Salaam wana JF
Bila shaka kishindo na mwangwi wa kauli ya Katibu Mkuu wa CCM Daktari Bashiru Ally kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu vimesikika kwa uwazi mkubwa!
Bila kupepesa macho Bashiru amesema CCM itatumia dola kubaki madarakani! Zaidi anasema ni uzembe kushindwa kwenye chaguzi wakati CCM ina uwezo wa kutumia dola kubaki madarakani!
Kwa upande mwingine, Katibu Mkuu wa CHADEMA amejibu kauli ya Bashiru na CCM kuwa, kama CCM watatumia Dola, CHADEMA watatumia nguvu ya umma kuwaondoa CCM kwenye madaraka watakayoyapata kwa kutumia mabavu ya Dola!
Kauli ya Bashiru ni ya kujigamba na kudharau maamuzi ya wananchi kupitia sanduku la kura ikiwa yataikataa CCM isiendelee kuliongoza taifa hili! Pia ni ujumbe kuwa dola tuliyonayo siyo ya wananchi wote bali ya Bashiru na chama chake!
Kwa msingi huo CHADEMA kama chama mbadala wanalo jukumu kubwa la kuutisha Umma ili ukatae dhuluma inayopangwa na CCM dhidi ya haki ya umma kuchagua viongozi wanaowataka kidemokrasia!
Kwa umma uliojengwa katika hofu, umasikini na ujinga, siyo kazi rahisi kuupa umma ujasiri wa kupambana na CCM yenye mabomu ya machozi, virungu, risasi, magereza, wasiojulikana nk.
Dr Bashiru kutoka Jalalani hadi kuwa Katibu Mkuu wa CCM, haoni aibu kuisema hadharani mipango dhalimu ya kupoka mamlaka ya wananchi kwa kuwa sasa anakula na kunywa kwa anasa pamoja na mfalme!
Kwa kauli hizi za viongozi wakuu wa CCM na CHADEMA ni wazi kuwa thamani ya kura ya mwamanchi imepuuzwa mapema kabla ya kupigwa!
Je Umma wataweza kulinda na kutetea mamlaka yao yatakayoporwa na Dola kwa kutumiwa na CCM!? Majibu ya swali hili wanayo Watanzania wenyewe na ni suala muda!
CHADEMA, macho ya watanzania yanawatazama kwa matumaini makubwa ili muweze kuwaunganisha na hatimaye nia ovu ya CCM ya matumizi Dola katika uchaguzi mkuu ujao iweze kushindwa.