Don Clericuzio
JF-Expert Member
- Dec 8, 2017
- 16,930
- 40,556
Huo mkataba umekaa kiujanja ujanja.
Hata mimi na wewe tusingeweza kukubali kuweka hizo bilioni 20 kwenye account ya simba wakati hatujui zitarudi vipi?.
Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
Simba na Yanga haziuzwi na haziuziki.
Basi tuache kupiga kelele kuwa tunanyonywa na moo na GSM wakati sisi wenyewe wananchi tumeshindwa kuziendesha club zetu.
Yanga mpaka Leo wanadaiwa na wachezaji wanashindwa kuwalipa kuwa na brand sio kuwa na HELA
Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
Kwa yeyote anayejua taratibu za kuuza kampuni, uwekezaji na uuzaji wa hisa, toka mwanzo angeona hili dili la Simba na Mo ni gumu.
Tuendelee kufurahia tu kipindi hiki maana timu inafanya vyema.
Mo anajua akiweka hiyo bilioni 20 atapoteza control, yeye aendelee hivi hivi tu.
Moo ataweka hela zake kulingana na mwenendo wa timu unavyokwenda.
Kuweka bilioni 20 sio shida,shida unaziweka zifanye nini?
Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
Hataweka hiyo hela, anajua akiweka atapoteza sauti (mamlaka) aliyonayo sasa hivi.
Licha ya hayo.
Bado haiingii akilini uweke bilioni 20 kwenye kitu ambacho haujui kitaleta faida gani..
Mpira wa uwekezaji hapa Tanzania bado sana.
Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
Mkuu ni zoezi jepesi sanaNaamini mpaka kuendelea kuwa na timu kwa muda wote huu lazima anaona jinsi anavyofaidika. Lazima kuna faida anayoipata.
Thamani ya timu hatuijui na haijulikani, Mo ana 49% ya umiliki lakini kila kitu anatoa yeye, 51% tunaambiwa ni ya wanachama, ambao hawatachangia hata shilingi.
Sijajua faida itagawanywa vipi, je kutakuwa na gawio kwa wanahisa?
Hii complexity ilionekana wazi ni zoezi gumu kulitimiza. Otherwise wamuuzie timu yote, na hapa ndipo swali litaibuka, wamiliki ni kina nani? Nani atapokea pesa ya mauzo?
Mkuu ni zoezi jepesi sana
Assume una basi lako lakini bovu bovu kila siku gareji na linakutia hasara
Nakuja mimi kuingia ubia na wewe, tunakubaliana mimi nitoe milioni 30 tulikarabati basi liwe vizuri halafu mapato tutagawana 50/50
Hapo wewe ni Simba mimi ni Mo
Huhitaji kutoa chochote sababu una asset ya basi tayari
Kama kwenye hilo basi upo na ndugu zako basi mimi ntachukua aslimia 50 yangu na nyinyi hiyo asilimia 50 itakayo baki myagawana kulingana na hisa zenu kindugu
Mo atachukua asilimia 49 ya faida na asilimia 51 wana simba watagawana kulingana na share zao
Simba SC sio mtu au watu ni kitu (entity)Wana Simba ni kina nani?
Swali liko hapo.
Simba SC sio mtu au watu ni kitu (entity)
Kwa mujibu wa sheria Simba Sc ni organisation
Tunapo sema wana Simba tuna maanisha waumini wanao amini katika simba kuhakikisha Simba Sc inaendelea kuwepo
Mkuu ufafanuzi wangu wa kwanza kuku quote wewe ilikua ni kujaribu kufafanua kwamba simba ni asset haihitaji kutoa pesa ila muwekezaji....nikatoa mfanoTuwe specific hapa, mfano ikipatikana faida ya milioni 100, Mo atachukua mil 49.
Nipe majina au vikundi vitakavyogawana hiyo mil 51 inayobaki.
Naamini umiliki wa kampuni siyo siri, kila kitu kiko wazi.
Mkuu ufafanuzi wangu wa kwanza kuku quote wewe ilikua ni kujaribu kufafanua kwamba simba ni asset haihitaji kutoa pesa ila muwekezaji....nikatoa mfano
Pili nikatoa ufafanuzi jinsi gawiwo la faida linavyokua kisheria......nikatoa mfano
Sasa kiundani sijui kama hizi hisa 51 za simba sc na zenyewe kuna wanachama wamepewa hisa na kwa utaratibu
Kimsingi mwana hisa ni muwekezaji anaweka pesa yake izungushwe aje kupata gawio.....hakuna mwanahisa anayeweka pesa asipate gawio
So kama wapo basi ni lazima watapata gawio......mimi siwajui mkuu
Lengo la club za michezo sio kupata faida na kugawia mahela kwa wanachama, lengo ni kuifanya club iwe imara zaidi iweze kujiendeaha na kubeba vikombe zaidi na zaidi
Kawaida inatakiwa timu ikipata muwekezaji anatia pesa timu inakua nauwezo zaidi inafanya vizuri zaidi na faida muwekezaji anachukua asilimia zake zinazobaki zinaendeleza club
Hata kama kuna wana simba watakua na hisa bado kuna hisa zitabaki za club kwaajili ya maendeleo ya club
Ndugu unauhakika simba inaufadhili wa zaidi ya 10b???? Aisee hembu karejee makabrasha yaliyokupa hii taarifa! Zaidi ya 10b???!!!Hatoi yeye
Simba ina ufadhili wa
voda
Azam tv
Sportpesa
Fedha hizo ni zaidi ya 10b
Yeye hatoi chochote