Aende tu, kwanza watanzania hakuna tunachokijua wala hatukijui tunachokitaka kwenye michezo. Angebaki hadi mwisho wa msimu, halafu akatoka patupu. Yangekuja majitu hapa na "mathread" yao hapa "oooh tuliwaambia hapa Omog sio kocha!" Afadhali ametupisha, huyo mgeni hata akifeli atakuwa na kisingizio cha ugeni. Yaani watu tunashuhudia mechi kibao tu za ligi, timu inacheza ugoro tu, morali iko chini alafu mwalimu upo tu!! Na umeshindwa kurekebisha hadi mzunguko wa kwanza karibia unaisha upo tu! Baadae unakuja kufungwa na timu isioeleweka, uendeleee kuachwa tu?! Kunyangisi!! Haiwezekani... Ila asisahau tu kufikisha salamu kwa ndugu Jama Mba!!