Mnyika anaipaisha Tanzania kidemokrasia mbele ya IPU

Real?

Kwanza wabunge wa IPU walishangazwa kuona speaker wetu ni mzungu (Zungu) hana rangi nyeusi kama Tulia Akson. Wamegundua Tz hakuna hata ubaguzi wa rangi, dini, jinsia wala makabila.
 

Kuna watu mnapata ela kirahisi sana dah

So kwa hayo maandishi ela imeingia
 
Umeandikia Nini sasa. Hiyo IPU walifanya mkutano hapa mwaka Jana na Samiah alikuwa mgeni rasmi. Pia lazima ujue Rais wa IPU ni Mtanzania hivyo anatumia influence yake.
Hoja dhaifu, hata kama wewe una ushawishi huwezi kuwashawishi wabunge wa dunia wakusanyike mahala ambapo sio salama kwao. Nchi zao (hasa nchi za Magharibi) haziwezi kuruhusu wabunge wao waende nchi ambayo wana ugomvi nayo, sio salama na haina demokrasia.

Ukweli hii kitu imewaumbua wale wote waliokuwa wanaitishia Tz na EU, Marekani, misaada, ICC, na ujinga mwingine. satellites zote za dunia zinaimulika Arusha, Tanzania.

Tuombe Mungu wageni wetu wote warudi salama kwao wakasimulie nini wamekiona Tz, Ngorongoro, Serengeti, Kilimanjaro, Zanzibar, nk.
 
Hizi picha hakuna inayoonyesa kuwa imetoka Tz. yaani wote hawa hakuna hata mmoja mwenye utambulisho wa tz hata japo fulana ya timu ya Simba au Yanga au Azam au ushanga mkononi wenye rangi za bendera ya Tanzania?. Watanzania sio wajinga wa kiasi hicho. Hapo unajitekenya na kucheka wenyewe.

Wale waliokufa Oct29 walikufa kizembe sana kwa kudanganywa na chadema kuwa wanaweza kuuzuia uchaguzi wa Kikatiba nchi nzima. Pia waliambiwa waiangushe serikali ili chadema kuleta mabadiliko ya uongozi nchini, kazi ambayo haikuwa SMART (Specific, Measurable, Achievable, Realistic and Time bound). Mafisimaji walijificha magerezani wakisubiri watoto walete mabadiliko. Sasa hivi vijana wamekufa wakati wao wanadunda mitaani na wengine wakitafuta loopholes za kisheria kukana walichofanya.
 
Umeandika ukumah
IPU bado wapo, itisheni press nyingine tafadhali, na wengine andamaneni japo kidogo tu na mabango yenu kufikisha ujumbe wenu. Ukimuona zumbe msalimie na kumwambia kero zako hapohapo.

Serikali pia imepata muda muafaka na watu sahihi wa kuwaambia na kuwaonyesha Tanzania.
 
Mkuu Mtoa Mada,
Nimesoma kwa umakini uchambuzi wako, lakini una shida kubwa moja: unachanganya diplomasia ya ukumbi wa mkutano na hali halisi ya uwanja wa siasa wa ndani (field reality). Kitendo cha Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, kuzungumza na kukosoa serikali mbele ya ujumbe wa IPU hakijathibitisha uwepo wa "demokrasia ya kiwango cha dunia" nchini Tanzania, bali kimethibitisha ujasiri wa upinzani kutumia kinga ya jukwaa la kimataifa kufikisha kilio cha wananchi.
Naomba nikujibu hoja zako kwa hoja kupitia mambo makuu manne (4) yafuatayo:
1. Kuhusu IPU Kuja Tanzania na Suala la Usalama
Mkuu, kufanyika kwa mkutano wa IPU Arusha siyo "cheti cha kusafisha" (endorsement) rekodi ya haki za binadamu ya nchi mwenyeji. IPU ni chombo cha kidiplomasia ambacho hufanya mikutano yake hata kwenye nchi zenye migogoro mikubwa au mifumo migumu ya kiimla ili kuhimiza mabadiliko. Kwa muktadha wako, IPU imewahi kufanya mikutano yake mikubwa nchini Rwanda (2022) na Angola (2023)—nchi ambazo ripoti zote za kimataifa zinajua mnyukano wao wa kisiasa. IPU inakuja kwa sababu ya usalama wa kijiografia na hadhi ya nchi kidiplomasia, siyo kwa sababu nchi husika haina makovu ya kidemokrasia.
2. Kitendo cha Mnyika Kukosoa si Fadhila ya Serikali, ni Kinga ya IPU
Unadai kuwa jambo hili haliwezi kufanyika Rwanda, Uganda, au Congo na kwamba lipo Ulaya tu. Huu ni upotoshaji. Kwanza, Mnyika hajazungumza kwenye jukwaa la ndani la CCM; amezungumza ndani ya mkutano wa IPU ambako kisheria na kidiplomasia kuna kinga ya kimataifa (diplomatic immunity). Serikali isingeweza kumzuia au kumkamata ndani ya ukumbi huo bila kusababisha mgogoro mkubwa wa kidiplomasia mbele ya wabunge wa dunia. Uhuisho wa demokrasia haupimwi kwa uhuru wa mpinzani akiwa ndani ya ukumbi wa kimataifa, bali unapimwa kwa nini kinamtokea baada ya wajumbe hao kuondoka na kurudi kwao.
3. Hoja ya Kujilinganisha na Nchi "Zilizofeli" (Rwanda na Uganda)
Kusema "huwezi kuona jambo hili Rwanda au Uganda" ni kujipongeza kwa kupita kiwango cha chini sana cha kimaadili (low bar). Tanzania tangu enzi za Mwalimu Nyerere imekuwa kinara wa diplomasia na utulivu; hatuwezi kuanza kujilinganisha na nchi zenye mifumo ya kiimla ili tuonekane tuna afadhali. Hata hivyo, kwenye nchi kama DRC (Congo), pamoja na changamoto zao zote, viongozi wa upinzani kama Martin Fayulu na Moïse Katumbi wanazungumza, wanakosoa serikali hadharani mbele ya jumuiya za kimataifa, na vyama vyao havifungiwi wala viongozi wao hawashtakiwi kwa uhaini kila kukicha.
4. Uhusiano wa Amani, Maendeleo na Kesi ya Uhaini
Mwisho kabisa, hoja yako inajigeuza yenyewe (self-defeating). Huwezi kusifu uwepo wa "uhuru wa kusema bila kukamatwa" huku kwa wakati huohuo kiongozi mkuu wa upinzani, Tundu Lissu, akiwa gerezani akikabiliwa na mashitaka ya uhaini kwa sababu tu ya maneno aliyoyazungumza kwenye hotuba yake. Amani ya kweli (positive peace) siyo tu kutokuwepo kwa milio ya risasi barabarani, bali ni kuwapo kwa haki, utawala wa sheria, na kutokuwepo kwa hofu ya kutekwa au kubambikiwa kesi kwa wanaotoa maoni mbadala.


Hitimisho:
Mnyika hajaipaisha serikali kama unavyoamini, bali ametumia fursa hiyo kuonyesha ulimwengu taswira halisi ya nchi yetu. Ni ukweli usiopingika kuwa, kwa macho ya kiushabiki na 'uchawa' yenye upofu wa kiitikadi, unaweza kuona andiko lako lina ukweli; lakini kwa macho ya watu wenye akili timamu na upeo wa kiuchambuzi, Katibu Mkuu John Mnyika ameiweka uchi mifumo yetu ya utawala mbele ya jumuiya ya kimataifa. Amethibitisha kuwa Tanzania ina taswira nzuri ya nje (facade) lakini ndani kuna mgogoro mzito wa kidemokrasia na kisheria unaopaswa kutatuliwa badala ya kufichwa chini ya zulia.


 
Ulisoma Hadi la ngapi dada
 
Umepuyanga kaka, Kuna mikutano mingi sana ya kimataifa imefanyikia Rwanda, lakini hakuna mtu, kundi wala chama huko Rwanda kina ubavu wa kuitisha maandamano au press ya kuikosoa serikali, viongozi, na kiongozi mkuu Rais Kagame wakati mkutano ukiendekelea kama alivyofanya Mnyika na chadema kwa Tanzania na IPU wakiwepo.

Kuna wazungu kwenye mkutano huu ambao ni mara yao ya kwanza wanafika Tanzania/Afrika. Wamekuwa wakisikia negatives tu kuhusu Tanzania kupitia Lissu na watu wengine wa chadema. Sasa wako hapa wenyewe wanaona namna watu walivyokuwa na furaha wakiwa bize na shughuli zao mbalimbali huku kazi za ujenzi wa nchi ukiendelea. Wanashikwa na butwaa kuona matunda fresh kabisa, supermarkets, barabara, majengo marefu, vyakula vingi, makanisa na misikiti watu wakiishi kama vile wao wanavyoishi kwao.

Hawashangai kusikia Mnyika akibwabwaja kuhusu kasoro za watawala kwani hata huko kwao wabwabwajaji wapo.

Hakuna nchi iliyomaliza kero na shida zote za wananchi wake, kule ufaranza wanafunzi wamepamba moto. Kitu ambacho Mnyika ameisaidia dunia na wajumbe wa IPU ni kufuta uongo kuwa kama ukiikosoa serikali na viongozi wa serikali unatekwa, unashitakiwa na unauliwa. Mnyika ameikosoa serikali, amewakosoa Rais Samia, Tulia Akson, Azzan Zungu na Waziri Mkuu kuwa wanasema uongo na wameua watu; sasa wanasubiri kuona kama atatekwa, atashitakiwa au kuuliwa baada ya kufanya ukoaji huo.

Hii imewapa picha kuwa kumbe hata hao waliouliwa Oct29 walifanya zaidi ya kukosoa serikali na viongozi, walienda mbali zaidi kutaka kuiangusha serikali na ugaidi wa kuharibu miundombinu ya serikali. Bila shaka wataonyeshwa vitu walivyoharibu pale Arusha kama bado vipo.

Kwahiyo kaka hoja zako sizichukui kwakuwa viongozi wengi Afrika huwezi kuwakosoa kama alivyofanya Mnyika. Hata JPM tu asingeruhusu Mnyika afanye vile.
 
Huu mkutano si kikao cha kifamilia, anayemaliza urais ndiko kikao kitafanyika.
 

Istoria ya Rwanda na Tanzania unaona zinafanana?
 
 
Huu mkutano si kikao cha kifamilia, anayemaliza urais ndiko kikao kitafanyika.
Hebu kuwa na disiplini basi na wazungu. Wazungu wana ile kitu wanaita "safety first". Wanajali usalama wao na maslahi yao kwanza mengine ndiyo yafate.

Kupata urais wa IPU sio an automatic thing, sio mzunguuko. Kwanza unajua namna/kwanini Tulia Akson aliupata?

Unajua kwanini Prof. JANABI alipata kule UN?

Unajua Tanzania Tz inawania uwakilishi kule UN, kwanini Afrika imekubali kutuunga sisi mkono?

Kuichafua Tz na kumchafua Rais Samia lazima utaanza wewe kujichafua kwanza. Yuko slow but powerful.
 
Bahati mbaya kwenu ni kuiona dunia nzima ikiwa nyuma ya Samia. Rais Magufuli alisema ukishindana na mwanamke utashindwa wewe.

Ni kazi ngumu sana kwa mwanamke kuwa Rais hata huko ulaya na Marekani. Hiyo ni agenda ya wanawake wote duniani kuungana dhidi ya mfumo dume wa dunia. Ndiyo maana dunia inamuona Lissu na chadema kama watu wanaonyanyasa wanawake, hawatafua dafu kimataifa. Dunia yote inaufahamu uhusiano uliopo kati ya Rais Samia na Lissu, haiamini kama Samia anaweza kumuonea Lissu kutokana na uhusiano wake na Lissu kabla ya kukamatwa. Hawaamini kama Samia anaweza kuua watu wake kipumbavu tu.

Chadema hakuna watu wenye akili za kuchagua moments, wanabuluzwa na Lissu kama watoto wasioweza kusema no tujaribu hivi au vile.
 
 
Hiyo taasisi ni ipi tena, Ni taasisi ya kuzuia xenophibia au nini?

Tuache habari za kuokoteza mitaani. IPU ni chombo kikubwa sana chenye uwezo mkubwa wa kupata, kutafuta, kuchakata na kufanyia kazi taarifa. Wajumbe/wabunge wake wako hapa nchini. Taarifa waliyonayo ni kwamba Rais mwanamke alitaka kupinduliwa na wanaume wasiotaka kuongozwa na mwanamke.

Habari imeishia hapo.
 
Hii nchi siyo ya baba yako, siwapendi machokoraa wanaopenda dharau.
 
Hii nchi siyo ya baba yako, siwapendi machokoraa wanaopenda dharau.
KOsa lenu ni kuichoma nchi yetu kama ya mama yenu. Hamna tofauti na wale makahaba 2 waliokuwa wakigombea mtoto kila mtu akidai ni wake, hadi pale Nabii Suleimani alipoamua kesi. Kahaba ambae mtoto hakuwa wake alikubali mtoto akatwe vipande viwili (auliwe) ili wakose wote.

Kama unaipenda Tanzania huwezi kuochoma moto miundombinu yake na ajira za watanzania wenzako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…