Asante mzee Kwa elimu nzuriMnyororo wa umaskini (Generational Poverty) siyo tu hali ya kukosa fedha bali ni mfumo wa kimaisha, kifikra, na kijamii unaorithishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Katika familia na ukoo
umaskini huu hufanya kazi kama gereza lisilo na kuta, ambapo watoto huzaliwa na kukuta madeni, ukosefu wa fursa, na mitazamo inayowafunga wasifikie ukubwa wa ndoto zao huku wengi wakiishia pabaya
Ninini asili ya hiki kitu kibaya kabisa?
.(Vyanzo)Urithi wa Madeni na Majukumu:
Katika koo nyingi, mtoto anayefanikiwa kidogo hubeba mzigo wa ukoo mzima. Badala ya kuwekeza ili kukuza utajiri, anatumia kila anachopata kutatua dharura za ndugu, jambo linalomrudisha kwenye umaskini uleule alioukuta.
.Ukosefu wa Elimu ya Fedha:
Koo nyingi huzungumzia jinsi ya "kutafuta pesa" lakini siyo jinsi ya "kuitunza na kuikuza." Maarifa ya uwekezaji hayarithishwi, badala yake inarithishwa tabia ya kutumia kila kinachopatikana.
.Mazingira na Malezi:
Mtoto anayekua akiona umaskini kila siku, anajifunza "saikolojia ya kunusurika" (Survival Mode). Hawezi kupanga mipango ya miaka 10 ijayo kwa sababu akili yake imeshulika na jinsi ya kupata chakula cha leo jioni tu huku kesho ikiwa ni mapambano mengine ya kudra!
ATHARI ZA MNYORORO HUU KWENYE UKOO
.Kifo cha Vipaji:
Watu wenye akili na vipaji vikubwa ndani ya ukoo huishia kufanya kazi zisizo na tija ili tu wapate mkate wa kila siku.
.Migogoro ya Kifamilia: Umaskini hupunguza uvumilivu na upendo. Mara nyingi koo maskini hukumbwa na migogoro ya ardhi kidogo au mali ndogo zilizofifia, hali inayozalisha chuki, ugomvi na visasi
.Hofu ya Kuthubutu:
Ndani ya ukoo, mtu anayetaka kufanya kitu tofauti (kama biashara mpya au kwenda mbali kutafuta fursa) mara nyingi hukatishwa tamaa kwa kuambiwa "kwetu hakuna aliyewahi kufanya hivyo akafanikiwa." Hili limewatokea wengi sana
JE NI MBINU ZA KUVUNJA MNYORORO HUU?
Ili kuvunja mnyororo huu, ni lazima kizazi kimoja kikubali "kuteseka" na kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu ili kutengeneza njia ya wengine..
.Kuwekeza kwenye Elimu ya Kisasa
Siyo tu shahada za darasani, bali ujuzi (skills) zinazohitajika sokoni na elimu ya fedha.
.Kujenga Utamaduni wa Akiba na Uwekezaji
Familia lazima ianze kuweka akiba ya pamoja au kuanzisha miradi ya ukoo (Family Trusts) badala ya kutumia kila kitu kwenye sherehe au dharura.
.Kubadili "Simulizi za Ukoo": Badala ya kusimulia historia ya kushindwa, anzeni kusimulia na kuenzi hatua ndogo za mafanikio.
.Ni lazima kujenga utamaduni wa kuinuana (mentorship) ndani ya ukoo.
Nimalizie kwa kusema mnyororo wa umaskini haukatiki kwa bahati mbaya au kwa maombi pekee ama uchawi; unakatwa kwa maamuzi magumu na nidhamu ya ya hali ya juu, Inahitaji mtu mmoja ndani ya familia anayesema: "Umaskini huu unaishia kwangu."
Na Huyo mtu anaweza kuwa ni wewe.💪🏿🔥 SIMAMA SASA SAFARI YAKO YA UKOMBOZI NDIO IMEANZA!
Thank you brotherHii mada ni kwa heshima ya Red black ni kama nyongeza ya ufafanuzi kwenye mada yake ya Leo kuhusu mnyororo wa umaskini
Red black kongole kubwa kwa kutupa tafakuri jadidi siku ya Leo💪🏿View attachment 3586074
Much appreciationFood for thought..! You deserve congratulations
Kuna kikundi cha watu wachache ndani ya mfumo wamejitengenezea mifereji yao ya kupiga na wanandaa mpaka familia zao ziwarithi🤬Sema tusipoyatoa mashenzi ya CCM madarakani hali itaendelea kuwa hivi hivi au mbaya zaidi ya hivi,mfumo uliotengenezwa na hawa washenzi unataka mtu 1 katika watu 100 ndio atoboe na kukata mnyororo wa ufukara wa ukoo,hii inatakiwa iwe kinyume chake yaani tukipata serikali makini watu 99 watoboe na angalau mmoja ndio afeli bahati mbaya
Vicious cycle of povertyMnyororo wa umaskini (Generational Poverty) siyo tu hali ya kukosa fedha bali ni mfumo wa kimaisha, kifikra, na kijamii unaorithishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Katika familia na ukoo
umaskini huu hufanya kazi kama gereza lisilo na kuta, ambapo watoto huzaliwa na kukuta madeni, ukosefu wa fursa, na mitazamo inayowafunga wasifikie ukubwa wa ndoto zao huku wengi wakiishia pabaya
Ninini asili ya hiki kitu kibaya kabisa?
.(Vyanzo)Urithi wa Madeni na Majukumu:
Katika koo nyingi, mtoto anayefanikiwa kidogo hubeba mzigo wa ukoo mzima. Badala ya kuwekeza ili kukuza utajiri, anatumia kila anachopata kutatua dharura za ndugu, jambo linalomrudisha kwenye umaskini uleule alioukuta.
.Ukosefu wa Elimu ya Fedha:
Koo nyingi huzungumzia jinsi ya "kutafuta pesa" lakini siyo jinsi ya "kuitunza na kuikuza." Maarifa ya uwekezaji hayarithishwi, badala yake inarithishwa tabia ya kutumia kila kinachopatikana.
.Mazingira na Malezi:
Mtoto anayekua akiona umaskini kila siku, anajifunza "saikolojia ya kunusurika" (Survival Mode). Hawezi kupanga mipango ya miaka 10 ijayo kwa sababu akili yake imeshulika na jinsi ya kupata chakula cha leo jioni tu huku kesho ikiwa ni mapambano mengine ya kudra!
ATHARI ZA MNYORORO HUU KWENYE UKOO
.Kifo cha Vipaji:
Watu wenye akili na vipaji vikubwa ndani ya ukoo huishia kufanya kazi zisizo na tija ili tu wapate mkate wa kila siku.
.Migogoro ya Kifamilia: Umaskini hupunguza uvumilivu na upendo. Mara nyingi koo maskini hukumbwa na migogoro ya ardhi kidogo au mali ndogo zilizofifia, hali inayozalisha chuki, ugomvi na visasi
.Hofu ya Kuthubutu:
Ndani ya ukoo, mtu anayetaka kufanya kitu tofauti (kama biashara mpya au kwenda mbali kutafuta fursa) mara nyingi hukatishwa tamaa kwa kuambiwa "kwetu hakuna aliyewahi kufanya hivyo akafanikiwa." Hili limewatokea wengi sana
JE NI MBINU ZA KUVUNJA MNYORORO HUU?
Ili kuvunja mnyororo huu, ni lazima kizazi kimoja kikubali "kuteseka" na kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu ili kutengeneza njia ya wengine..
.Kuwekeza kwenye Elimu ya Kisasa
Siyo tu shahada za darasani, bali ujuzi (skills) zinazohitajika sokoni na elimu ya fedha.
.Kujenga Utamaduni wa Akiba na Uwekezaji
Familia lazima ianze kuweka akiba ya pamoja au kuanzisha miradi ya ukoo (Family Trusts) badala ya kutumia kila kitu kwenye sherehe au dharura.
.Kubadili "Simulizi za Ukoo": Badala ya kusimulia historia ya kushindwa, anzeni kusimulia na kuenzi hatua ndogo za mafanikio.
.Ni lazima kujenga utamaduni wa kuinuana (mentorship) ndani ya ukoo.
Nimalizie kwa kusema mnyororo wa umaskini haukatiki kwa bahati mbaya au kwa maombi pekee ama uchawi; unakatwa kwa maamuzi magumu na nidhamu ya ya hali ya juu, Inahitaji mtu mmoja ndani ya familia anayesema: "Umaskini huu unaishia kwangu."
Na Huyo mtu anaweza kuwa ni wewe.💪🏿🔥 SIMAMA SASA SAFARI YAKO YA UKOMBOZI NDIO IMEANZA!View attachment 3586073
hata bado sijathibitishwa kazini tayari ndugu watatu watu wazima wameshatoa oda wanataka kuja kukaa kwangu.🥺🥺🥺Vicious cycle of poverty
Baada ya kukaa mtaani (in a survival mode) kwa miaka zaidi ya saba, nimepata ajira mwaka jana hata bado sijathibitishwa kazini tayari ndugu watatu watu wazima wameshatoa oda wanataka kuja kukaa kwangu.
Nawaza huu mnyororo hautoweza kukatikia kwangu.
Vicious cycle of poverty

Nina mfano halisi nitausimulia kwa wakati unaofaa.. Ni simulizi ya kweli lakini yenye kuumiza SanaTena familia za kimaskini ambazo wanaishi tu na chanzo cha kipato cha familia hakijulikani kuuacha umaskini huwa kazi sana maana binti akishaota matiti tu ruksa kuwa na bwana na kijana akifikisha miaka 12 tu ruksa kuacga shule kuanza vuta bange wizi so ndio kozazi kinaenda hivyo hivyo
ambaye anaweza kupindua meza ni yule binti aliyetoka nyumbani akaenda kufanya kazi za ndani nje ya mji akakakutana na mtoto wa boss au rafili wa boss akampiga mimba mtoto akazaliwa familia ikagoma muachia mtoto aende umamani uyo mtoto kidogo anaweza badilishq game maana anaweza kupata elimu nzuri kazi na akamua msaidia mama yake na wadogo zake kielimu familia inaweza anza badilikia hapo
InterestingNina mfano halisi nitausimulia kwa wakati unaofaa.. Ni simulizi ya kweli lakini yenye kuumiza SanaView attachment 3586152
Na naona hapa kwenye darubini washakuchafua nyota 😀Vicious cycle of poverty
Baada ya kukaa mtaani (in a survival mode) kwa miaka zaidi ya saba, nimepata ajira mwaka jana hata bado sijathibitishwa kazini tayari ndugu watatu watu wazima wameshatoa oda wanataka kuja kukaa kwangu.
Nawaza huu mnyororo hautoweza kukatikia kwangu.
Asante sana mleta madaNa Huyo mtu anaweza kuwa ni wewe.
Mbaya zaidi umaskini upo ili matajiri wanufaike nao. Hiyo ndo structure ilivyo, mana utajiri na umaskini ni pande mbili zilizo kwemye sarafu moja. Ukiona kuna maskini hata hela ya kula hana, hao ndo wanauza nguvu zao bei rahis kwq bahresa aendelee kupiga helaAsante sana mleta mada