Mo Dewji amshauri Kocha Omog aachie ngazi, Simba yavunja naye Mkataba

Inatosha aisee! Hana mbinu mpya kwa wachezaji waliopo. Anapanga kwa kukariri. Zidane amebeba makombe matano lakini atatolewa mkuku. Omog hana hata kikombe cha kahawa alaf avumiliwe! Utakuwa uzwazwa huo.
Nyie ndio mliokuwa mnadai Yanga ananunua mechi,malinzi na mwesiga wanawahujumu!mikia kila kukicha mnakuja na sbb mpya
 
Pumzi imekata mnaanza kumtafuta mchawi...kamati ya usajili inasajili wachezaji pancha kisha unatamba kuwa una kiķosi cha bilioni 1.3 baadae mnampa kòcha lawama...only in mşimbazi
 
Ngoja akabidhiwe tuone mengine zaidi
 
Aende tu timu ilimshinda toka kitambo. Ametupotezea muda tu
 
Omog ni kocha mzuri ila dizaini kama simba ameishindwa au ameishiwa mbinu, ana kikosi kipana sana na chenye washambuliaji wengi mno ila team imekuwa ya kushinda goal 1 na draw ambazo hazina kichwa wala miguu

Kwa kocha mzuri akiwa na kikosi kama cha simba angefanya vizuri sana, me naona bora apishe mwingine mapema kabla mambo hayajafikia kama msimu uliopita, kufukuza kocha ni jambo la kawaida kwenye mpira ndo alitimulia Enrique barca na ameshinda vikombe vyote sembuse kocha alieongoza kwa tofauti ya point 12 na kuto win ligi
 
Hapo ni siasa katika soka na Omog kawa kondoo la kafara, wajiandae kupotea zaidi.
 
Ila simba ni litimu linalo endeshwa kienyeji enyeji sana, ingawa mimi ni mshabiki wa yanga, nimesikitishwa sana na matusi ya hanzpopo aliyowatukana wachezaji, timu ya simba ilikuwa imeanza kuimarika vizuri ila matusi na comments za vile zina demoralize spirit ya wachezaji, kwa kufungwa mechi 1 tena kwa bahati viongozi wanapoteza imani kwa wachezaji? Hapana something iz wrong, na kwa stahili mpira wetu hauwezi kuendelea
 
Hapana mo hakupaswa kutoa comments kama hizi hadharan tena mchana kweupe! Angaweza kumshugulikia omog vizuri tuu through vikao halali vya ndani.....ni kweli inasemekana aliushinikiza uongozi kumtimua omog alivyo ona kuna delay delay akaamua kuruka na hiyo comment yake hadharani, ki ukweli hii sio njia sahihi ya ku confront destructive conflict kama hii ya omog!
 
Inatosha aisee! Hana mbinu mpya kwa wachezaji waliopo. Anapanga kwa kukariri. Zidane amebeba makombe matano lakini atatolewa mkuku. Omog hana hata kikombe cha kahawa alaf avumiliwe! Utakuwa uzwazwa huo.
F.A last season... Au tumeshasahau?
 
Breaking news Timu ya Simba imeachana rasm na aliekua kocha wake OMOG .

Simba Sports Club Dar es Salaam

23/12/2017 TAARIFA KWA VY0MB0 VYA HABARI

Klabu ya Simba na kocha wake mkuu Joseph Omog, wameamua kwa pamoja kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalum yanayozingatia maslahi ya pande zote mbili. Klabu inamshukuru kocha 0mog na inamtakia kila la kheri kwenye maisha yake nje ya Simba.

Kwa wakati huu Timu yetu itakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma na itaendelea na mazoezi kesho,na kupumzika Siku ya Jumatatu kwa mapumziko ya sikukuu ya Christmas na itaingia kambini Jumanne kabla ya safari ya Mtwara,ambapo tutacheza na Timu ya Ndanda kwenye mchezo wa Ligi kuu wiki ijayo.

Pia kwa niaba ya uongozi, benchi la ufundi na wachezaji.tutumie nafasi hii kuwaomba radhi sana Wanachama na washabiki wetu kwa matokeo ya jana, sote tumeumia ila ndio mchezo wa mpira ulivyo, na tuwaombe muwe watulivu katika kipindi hiki ili tufikie malengo yetu.

Mwisho klabu inawatakia nyote Sikukuu njema ya Noeli na mapumziko mema ya wikiendi.

IMETOLEWA NA.... Haji S MANARA Mkuu wa Habari Simba Sc SIMBA NGUVU MOJA


 
Mo naye anaingia kwenye siasa za Simba na yanga.kwani Simba kafungwa na nanii.
 
duu kweli timu ilipoteza uelekeo sio simba ya Enzi zangu nikiwa mchezaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…