Uhuru unatakiwa uanzie ndani ya chama... viongozi wa ngazi za juu wa chama waache kuhodhi mamlaka na demokrasia ya wanachama wake kufanya lililosahihi bila kuathiri katiba ya nchi, sheria na kanuni zilizopo.
Mfano wa kwanza, kitendo cha viongozi wa chama kuwanyima haki wanachama kugombea nafasi za uenyekiti serikali za mitaa kwa uchaguzi uliopita kwa sababu walizozisababisha wao (viongozi wa juu wa chama) kwa kushindwa kuwandaa wanachama vyema namna ya ujazaji fomu za kugombea, ni kitendo cha kupoka uhuru. Ili kuonyesha dhamira halali na sahihi ni lazima chama ki- tembelee yale kinayozungumza (Walk the Talk).
Mfano wa pili, kitendo cha kuwanyima haki wagombea nafasi ya uenyekiti wa chama kujieleza kwa muda sawa na wengine huku akipendelewa mgombea mmoja kujieleza kikampeni mara nyingi zaidi ya wenzake kwa visingizio mbalimbali...ni ukosefu wa uhuru ndani ya chama. Chama kiWalk the Talk.
Katibu Mkuu wa chama arekebishe hayo kwanza kwenye chama chake ndiyo aje kwenye jukumu hili lake analojipa la kufikirika.