Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, leo Juni 20, 2026, ameweka msimamo mkali mkoani Ruvuma na kukitenga chama hicho na vuguvugu la maandamano yanayodaiwa kupangwa na wananchi mitaani ifikapo Julai 7 (Saba Saba), akisisitiza kuwa chama chake hakijapanga ratiba hiyo.
Pia Soma Kihongosi: CHADEMA wamefanya vikao vya siri ili kuhamasisha vurugu kupitia maandamano wanayoratibu
"Polisi anasema kuna watu wanaandaa maandamano na kudai Chadema inapanga kufanya vurugu, lugha yao inafanana na msemaji wa CCM. Sisi hatujafanya vikao vya vurugu. Sheria inaruhusu raia au vikundi kuandamana, lakini kwa upande wetu sisi msitupangie tarehe; Chadema tutaitangaza tarehe yetu wenyewe ya maandamano," amesema Mnyika.