Mnyonyaji 'Panjuani Kibyongo' anatudanganya kaweka 20B halafu tunasajili akina Kapama na Okwa na tunataka kushindana na watu makini kama Yanga SC?

Mimi simu yangu aioneshi picha vizuri ila najibu kulingana na komenti za watu mimi hapo nashauri uyo mtoto aliye fanyiwa icho kitendo akimbizwe hospitali na huyo mtuhumiwa akamatwe afungwe kifungo cha maisha mana ataendelea kuharibu watoto wengine kama watamuacha huru.
 
Ameweka 20B ila mbumbumbu a.k.a mchwa mmesosomola zote,naye kaamua kususa😄
 
MO kachukua steak ya asilimia 49%na nyie jichangeni vipesa vyenu vya ngama muweke pesa hio ya asilimia 51% ili mambo yawe sawa.
Sisi tulikuwa tunamiliki 100%
.Ponjoro amekuja anataka ubia achukue 51% sisi atuachie 49% .Tukasema hapa, itakuwa kinyume chake.
Ponjoro amekubali kutoa bilioni 20 ili kulipia 49%.
Sisi tuweke hela ya 51% kulipia nini wakati hizo share tunazimiliki sisi wenyewe?
Au sijaelewa, timu ilikuwa haina wenyewe, ili iwe na wamiliki inabidi muwekezaji aweke mpunga na wanachama waweke mpunga?
 
Ni sawa kabisa, hizo 51% ndio hiyo timu,
Ni sawa na mwekezaji akiingia ubia na mwenye nyumba, mbia atatoa hela ajenge na mwenye nyumba atatoa kiwanja
 
Mkuu kuna watu wanajifanya hamnazo! Yaani ulitaka Simba(wanachama) aweke pesa kwa ajili ya 51% ya hisa wakati yeye ndo kauza 49% ya hisa zake kwa Kanjibai? Wanaouliza kuhusu hizo billion 20 za ununuzi wa 49% ya hisa wako sahihi, aseme ziko wapi au yale madeni aliyokuwa anaisaidia Club kabla ya kuwa mwanahisa ndiyo kaamua kukata juu kwa juu? Ili nalo litazamwe maana Kama kulikuwa hakuna makubaliano hayo basi ni utapeli mtupu.
 
Genta kama genta salute Sana shemeji yangu... Umenena mkuu...huna unafiki kabisa..
 
Viongozi wa Simba mafala sana alafu wanakuja na vidrama vya kijinga oooh mara Simba queen imepata udhamini wa kiasi Fulani, mara vunja bei kaja sijui na nn. Hizo danganya toto haziwezi kuleta ubingwa. Wekeza pesa update pesa. Nje ya hapo n bahati ya mtende. Huyu Mo utadhani sio mwanauchumi the way anavyoiendesha timu
 
Pumba tupu. Unalipa mishahara wewe?
 
Punguza jazba. Tatizo mmeanza ushabiki juzi. Kama umejaa upepo kiasi hiki, vipi wenye Manchester United yao, Barcelona au Chelsea wafanyeje? Aliyekuambia kuwa simba itakuwa kwny peak muda wote ni nani?
 
Umeanza tena! Mwaka huu unalo. Suluhisho ni wewe kuanzisha timu yako wewe. Iwe yako, usajili kocha na wachezaji unaowataka ili uchukue ubingwa miaka yote ya uhai wa taifa letu. Vinginevyo utaokota mkopo.
 
Kitu ambacho haufahamu hio 51% ndio Simba yenyewe (brand) unataka waweke nini tena?
 
Simba ilikuwa inajiendesha kwa mfumo wa michango ya wanachama,wakabadili katiba na kuwa kampuni wakasajili Brela,wakauza steak ya asilimia 49%kwa muekezaji.

Wanachama wakabaki na 51% ambazo zitagawiwa kwa wanachama wote ambao walikuwa wanachama hai kabla ya mfumo kubadilika.

Baada ya hapo watabadilika automatic kutoka kuwa wanachama na kuwa wanahisa, hivyo watasajili kampuni yao na kujiunga kwenye soko la hisa na mitaji ili kukuza mtaji,hivyo hio steak yao ya 51% lazima iingie sokoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…