Mo afafanua ununuzi wake kwa Simba


Unachosema ni sawa, ila kwa case ya Simba ni ngumu sana kiutekelezaji!

Ngoja tusubiri tuone wataalamu watakachoshauri, ila mimi kwa mtazamo wangu namwona Mo anataka kujimilikisha timu kijanja, yaani atoe hela bil 20 kuinunua timu halafu aje aiendeleze kwa kutumia bili 20 hiyo hiyo! Logic zinagoma hapo.
 
Hehe...ni kununua kwa aina yake, kumbuka lilikuwa jengo kubwa mnalala watu wachache, anatoa hiyo pesa mnaitumia kulikarabati jengo na kuwa safi, mnampatia vile vyumba vingi ambavyo havikuwa vikitumika avitumie na nyie mnabaki na sehemu ndogo inayowatosha lakini kuta zikiwa hazipitishi nyoka na wala mvua ikinyesha hamlowi..ni faida.
 
West Bromwich albion wamepanda daraja gani kutoka daraja gani!!!???.....
 

Mkuu hii falsafa yako nimeielewa sana. Nadhani ndicho kinachoenda kutokea, ila sasa bora tungekubaliana kumpangisha tu kuliko kusema tumemuuzia.

Isije yakawa yale ya kwenye story ya Abunuwas, nyumba ina gorofa, ground floor ikauzwa, siku ya siku mmiliki wa ground floor akamwambia yule wa gorofani kwamba yeye anataka kubomoa nyumba yake, hivyo mwenye gorofa inabidi alishikirie
 
Mo alisema na siyo 'Simba ilisema'.
 
Na MO akishachukua 51% yeye ndo mwenye maamuzi ya vikao.
49% haiwezi kuilazimisha jambo 51%.
Kwa hiyo swala la hata nani atapata share ya hizo 49% ataamua MO isipokuwa pale tu maamuzi yatafanyika kabla ya kumkabidhi MO na iwe sehemu ya mkataba wa makabidhiano
 

Precisely....kimsingi hiyo ndiyo position yangu...na hapo ndipo umakini wa wanasimba unatakiwa kuwepo

Hii timu ina historia yake ...kumpa tu mtu mmoja hivi bila utaratibu makini ni hatari

Hii kazi ingefanywa na professional firm ya sharia katika kushauri structure nzuri
 
Unafahamu biashara za vilabu zilivyo?
 
Hapana mkuu, leta ufafanuzi ndugu.
Pitia kidogo tu katika vilabu vichache hapa duniani vilivyonunuliwa na mchakato wa ununuaji ulivyokuwa.

Tuna hofu tu ambayo kimsingi mwezi mmoja au hata chini ya hapo kila kitu kinashughulikiwa vizuri na club inaendeshwa kisasa.

Simba haiwezi kuja kukaa vizuri tena,wafadhili nao hali zao za kiuchumi zimeyumba.Inaendeshwa kwa hasara na bado fedha zinaliwa sana hapo Simba...

Watanzania sijui nani katuloga kila kitu ni mashaka mashaka tu....wakati unachotakiwa ni kutathmini mali zako,kuweka vigezo na masharti then mnasonga mbele.Kuna makampuni yanaweza kukufanyia yote hayo maana inaelekea hatuna wataalam au hatutaki kuwatumia.

Katika hili,vigezo vikitengenezwa vyema wala hakuna cha kuhofia.

Wewe unauliza fedha atapewa nani...pitia masuala kidogo ya mambo ya share na hisa.
 
Ungempa huo mfano kungekuwa na tatizo!!!???
 
Kwa mifumo iliyopo ya hizi timu za Simba na Yanga, Mo anakuwa anakosea kuweka hizo fedha katika timu ya Simba.

Hizi timu nina matatizo ya muundo na mfumo.

Yanga ilijaribu wakati wa katibu mkuu wake marehemu George Mpondela alipopendekeza suala la kuigeuza Yanga kuwa kampuni na akashindwa.

Hizi timu ni kubwa na zina rasilimali na watu wa kutosha kuzifanya ziwe timu imara na zinazojendesha kibiashara kwa ufanisi unaotakiwa.

Wazo la Mo Dewji ni zuri lakini ni vema akaanzia chini asuke timu yake kama walivyoanza Bakhresa kwa Azam au awekeze kwenye timu ingine ndogo kama Kariakoo ya Lindi au aazishe na kuwekeza katika timu mpya kabisa "Brand new" tena ilaleta ahueni kimaisha na kimaendeleo akifanya hivyo huko kwao Singida.
 

Mkuu umeniacha ulivyonikuta!

Yaani maana yake ni kwamba sijaelewa kama nimejibiwa au labda nimejibiwa sijaelewa.
 
Hahahahaa...nimecheka kwa sauti mpaka watu wamenishangaa.
 
Cha msingi Mo apewe tu timu, tumeshachoka kufungwa sisi nawashangaa sana mashabiki wanaopiga domo jamaa asipewe timu, mtakua wanasimba uchwara nyie
 

Majibu

1. Simba ya wanachama wa Simba. Hii club inamilikiwa katika zama za Mwl wetu JK Nyerere japo tupo kwenye digial world. Anayeuza ni wanachama wa Simba ambao wao ndio wamiliki. Faida atakayopa itaonekana baada ya mahesabu ya mwaka kufanyika

2. Hio 20bln ni kununua maamuzi yaani kumiliki Simba kwa 51%. Kwa maneo mengine kuiendesha na kuisimamia Simba iwe kwa kutumia hizo 20bln pamoja na hela zingine na Assets zingine Simba walizonazo

3 & 4. 49% wanaendelea kumiliki wanachama wa Simba. Hizo hisa so far bado wanamiliki wanachama, lkn baadaye wakiamua kuuza watajua wenyewe huko. Ila kitakachobadilika kikubwa sana ni kuwa Mo ndio mwenye last say kama Ibra alivyo Chelsea. Akiamua kula sahani moja na Kocha anakula, na wanachama hawatakiwi kufungua mdomo.

Akiamua mchezaji fulani asisajiliwe ndo inakuwa hivyo na wanachama wanatakiwa ku shut up!
 
Mkuu umeongea ukweli mtupu na jamaa anatumia matatizo ya simba kumilliki kiulaini kwasababu simba ina madeni,uongozi mbovu ambao ushachokwa na wanachama na wapenzi na kukosa ubingwa miaka minne mfululizo ndio maana mo anatumia iyo advantage
 
Kwa mifumo iliyopo ya hizi timu za Simba na Yanga, Mo anakuwa anakosea kuweka hizo fedha katika timu ya Simba.

Hizi timu nina matatizo ya muundo na mfumo.

Inaonekana huelewi hata unachokisema

Simba wameshaona hayo matatizo ya Muundo na Mfumo ndio maana wameamua kuubadilisha

Na mfumo waliochagua Simba ni sahihi sana kwenda kwa kipindi hiki na ni mfuo unatumika na klabu zote zilizofanikiwa duniani na Africa

Tunachosema sisi....Ni Transformation hii ifanyike ki utaalamu sana ....Na kwa umakini mkubwa

Ila ishu kama tubadili mfumo au la...simba tumeshaaamua kuubadili huo mfumo
 
Mkuu umeongea ukweli mtupu na jamaa anatumia matatizo ya simba kumilliki kiulaini kwasababu simba ina madeni,uongozi mbovu ambao ushachokwa na wanachama na wapenzi na kukosa ubingwa miaka minne mfululizo ndio maana mo anatumia iyo advantage

However,...hata kama akitumia hiyo advantage...its not a problem so far

Timu ibadilishe mfumo iwe kampuni.......

Katika hiyo miaka yote 80 Timu ilikuwa na hela? na ilifanya nini? Mpira wa sasa sio wa ujanja ujanja kama simba na yanga za miaka 80 iliyopita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…