Mnyika: Hekima iliyotumika kufuta kesi ya Mbowe, itumike kwa Lissu

Mnyika: Hekima iliyotumika kufuta kesi ya Mbowe, itumike kwa Lissu

Hapana.
Ni dhahiri wewe ndiye unayetaka kupotosha.

Mnyika anazungumzia "HEKIMA" juu ya mtu asiyekuwa nayo.

"HEKIMA" kama ilikuwepo kwenye kesi ya Mbowe; ambayo mimi bado nasema haikuwepo; haiwezi kutumika kwa kesi ya Tundu Lissu.

Jambo pekee lilo wazi bila hata ya kusubiri hiyo "HEKIMA" ni kumaliza kesi, ambayo tayari Tundu Lissu amekwisha wabwaga, na kila mwenye akili anatambua hivyo

Sasa hii "HEKIMA" tena inayoombwa na Mnyika ni ya kitu gani?

Sijapotosha popote kuhusu aliyosema John Mnyika; na nadhani hata yeye mwenyewe kama hakukusudia kusema alivyosema atakuwa anajutia kuwa angeyasema vinginevyo.

Mbowe alitoka jela moja kwa moja na kwenda ikulu kupanga maridhiano.
Sitegemei kamwe Tundu Lissu na yeye afuate njia hiyo hiyo eti kumetolewa "HEKIMA" na mtu asiyekuwa na chembe hata ndogo ya hekima.

John Mnyika ni kijana ninayemheshimu sana, tokea huko mwanzo wa nilipoanza kumfahamu.
Kauli hii hapa aliyoitoa juu ya "HEKIMA" haiendani kabisa na nimjuavyo kwa muda mrefu.

..nimesikiliza press conference ya Mnyika.

..mara kadhaa ktk press hiyo ameweka msisitizo kwamba TL hana makosa, na aachiwe bila masharti.

..nadhani kichwa cha habari cha mada hii kinapotosha uhalisia wa press conference ya Mnyika.

..infact Cdm wametoa TAMKO ambalo limesomwa na Katiba Mkuu, na hilo ndilo linalopaswa kuzingatiwa.

..suala la " hekima " Mnyika alisema wakati akijibu maswali na halipo ktk tamko.
 
..mara kadhaa ktk press hiyo ameweka msisitizo kwamba TL hana makosa, na aachiwe bila mashart
Ninakubaliana na hili moja kwa moja.; lakini ule mfano wa Mbowe aliotumia, hata huko kwenye maelezo yake ndiyo iliyoleta sintofahamu.

Hakuna "HEKIMA" yoyote inayoweza kutumiwa kuelezea kuachiwa kwa Mbowe, na mbaya zaidi kuihusisha na hii ya Tundu Lissu.

Tuliachie hapa hili, siyo jambo la muhimu sana.
Naamini hata John Mnyika mwenyewe hakunuia kueleweka kama ilivyojitokeza hivi.
 
Mbona ilikuwa wazi toka mwanzo? Tatizo la Chadema ni kuwa wanapenda sana kutafuta wachawi. Hata matumizi ya neno "hekima" sio controversial kama watu wanavyotaka kuligeuza. Chadema ni wepesi mno kuwa manipulated. Ndani ya Chadema kuna Fifth columnists ambao kazi yao ni kuwagawa. Kazi yao ni rahisi kwa sababu CDM inapenda mno conspiracy theories. Walianza na Mbowe, wakaja G-55, wakaja Heche na sasa Mnyika!

Amandla...
 
Mbona ilikuwa wazi toka mwanzo? Tatizo la Chadema ni kuwa wanapenda sana kutafuta wachawi. Hata matumizi ya neno "hekima" sio controversial kama watu wanavyotaka kuligeuza. Chadema ni wepesi mno kuwa manipulated. Ndani ya Chadema kuna Fifth columnists ambao kazi yao ni kuwagawa. Kazi yao ni rahisi kwa sababu CDM inapenda mno conspiracy theories. Walianza na Mbowe, wakaja G-55, wakaja Heche na sasa Mnyika!

Amandla...
Hata uligeuzegeuze namna gani, swala la Mbowe halibadiliki. Hiyo ni historia isiyofutika katika historia ya nchi hii.
 
..disgrace kwa nani?

..mbona TL kaishawabwaga kwa utetezi wake?

..hakuna kesi pale na TL ameonyesha ktk kila hatua.

..how can TL be disgraced baada ya umahiri na ushupavu wote ule mahakamani?

Hangewabwaga leo Lissu angekuwa mtaani!!!
 
Back
Top Bottom