dunia haikuwepo huo muda 😅😅
 
Sasa si wamefanya utafiti wa Kisayansi wamegundua ni miaka milioni 240 iliyopita, kwani dunia haikuwepo huo muda 😅😅
Sio kila historia ina ukweli, kwa mfano habari ya kuwepo kwa Dragons zamani na kwamba walikuwa ni wanyama wanaotoa moto
Wewe unaamini Dragons walikuwepo?
 
Sio kila historia ina ukweli, kwa mfano habari ya kuwepo kwa Dragons zamani na kwamba walikuwa ni wanyama wanaotoa moto
Wewe unaamini Dragons walikuwepo?
Dragons wako kwenye fairy tales tu. Hakuna fossil au archaeological evidence kuwa dragons walikuwepo na hata Science haijawahi kusema Dragons waliwahi kuexist
So siamini kuhusu uwepo wa Dragons
 
Back
Top Bottom