MO Dewji anawazidi vipi utajiri Bakhresa na Rostam Aziz?

MO Dewji anawazidi vipi utajiri Bakhresa na Rostam Aziz?

Huyu jamaa utajiri wake wa magumashi na kiwanda cha juice eti ndiyo tajiri namba moja. Ukija kwa Bakhressa ana meli, ngano, soda, kiwanda cha sukari chenye thamani ya bilioni 600, Azam TV na Azam Pesa.

Rostam Aziz anayemiliki kampuni ya ndege, caspian, Tigo Tanzania, Taifa gas, inakuwaje tunaambiwa huyu mbabaishaji eti ndiyo tajiri wa Tanzania? Ama anafanya ubabaifu aonekane hivo?
Mkuu anayesema Mo Dewji ni tajiri namba moja Tanzania sio mimi na wewe, bali ni Jarida la Forbes. Nakushauri uingie kwenye page yao mtandaoni uangalie vigezo vinavyotumika. Mfano, R.D. TATA ambaye Wahindi wengi wanaamini ndiye tajiri mkubwa India hayumo hata kwenye matajiri mia wa India kwa mujibu wa Jarida la Forbes. Kwanini? Kwasababu ya vigezo vinavyotumika. Google ujielimishe!
 
Kwa kukusaidia tu MO dewji anamiliki uchumi wa taifa zima la TANZANIA kwa 4% na asilimia 96 tunagawana watu wote 62M. more anafanyabuashara katika mataifa 36 africa nzima. Azam n mataifa 12 tu.

MO anabiashara nying sana hazihesabiki
Acha basi 😁😁😁
 
Biashara pekee aliyonayo Bakhressa, hana ni Marine transport pekee. Biashara za Mo ambazo wengine hawana mafuta (Star Oil Ltd), Bima (Mo Assurance), Fedha na Mitaji (Mo Capital Finance Ltd, Sifa Advisory Ltd), Simu (Zefona), electronics (Mo electronics), Boxer, Korosho etc. Huyu jamaa yuko kwenye maisha ya watu wa kipato cha kati na cha chini.

Ukiwa juu juu huwezi kumuona
Haya tuambie hiyo zefona ina operate wapi? Na azampesa ina operate wapi

Haya hizo tv na friji zake za kichina aleta akaona hasara zaidi ya miaka 4 sijaziona tena hapa bandarini zikiingia (mo electronics)

Boxer yeye ni wakala na wapo mawakala wengine wengi tu
 
Naamini Rostam Azizi ndiye Tycoon namba moja hapa nchini, hawa wengine ni Chawa tu.

Fuatilieni vizuri ukweli mtaujua.

Huyu Mwamba ni level ingine.

Hope one day nitazidi hapo alipofikia.
Tupe data ..... Nikuulize je mo ameajiri watu wangapi ??? Ana mchango kiasi Gani kwenye GDP ya bongo ... Tusipende kuharibu watu tunafaa kujifunza kutoka kwao maana ukizungumzia Metl ni kampuni iliyoajiri watu zaidi ya 25000 sasa unataka kusema Nini hapo
 
Tupe data ..... Nikuulize je mo ameajiri watu wangapi ??? Ana mchango kiasi Gani kwenye GDP ya bongo ... Tusipende kuharibu watu tunafaa kujifunza kutoka kwao maana ukizungumzia Metl ni kampuni iliyoajiri watu zaidi ya 25000 sasa unataka kusema Nini hapo
Sasa anaviwanda vya dawa za mbu dawa za meno sabuni maji laziwa awe ameajiri watu wengi ila je return yake ipoje?
Mwenzake anahisa tigo tz vodacom SA caspian taifa gas
Hebu nambie uwekezaji wa sabuni waweza kuwa return sawa na uwekezaji wa kampuni ya tigo?
 
Back
Top Bottom