Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi
Kama kawa, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi za Kwa Maslahi ya Taifa, zenye swali, hoja na majibu utaweka mwenyewe. Hoja ya leo ni kuhusu usikivu wa Rais Samia, hakuna ubishi ni msikivu, vipi serikali yake, ni serikali sikivu? Bunge lake ni Bunge sikivu, na Mahakama yake ni Mahakama Sikivu? Kama Rais ni msikivu, halafu serikali yake sio sikivu, Bunge lake sio sikivu na Mahakama zake sio sikivu, what does this mean, yaani inamaanisha nini?
Angalizo za Sifa za Kweli na Sifa za Kichawa Chawa. Siku hizi kila ukimsifu Rais Samia kwa mazuri yake yoyote, unanyooshwe kidole cha uchawa kuwa unasifu kutafuta shavu, hivyo ni sifa za kichawa, naendelea kusisitiza humu mimi sio chawa wala sitafuti shavu, nikisifu ni sifa za Kweli na hili sio tuu nimelisema humu, hadi nimeliandikia makala. Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!
Usikivu wa Rais Samia
Sote ni mashahidi wa utendakazi wa mtangulizi wake hali ilikuwaje kwenye baadhi ya maeneo, Rais Samia alipoingia aliangushiwa vilio kila sehemu, karibu kila kilio japo huwa hajibu kuwa nimesikia, utashuhudia tuu vitendo vya kuwaita wahusika kusemezana na mara mambo kutekelezwa.
Amefanya mengi nikianza kuyataja hapa moja moja, tutakesha, ila naomba nikutajie vilio vichache na matokeo yake.
Rais Samia alipoingia, niliandika makala mfululizo za kilio cha haki Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
Baada tuu ya Makala hii, DPP mpya akaingia kazini na kuanza kufanya mambo, Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana! Hongera sana, kazi umeianza vizuri. Sasa haki sio tu inatendeka, inaonekana! Kazi Iendelee…
Kwa vile ofisi ya DPP kwa mujibu wa Katiba yetu ni an independent office, wale mnaoamini ni DPP, endeleeni kuamini, sisi wa jicho la tatu tunamjua ni nani!, apewe tuu maua yake!.
Ukaja mtanziko wa kisiasa, kiongozi mkuu wa chama pendwa akaburuzwa kwa Piloto, watu tukamuombea msamaha Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?
mara paap!, DPP kafuta kesi kwa nolle, kiongozi kaachiwa!, wale mnao ni DPP ndiye aliyeifuta ile kesi kwasababu kwa mujibu wa Katiba yetu ni DPP pekee ndie mwenye mamlaka ya nolle, endeleeni kuamini ni DPP, sisi wa jicho la tatu tunamjua ni nani!, apewe tuu maua yake!
Naendelea na mada hii ya usikivu wa Rais Samia kwenye hoja mbalimbali. Leo naomba kuzungumzia usikivu wa Rais Samia kwenye issues za TRA.
Alipoingia ilikuta TRA na wafanyabiashara ni paka na panya. TRA wanaingia kwenye account za wafanyabiashara na kuchota fedha zote wanazozikuta kwenye account as if ni account yao na fedha ni zao. Wengi walifunga biashara, na wale wenye uwezo mkubwa, walihama nchi.
Mama akawaambia TRA tabia hiyo, wasamehe madeni ya nyuma, "wapeni raha wafanyabiashara wafanye biashara zao!, wasiingilie account za watu, na wakae chini wasemezane na wafanyabiashara na sio kukomoana.
View: https://youtu.be/QRZFo7dDEgM?si=Kv5qfBdcnyUM0HXa
Kwa vile mimi sidaiwi kodi, sijui kama kweli kuna wafanyabiashara waliosamehewa madeni yao ya nyuma.
Sasa TRA, wameanza tena ile tabia mbaya ya ule mtindo wa kuingilia account za watu, kuzifunga, kukomba every cent wanayoikuta as if hiyo account ni yao!.
Tena na hizi Benki zetu... we acha tuu!.
Vita kati ya TRA na wafanyabiashara biashara kuhusu kodi mbalimbali imekuwa ikiendelea, mwisho wa siku ni wafanyabiashara kutumia silaha yao ya mwisho, kufanya migomo ya kufungua maduka. Huu mgomo wa mwisho, umemng'oa CG wa TRA, Kidata!.
Rais Samia alivyo msikivu, sasa ameunda Tume ya kuangalia issues za kodi na sisi wa kupongeza tumeisha mpongeza. Asante Rais Samia Kumteua Prof. Assad, ni Mkweli, Atakusaidia Sana Kukuambia Ukweli, Tatizo Viongozi Wengi Hawapendi Kuambiwa Ukweli, Je Uko Tayari?.
Inaendelea
Paskali