Nadhani kwa hili Mnyika ameongozwa na hisia zaidi kuliko uhalisia. Wote tunajua kuwa Kabendera anakomolewa, lakini sioni kama ni jambo kubwa sana la yeye kulitolea tamko. Ni vyema Mnyika akajikita kwenye jambo kubwa kama la katiba mpya na hasa tume huru ya uchaguzi, kuliko jambo dogo la kihisia zaidi. Mnyika na cdm mnakwama wapi, mbona mnaelekeza nguvu kwenye tukio kuliko mambo makubwa ya msingi?
Tunahitaji jambo kubwa la msingi ambayo ni tume huru ya uchaguzi, hilo la kwenda kuzika, sawa ni suala sahihi lakini sio muhimu hivyo.