Uchebe na Sven wote ni wabelgiji, falsafa yao ni mpira wa pasi nyingi na taratibu.walikurupuka sasa inaanza kula kwao, huyu mzungu mtoto kaja kuvuruga mfumo wote!.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sidhani kama unajua maumivu ya kupoteza pesa namna ile.Duh
Mwekezaji anataka kila mechi ashinde as if uwanjani anacheza na team/wapinzani vivuli tupu.
Atengeneze timu yake ili aweke pesa zake anakua kama hajaenda shule bhana.
Hapana mimi wala sio mpenzi wa Simba wala Yanga kwa sasa zamani nilikuwa napenda sana Simba ila sina yale mapenzi ya zamani mimi nitalia kwa Liverpool. naongelea hali ya ujumla tu hata Yanga yaliwafika haya nadhani hizi team zinarudia makosa yaleyale kila siku na Yanga wataingia katika mitego kama hiyo ya GSM japo inaweza kuwa kama mdhamini ila najuwa mdhamini analipa anafanyiwa kama mkataba ila sio tena mpaka kocha wao. Hizi team kubwa haziwenzi kujifunza mpaka siku washabiki watakapo amka Tanzania nzima na kuacha kushabikia hizi team badala wapende team zako za mikoa yao na mitaa yao ndio kutakuwa na adabu kama walivyofanya Kenya kwa Leopard na Gor Mahia ndio tutaheshimiana.Si mlimpa timu tena kwa vifijo, mapambio na vigelegele huku mkimtukana mzee kilomoni sasa leo mwalalama nini? Heijah,
Sent using Jamii Forums mobile app
Mie kwenye kejeli za Manara huwa napata ukakasi sana japo naipenda Simba.Shida nyingine kubwa ni Mwekezaji kufanya mambo kama Haji Manara. Alikuwa na sababu gani kujiuzulu huku akitambia fedha alizotoa? Kwa mini asiseme nawajibika kwa kukosa kombe hili?
Klabu kubwa haiwezi kupelekwa kwa mtindo afanyao Manara wa vijembe vya kanga moko na personal assassination kuelekea kwa wapinzani wako. Tubishanie soka na uwezo wa klabu zetu na sio afanyavyo Manara.
Ni wajinga tuu wanaweza kumuunga mkono anavyo dhalilisha wengine, bila kujua kuwa kuna mahali hata yeye wanatamani wamuite zeruzeru lakini utu na utii wa sheria unawazuia.
Simba haiwezi kuendeshwa kiswahiliswahili namna hiyo hadi kuifanya ichukiwe badala ya kuonewa wivu wa mafanikio na wapinzani wake kwa sababu ya maneno yasiyo staha kwa watu ya Manara.
Nazungumza haya kama mpenzi wa Simba wa zaidi ya miongo minne, hivyo kuna uchungu wa nikisemacho
Sent using Jamii Forums mobile app
Alikuwa anatafuta pa kutokea huyo.Heheh kama ni kweli basi Mo ni mbabaishaji naye...
Yaani ukose kombe la mapinduzi ndio utoke povu hadi kukimbia uongozi...
Akitoa pesa kama investor ndio hatopata hasara aliyoiepuka? Kasema kuwa atawekeza kwenye infrastructure na kuendeleza soka la vijanaPesa ataendelea kutoa kama investor, alichojiuzulu ni uenyekiti wa bodi.
Hii ni point ya muhimu sana lakini kwasababu tunaiabudu dezo wacha dezo ifanye kazi....tunaweza kutoa kelele za kushangilia na labda hela tuitoe kwenye bet kwa maslahi binafsi lakini michango ya 3000 tunahitaji msukumo kama si kulazimishwa..Beira Boy, Real Madrid timu ya wananchi inaendeshwa na wanachama. Perez pale amechaguliwa na mkutano mkuu kuwa Rais.
Simba na Yanga wanakwama wapi. Mbona wananchi kwa pamoja wanayo pesa nyingi kuliko za Mo na Gsm. Kila mwanachama na shabiki wa hizi timu kila mwezi akachangia timu yake 3,000 ni zaidi ya bilioni 20 kwa mwezi.
Michango hii kwa mwaka hizi club zinauwezo wa kujenga viwanja, kulipa mishahara, kununua ndege binafsi ya club.
Mimi siwalaumu Mo wala Gsm nawalaumu wanachama na mashabiki wa hizi club simba na Yanga pamoja na viongozi wao wameshindwa kuziendesha hizi club.
Sent using Cash Money Wings
Kwa uelewa huu tuna safari ndefu sana. Umeambiwa ameng'atuka kwenye board lakini atabaki kuwa muwekezaji sasa hayo maneno yote ya nini!!??? Hivi wengine vichwa vyenu mnavitumia kufugia nywele tu!!???Mpira bongo haulipi, alitegemea timu ikacheze Champions league ,matokeo yake inapambania kikombe cha million 100 , mech za kujaza had kariakoo derby. , mapato yanayoingia kwa mwaka hayazidi mil 500, wakati gharama za uendeshaji ni zaidi ya billion 5, kwanini asikimbie [emoji1787][emoji1787]
Manara ni mshamba sana na mpenda kujipendekeza kuliko pitiliza. Sijui Simba tunakuwa na watu wa aina hiyo wa nini! Kwanza anachofanya sio kukuza upinzani wa kimpira bali chuki kwa klabu tuuMie kwenye kejeli za Manara huwa napata ukakasi sana japo naipenda Simba.
Hicho ni kiwango cha juu sana cha ushamba wa mpira.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama namwona Mzee Kilomoni akicheka kwa dharau.Mlimtukana sana mkisema ana vuruga timu! Lkn yeye nina hakika alikuwa anajua MO ni mbabaishaji tu. Nadhani sasa mmeanza kumuelewa.
Uzi tayari, na mods tafadhali msiunganishe huu uzi na uzi mwingine.
Sent using Jamii Forums mobile app