Mnyika: Tulipeleka barua za kufukuzwa uanachama Wabunge mara mbili

Mnyika: Tulipeleka barua za kufukuzwa uanachama Wabunge mara mbili

Kwani si walikata rufaa baraza kuu?!!! Je baraza kuu limekaa lini kuridhia kufukuzwa kwao? Tafadhalini JM zingatieni taratibu.

Ili ifahamike kama unajua unaloliongea na sio kudandia mambo, ni wangapi wamekata rufaa na wangapi hawajakata?
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema walieleka barua rasmi kulitaarifu bunge kuhusu kufukuzwa uanachama kwa wabunge 19 walioteuliwa kuwa wabunge wa viti maalum katika bunge la 12

Mnyika ametoa ushahidi huo leo, baada ya Naibu Spika wa bunge kusema kuwa hawana taarifa ya wabunge kufukuzwa uanachama alipokuwa akisikiliza hoja za mbunge wa viti maalum Jesca Kishoa

Barua ya kulitaarifu bunge kukoma kwa uanachama wa wabunge wa viti maalumu zilitumwa mara mbili tofauti ikiwa ni Desemba 1, 2020 na Desemba 19, 2020

View attachment 1761800
Kuna kamchezo hebu mnyika aweke hadharani barua alizoandikia bunge. Kama bunge walipata hizo barua kwa nini naibu spika kwa mara ya kwanza ndio amekanusha kupokea barua yoyote toka chadema?
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema walieleka barua rasmi kulitaarifu bunge kuhusu kufukuzwa uanachama kwa wabunge 19 walioteuliwa kuwa wabunge wa viti maalum katika bunge la 12

Mnyika ametoa ushahidi huo leo, baada ya Naibu Spika wa bunge kusema kuwa hawana taarifa ya wabunge kufukuzwa uanachama alipokuwa akisikiliza hoja za mbunge wa viti maalum Jesca Kishoa

Barua ya kulitaarifu bunge kukoma kwa uanachama wa wabunge wa viti maalumu zilitumwa mara mbili tofauti ikiwa ni Desemba 1, 2020 na Desemba 19, 2020

View attachment 1761800
Hivi humu JF chooni ni wapi? Kuna mijitu inakomenti kwa kudemka mpaka tumbo linavuruga. Mataga bwana.
 
Chadema hawaukubali uchaguzi wa 2020, sasa huyo spika waliomuandikia ni spika wa kenwood au panasonic. Maana spika kapatikana kwa uchaguzi wanaoukataa
 
Hapo kuna ujanja unafanywa na uongozi wa CHADEMA ili kuwazuga wanachama wao. hivi wewe hujiulizi kama kweli wana nia ya kuwafukuza mbona hawasikilizi hizo rufaa zao? Hao wanawake 19 wamewekwa kwenye suspense makusudi ili waendelee kuwa wabunge. Rufaa itasikilizwa baadae sana siyo hivi karibuni.
Hivi mtu akishitakiwa kwa wizi rufaa yake inasikilizwa akiwa huru au akiwa Lumande ?Kisheria Covid-19 hawakutakiwa kuwepo mbungeni mpaka rufaa yao isikilizwe.Je ikitokea wameshindwa pesa walizochukua watazirudisha? Ndugai katumia ubabe wa kijinga na bahati mbaya aliyekuwa anamuagiza kufanya huo upuuzi hayupo tena.
 
Back
Top Bottom