Mo Dewji akana kujiuzulu Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba na Kubakia kuwa Mwekezaji

Status
Not open for further replies.
Tutaanza kupitisha bakuli? Daaaa ntambia nini mashabik wa yanga mo rudi tu baba mpira ndio ulivyo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Shida nyingine kubwa ni Mwekezaji kufanya mambo kama Haji Manara. Alikuwa na sababu gani kujiuzulu huku akitambia fedha alizotoa? Kwa mini asiseme nawajibika kwa kukosa kombe hili?
Klabu kubwa haiwezi kupelekwa kwa mtindo afanyao Manara wa vijembe vya kanga moko na personal assassination kuelekea kwa wapinzani wako. Tubishanie soka na uwezo wa klabu zetu na sio afanyavyo Manara.
Ni wajinga tuu wanaweza kumuunga mkono anavyo dhalilisha wengine, bila kujua kuwa kuna mahali hata yeye wanatamani wamuite zeruzeru lakini utu na utii wa sheria unawazuia.
Simba haiwezi kuendeshwa kiswahiliswahili namna hiyo hadi kuifanya ichukiwe badala ya kuonewa wivu wa mafanikio na wapinzani wake kwa sababu ya maneno yasiyo staha kwa watu ya Manara.
Nazungumza haya kama mpenzi wa Simba wa zaidi ya miongo minne, hivyo kuna uchungu wa nikisemacho
Sent using Jamii Forums mobile app
 
MO pesa za familia, wanafamilia wanashangaa pesa inazama tu hairudi, hasara, hasara ,hasara, bora kipindi cha JK ukiwa mfadhili wa hizi timu unasamehewa kodi , sasa hivi ni ngumu!
 
Tatizo la Simba ni usajiri mbovu ilioufanya.. kuna wachezaji wengi tu hawafai hata kufanya mazoezi Simba....wale wabrazil ndio kabisa hawafai...na hii inachangiwa na kupenda wachezaji wa bei rahisi....Kiufundi Timu inacheza taratibu sana tena legelege utadhani hawajala...pongezi kwa kakolanya umetupungizia aibu.
 
Ni muhuni mmoja ame-hack account ya Mo, leo ameandaa press conf. anakuja kukanusha hayo mambo.
 
Wengi wanasema Uchebe arudi lakini nafikiri hata yeye hakuwa na timu yenye kasi ya kuwasumbua mabeki.
Simba wanapaswa wapate kocha mwingereza awafundishe mpira wa kasi na nguvu.

Mpira wa ulaya (continental Europe) ni wa taratibu sana (pedestrian football) tofauti na Uingereza (kisiwani) ambapo wao mpira ni replica ya Rugby.

Kuwa na kocha kutoka Ubelgiji au nchi nyingine ya Ulaya ukiondoa uingereza kunafanya timu icheze pasi nyingi sana na taratibu sana.

Mara kumi hata kuwa na kocha mtanzania kuliko hawa wazungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

ahahaha,dah
 
Maamuzi ya hovyo , kutoka kwa Kiongozi wa hovyo.
Ya hovyo kivipi? Kama Mwenyekiti kuna wakati huwa anaweka mzigo kwenye timu ulio nje ya mkataba wa uwekezaji, sasa unataka aendelee kupoteza pesa zake? Wewe ungekuwa tayari kupoteza pesa namna ile?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…