Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni: Katika Mgomo wa wafanyabiashara, kosa la Mwigulu Nchemba ni lipi?

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni: Katika Mgomo wa wafanyabiashara, kosa la Mwigulu Nchemba ni lipi?

point namba 2, nakubaliana nayo 100% kuhusu viwango ilo wataalamu wakae waone wanafanyaje , ila kusema iende kwenye diesel si sawa maana kuna watu wanatumia diesel na si walengwa wa hiyo kodi
 
Kuna sababu nyingi sana za kulaumiwa Mwigulu.

Wafanya biadhara mbona walisema moja wspo na ya msingi pale pale mkutanoni. Hujaisikia?

Nionavyo mimi ibinafsi, Mwigulu ana kiburi sana, amelewa madaraka.
 
Yeye ndio Top official kwenye hio sekta ya Kodi.

Ana impose na kufacilitate Kodi uchwara na tozo Kausha damu.

Ana wagroom TRA wafanya ukandamizi huo.

Badala kuwasikiliza wafanyabiashara sidhani kama anafanya hivyo maana ana madharau. Hadi aje kiranja wake kusovu hio ishu huoni kama mtu huyo kaharibu sana au gamemshindwa.

Mtu wa kukaa kwenge huo mkutano alipaswa awe rais wa mawe sio PM ila .

Wafanyabiashara wameona hawasikilizwi ndio maana wameomba PM waongee nae.

Never trust this dude huyu MAGU 2.0

Sio kweli acha uongo Hakuna jipya lililoletwa na Mwigulu sheria za kodi zinatungwa na kupitishwa na bunge
 
Mh waziri njoo chamber na siri nzito
968282129.jpg
 
Akome kujidai anatumia maneno ya shombo.

Binafsi bila nimefurahi sana walivyomchamba.
Jamaa walikuwa hawapepesi maneno,,wanalemgesha mule mule[emoji1787][emoji1787]
Eti dokta wa wapi wewe Mwigulu [emoji23][emoji23][emoji23]

Kuna mfanyabiashara gani anaakili kama lile limama akili zimejaa mavi tu
 
Nimesikiliza hoja za wafanyabiashara akiwemo huyo Fredy vunja bei,kwa kweli hoja zao hazina mashiko hata kidogo labda ile ya kutaka kila mfanyabishara kufanya clearance ya mzigo bandarini.

Hoja zingine zote hazina kichwa wala miguu,ni kutaka kuhalalisha faida kubwa tu.

Bila aibu hivi mfanyabishara gani awe na mtaji chini ya 5M halafu umiliki frame Kariakoo,huku sote tunajua frame ndogo tu Karikaoo kodi kwa mwezi sio chini ya 800K.
Wafanyabiashara wengi ni makanjanja wasio lipa kodi stahiki za Serikali wakishirikiana na wezi wa TRA.
 
Kama kawaida habibu mchange ushaanza uchawa wako wa siku zote
 
Madilu na PhD yake wafanyabiashara wamemwacha mbali kiufikiri, I think hizi wizara sijui uchumi, au biashara wawe wanateuliwa watu walio wazoefu na hizo biashara kuliko kuteua watu walio cremisha madesa na hawajui Hali halisi

Kweli akili yako ndogo watu wanapiga magoti awasaidie unasema amewaacha mbali yaani sheria zilipita bungeni ambako kuna wafanyabiashara na walizipitisha utasemaje wamemzidi akili
 
Huwezi kuwa mfanyabiashara ukaja kumtetea Mwigulu..
Mfumo WA Kodi WA kukadiria unaotoa mwanya Kwa watu wa TRA sio fair..
Mtu anakdiriwa Kodi milioni 350 wakati Kenya Kodi milioni 45 Kwa kontena Hilo Hilo...yote hayo ni policy..na usimamizi na Mwigulu ndo mhusika wa kubadilisha vyote...na kashauriwa kagoma ....

Wewe labda kakutuma uje umsafishe
mi nachoelewa waziri yupo chini ya Raisi, nani wa kumshambulia raisi kama alivoshambuliwa mwigulu hilo ni jambo jingine.. mfano waziri mkuu kapata sifa kemkem kwa baadhi ya watu ila si ndo huyu mzee wa kuunda kamati na mwishoe kamati imeundwa
 
Ns majibu yake anayowaambia watu hamia Burundi

Leo Cha moto amekiona[emoji1787]
Nimefurahi hadi nikapiga makofi.

Ungekua na akili ungesikitika kwa sababu walikua wanachamba hawaelezi wanataka nini kifanyike akili zenu Sawa tu wakinga wengi hamna akili shule kichwani tee
 
Unaweza kuthibitisha haya madai Yako?

Hayo unayiyasema TRA wameanza kuyafanya Waziri akiwa Mwigulu?

Lini hao Wafanyabiashara wamesema waliomba kikao na Waziri akafanga dharau? Au wewe Kwa shida zako binafsi ndio unasema hayo?

Muongo Muongo hana hoja
 
Hauijui historia kijana, ngoja nikuache ukiendelea kukaza fuvu.
Huyu Ramadhan Ntuzwe issue yake ilitokea around six years back kabla haujajiunga Jf

Sasa six years back Waziri wa fedha alikua Mwigulu Nchemba utawala wa nani huo kama sio ndugu yenu mfilisi watu
 
Ila nimependa wamemnanga sana kwa maneno ya kejeli maana yeye huwa anajidai bingwa wa maneno ya kukararisha.

Kuna mwamba anasema,unajitia Dokta,Dokta wa wapi wewe[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna wafanya Biashara yule kweli mwamba.
 
Wakuu Salam,

Naomba nitangaze maslahi, mimi ni mfanyabiashara, nipo Kariakoo, nje ya Kariakoo na mkoa wa Pwani.

Malalamiko yetu wafanyabiashara mengi ni justifiable, lakini hili la kumlaumu Mwigulu Nchemba bila supporting evidence is ungrounded.

Kuna watu wanatumia udhaifu wa migogoro ya sheria zilizopo kumgandamiza bila sababu. Mfano;

1. Hoja ya fine ya kutokutoa EFD recept sio ya leo, na hii ilipingwa sana na aliekuwa mbunge wa Muleba Anna Tibaijuka, nilishangaa sana yale mapendekezo, kama kawaida ya bunge letu, papatu papatu hoja ikapita ikawa sheria, kipindi hicho Mwigulu ni Waziri wa mambo ya ndani.

2. Hoja ya ushuru wa malori, Ndugu Chuki anaweza kuwa ana issues personal na Mwigulu na siwezi kuwaingilia, ila kodi ya 2.7M sio kubwa kama anavyodai, kumbuka kubeba ton nne au 10 hadi Mwanza ni zaidI ya 1.5M na hiyo ni non negotiable. Kutaka hiyo gharama iingizwe kwenye diesel ni ku shift tax burden to non beneficiaries, ambayo ni unfair taxing.

3. Hoja za registration of warehouse sio kitu kipya na wengi tumesajili nikiwemo, hoja za umiliki ni jambo jingine, labda tuseme issue ya With holding Tax ndio haijakaa sawa, lakini kulalamika kwamba tusisajili sio Sawa kabisa.

Kwenye ethical business ni lazima usajili store na ulipie usimamizi wake, ikiwa na vigezo vyote. Hii ni excuse ambayo kumlaumu nayo Mwigulu ni ku choose easy victim.

4. Hoja za task force zilikuwepo toka kipindi cha Mwendazake, kwamba tunasumbuliwa hili ni kweli na ni suala la kuweka utaratibu tu wa namna ya ku control, ambayo sikuona sababu ya kumzodoa mwamba vile.

5. Utitiri wa kodi kwenye biashara na mamlaka nyingi zinazosimamia jambo moja ni suala la kurithi na Mwigulu sidhani kama ni wa kulaumiwa 100% , issue hapo ni CCM kuweka na kuunda hizi taasisi kutafutia washkaji wao ulaji.

Kuna kila sababu ya kuunganisha taasisi nyingi sana ili kuondoa usumbufu.

Ni hayo tu, tumuhukumu Mwigulu kwa mengine lakini sio moja kwa moja kwa baadhi ya sheria ambazo amezikuta.
Sheria alizozikuta ambazo ni kero anaziacha ziendelee kuumiza ili nani aje kuziondoa.

Safari inaishia njiani anashuka kituo kinachofuata.

Mwigulu amesababisha mgomo wa kwanza wa wafanyabiashara nchini.
 
Binafsi nimekuwa napinga sana hili swala la kuleta chuki binafsi za Kisiasa Kwa mtu..

Hakuna anaweza kukupa majibu hapa isipokuwa ni upuuzi tuu..

Ukiangalia kinachoitwa mgomo hapo ni issue Zenye msukumo wa Kisiasa ndio maana eti Kodi akusanye mwingine,Rushwa aombe mwingine,Sheria za Kodi zitungwe na Bunge harafu aje kulaumiwa Mwigulu,inakuja?

Nimeuliza hili swala sijapata majibu Hadi Sasa hivi.
Uliza hilo swali tukujibu.

Mkuu it is a time Mwigulu kushuka kituo kinachofuata.

Dereva anamuona ni asset lakini ndiye mchomoa nati kwenye tairi za gari
 
Hakuna mfanya biashara anayeweza kuandika upuuzi ulioandika! Mtetee Bwana'ko ila usijivike ufanyabiashara.
Wewe unafanya biashara gani na ipo maeneo gani mkuu.
Embu eleza kosa la huyo Bwana ndugu mtaalamu.
 
Sheria alizozikuta ambazo ni kero anaziacha ziendelee kuumiza ili nani aje kuziondoa.

Safari inaishia njiani anashuka kituo kinachofuata.

Mwigulu amesababisha mgomo wa kwanza wa wafanyabiashara nchini.
Mkuu heshima kwako.

Kwahiyo tunakubaliana tatizo halikuanzia kwake.
 
Back
Top Bottom