MO anawapa watu njia za mafanikio

Umeongea pumba tupu. Direction ni nini ukilinganisha na mitaji, connections na exposure kwenye biashar?
Yaani umkute mtu kapiga shule nje( exposure) kapewa kampuni tayari imesimama na equity bank ya kutosha(mitaji) ana connections na network ya kutosha ikitokea ishu moja tu anapiga simu anapewa tender mizigo inapita fasta bandarini anapunguziwa kodi etc etc alafu wewe famba utoke zako na kagadigrii chako cha udsm huna exposure yoyte ya biashara mtaji wenyewe huna hata mia connection yenyewe huna ndio uje useme wewe ni rahisi kuwa tajiri duuh embu acha kuota amka toka usingizini[emoji23][emoji23]
 
mc gregor,

swali moja: wako wapi watoto wa dangote? wako wapi watoto wa bilgate? watoto wa roastam wapo wap? watoto wa lowasa wapo wap? watoto wa steve jobs wapo wap ? mbna kampuni inaendeshwa na watu wengine? je hawana connection, mitaji hawana mbona biashara zao haziskiki? alafu unaongea na mtu ambae alivokua na miaka 19 aliclose deal la 2.1M, apo nna miaka 19:

unaongea na mtu ambae maisha yake yote amekua mfanya biashara, najua ins and outs zote: we kaa apo endelea kusema mtaji, sjui kasoma nje: sjui kakwepa kodi, exposure(ingekua hivi maskini wasingekua wanatoka kimaisha) je unajua unaweza kua na idea tu na usiwekeze hata kumi na ukawa na pesa maisha yako yote? je wewe unafanya bussiness yoyote? je unajua kuna watu walirithi pesa nyingi na makampuni makabubwa wakashindwa kuenedeleza? niishie hapo
 
stakehigh,

We jamaa unaongea pumba tupu. Nani kakwambia watoto wa dangote ni masikini? Nani kwambia mtoto wa gates ni kapuku??Mtoto wa lowassa namjua vizuri ana pesa balaa tatizo lenu hamfatilii vitu mnaishia kusema unamjua mtu flani sijui nn pumba tupu.
Huyo dangote mwenyewe unaemuhusudu unajua alipewa mtaji wa sh ngap na mjomba wake kuanza biashara??
Iv unamjua baba yake gates gates seniour alikuwa sio kapuku??alikuwa ni mtu anaejiweza kusomesha mtoto havard usa sio kitu rahisi
Ukoo wa kina rostam , lowassa etc unadhani ni makupuku wale? Fanya home work yako vizuri dogo sio unaongea pumba tu mifano ipo mingi kina manji kina trump kina dewji wote hao ni muendelezo tu wa pesa za nyumbani

Unajisifia sijui kuclose deal ya 2.1 m we jamaa ndio maana nasema ni either motivational speaker au una hela tu ya kubadilisha mboga duuu sasa 2.1 m ni hela hio??
Unajisifia kuwa mfanya biashara ilihali huujui umuhimu wa mtaji , exposure na network kwenye biashara ujue unachekesha sana wewe hakuna business man yoyote asiejua umuhimu wa hivyo vitu.
Nani kasema kwamba ukiwa masikini hutoboi? Hapa tunaongelea chaces na urahisi wa kutoboa yaani masikini choka mbaya atoboe kiurahisi kuliko mtoto wa tajiri alieandaliwa vizuri?? Amka mzee izo motivational qoutes zimekuweka kwenye usingizi mzito
 
Okay kumbe ulisaidiwa hongera sana.
 
Nimesoma kwa umakini mkubwa sana huu mtanange wa kufanikiwa Katika Biashara ila tatizo lipo sehemu limetulia huku likijichekea na kufurahia.

Na Mimi ngoja nitoe mawazo yangu kwa kuzingatia uzoefu wangu katika Biashara lakini kwa kupitia mawazo ya ma-Guru Katika Biashara.Kuna mtu mmoja mwenye hekima alipata kusema hivi"If you want to go somewhere it's best to find someone who has already been there".

Tofauti uliyopo kati ya umasikini na utajiri ni mindset tu hakuna kingine.
Ukitaka kulijuwa hilo,Mo ametoa ushauri kwa uzoefu wake katika Biashara kwa miaka yake yote aliyofanya lakini badala ya watu kujadili kile alichosema badala yake wanamjadilj Mo.Na hii ndo tabia ya masikini karibu wote Duniani hawakosi sababu ili kujiweka Katika comfort zone.

Kurithi mali si vibaya Kama baadhi ya watu wanavyojaribu kuaminisha hapa lakini pia kuendeleza Biashara uliyoachiwa si kazi ndogo Kama wengi wenu mnavyodhani.
Ebu tujiulize ni watu wangapi wameachiwa mali/Biashara za urithi lakini leo hii hawana hata mtaji kidogo.
Kila kitu ni foundation tu.
Huwa nina tabia ya kupitia kila siku page insta ya Mo ili kujifunza na kupata hekima zake.Jana amepost picha ya zamani sana akiwa na umri wa miaka 12 Baba yake alimpeleka China kuangalia fursa za Biashara.You see yaani akiwa na miaka 12 tayari Mzazi wake anamwekea msingi mtoto wake.
Nadhani kuna Cha kujifunza hapa......


Lakini pia inawezekana tena sana kukuza Biashara from scratch na kuwa global.
Ebu tuwe tunajifunza kwa waliotangulia huko kabla, Jaribuni kusoma hata biography zao basi sio mnapenda kusoma udaku tu.Jaribuni kumsoma Walt Disney alifanya maajabu Katika Dunia hii.

Mwanzoni kabisa nilisema tofauti uliyopo kati ya masikini na tajiri ni mindset tu,Kama masikini nao wakiweza kuwaza kama matajiri basi nao watafanikiwa.
Kama unataka ujenge skyscraper Basi lazima uanze na one block,two block, third block na kuendelea.

Daima msimamo wangu ni huu"Hakuna kinachoshindikana katika Dunia hii.
 

we ni pimbi kabisa: hapa tunaongelea biashara hatuongelei mtoto kua na pesa za kurithi, your useless to this thread: kama ni kua na pesa hata wauza madawa wanazo za kutosha, ebu rejea kwenye mada: sisi tunaongelea chances za kusucced biashara ukianza from 0 na ukirithi: "mada sio pesa" mada ni biashara kufanikiwa,


sasa swali ni biashara za hao madogo zipo wap mbona haziskiki kama za wazazi wao: ndo nmetoa mfano wa dangote, bilgates mbna watoto wao hatuwaskii: fact ni simple , hawana direction ya biashara walioanzisha wazazi wao, ni tafaut sana na mtu alieanzisha biashara from 0 ambaye ana direction ya biashara inatakiwa iwaje:


tusiende mbali ukiwa na miaka 19 ulikua unajua nn wewe kuhusu biashara? eti 2.1M ni hela? taratibu baba na hio bangi:
sasa kama umri huu tu hujui kitu kuhusu biashara miaka 19 ulikuaje?

sasa ngoja nkupe fact from documents uache kutoa toa maneno ambayo hayana facts: and remember i told you my whole life mimi ni mfanya biashara najua ins and outs: sasa soma research hizi na ufunge huo mdomo



AYA SOMA HAPA KWA SAUTI NA UFICHE HUO UPUUZI WAKO KICHWAN:



There are 2,604 billionaires in the world, and 55.8% of them are self-made.

Taken together, self-made billionaires have a total of nearly $5 trillion.

Another 30.9% of billionaires made at least some of their wealth themselves, according to the report, while 13.3% inherited their wealth entirely.


so from this umeelewa nn?
more details link hii apa The majority of billionaires in the world are self-made
 

Jamaa anasoma udaku anadhan kusimamisha biashara ni mtaji na connection: very stupid, ni dhahiri kua jamaa hajui chochote kuhusu biashara, zaidi ananchekesha anavosema simu moja unafikisha mzigo kana kwamba hata alieanzisha biashara alikua anapokea simu hivo: very very stupid mindset he has

in most cases even the most successful business zna matatizo kibao, madeni ndo usipime: there is more than we see, people should learn that sio pesa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…