DPP anazo kwa sababu yeye ndie aliyeleta mashtaka. Committals ni makrabasha ambayo DPP anampa mtuhumiwa kumuelezea makosa anayoshitakiwa, kwa nini anashtakiwa na ushahidi uliomfanya DPP amfungulie mashtaka. Sasa ulitaka apelekewe kabrasha ambalo ameliandika mwenyewe. Mangula na wenzake walipewa kwa sababu alihoji wao kusema kuwa kesi ya Mbowe ni ya jinai.
Hawakufanya siri. Hizi ni public records na sio confidential records. Yaliyomo kwenye hizo committals ndio tunayasikia siku zote wakati wa uendeshaji wa kesi.
Ulikuwepo kwenye kikao cha Mbowe na Zitto? Lugha ya kusema hakupinga ni ya kisanii. Kwa nini hakusema alimuunga mkono na kumuomba aendelee na huo mpango? Mbowe anataka aachiwe na asiombewe msamaha. Kama Zitto alisema atasaidia ili aachiwe, kwa nini amzuie? Ingekuwa vinginevyo, Zitto angesema Mbowe alimuomba akamuombee msamaha kwa Mheshimiwa Rais.
Ndio. Wengi wao waliisha kaa ndani na hawakuwahi kuomba msamaha. Mahakama ndio zilikuja baadae kutupitilia mbali kesi zao kwa kuona hazikuwa na mashiko. Ilikuwa hivyo kwa Sugu. Ilikuwa hivyo kwa Lema. Ilikuwa hivyo kwa wakina Mbowe, Heche, Msigwa, Halima, na Esther ( kumbuka Mbowe alikuwa wa mwisho kutoka gerezani) . Ilikuwa hivyo kwa Mdude. Ilikuwa hivyo kwa Twaha. Na wengine wengi tu Hawa wote wana msimamo ndio maana mpaka leo wanawapigania watu wao walio ndani na wanadai haki itendeke kwa wale walioumizwa au hata kuuawa kwa sababu za kisiasa. Wakina Zitto walisema watu wao waliumizwa na wengine kuuawa lakini hamna kilichofanyika hadi leo kuwapatia haki zao.
Mradi gani wa European Union? Ni wajibu wa wakili kuonyesha dosari zote zinazojitokeza katika kesi ya mteja wao. Wao hawako pale kutaka fadhila za Jaji. Wanapigania haki za wateja wao hata kama wanahisi kuwa Jaji ameelemea upande mwingine. Na kumbuka yote haya yatahojiwa tena kama watakata rufaa. Hawawezi kukumbushia wakati wa rufaa kama hawakuhoji wakati wa kesi ya msingi. Mbowe ana familia. Ni matusi kusema kuwa familia yake inafaidika kwa yeye kuwa ndani.
Amandla...