Kim Jong Jr
JF-Expert Member
- Mar 15, 2014
- 11,074
- 20,608
Huyo Rage aliifikisha wapi Simba kimapato si amewahi kuwa Kiongozi simba.Kuna vitu watu hawaelewi wengi hawana elimu ya uwekezaji bahati mbaya mfumo wa vilabu vyetu umeruhusu wajanja kuwa na sauti.
Kabla ya Simba kuingia kwenye mfumo wa hisa ilitakiwa ije kampuni ya uhasibu itathimini thamani yake. Thamani ya timu sio majengo tu bali ni pamoja na fanbase.
Kitu ambacho Simba hawajui mo anaitaka simba kuliko simba inavyomtaka mo rejea alipotishia kujitoa na kudai anatumia pesa nyingi hakuna mwanasimba aliyembembeleza badala yake Raga na Kigwangala walimhoji aseme hizo pesa zinatoka mfukoni mwake au ni sehemu ya uwekezaji.
Alianza kuikopesha simba pesa kabla uwekezaji haujaanza lakini simba ilipoingia mkataba na sportpesa alikuja juu.
Kama simba ingetulia hizo hisa zingeuzwa kwa bei kubwa simba mpaka sasa hivi haijitegemei kitu ambacho ni hatari kwa mustakabali wake hata mipango yake ni vichekesho huwezi kumtoza shabiki pesa ila unaweza kumuuzia shabiki bidhaa za timu. Hata mapato ya jezi hayaeleweki pamoja na kwamba kuna mkataba jezi zinatakiwa ziuzwe maduka maalumu lakini ukienda taifa jezi zinasambazwa chini au hata klabuni unaona zimetundikwa jezi feki.
Lakini yote yanafanyika sababu ya kukosa uongozi makini.
Huyo kigwangala ameifikisha wapi simba.
Hivi unajua kabla ya MO kuwa muwekezaji Simba ilikuwa hovyo kimapato Kama Mbao FC ndio sababu ya Kile kikosi Cha wakina Ajibu , Ndemla kupandishwa kuja kucheza timu ya wakubwa na timu ilikuwa haina hela kununua hata wachesaji. Ndio msimu ambao Azam ilitoa hata wachesaji wao kuja Simba kwa mkopo kuokoa jahazi (Kimwaga alipelekwa Simba kwa mkopo). Hali ilikuwa mbaya msimbazi. Hao wakina Rage na wewe kilaza hatukuwahi kuwaona mkipeleka hata mabakuli ya chakula kuwapa wachezaji.
Mtu aliefuatwa kupigiwa magoti alikuwa MO dewiji ndio alikuja kuokoa jahazi na akaanza kulipa mishahara na usajili wake wa kwanza kufanya akamleta MAVUGO. Nyie mnapiga kelele mitandaoni ndio mnachoweza ila hata laki 1 mifukoni hamna.
Hata marehemu mzee Yahaya Akilimali alikuwa anaweza kuchapa Domo lake na kumuita Yousuph Manji ni mwizi pale yanga ila baaada ya manji kujitoa hakuwaji kutoa hata 50,000 kulipia mishahara wachezaji. Yanga ilifikia hatua inachangiwa hela na mashabiki tena kwa kutembeza bakuli uwanjani. Ilifikia hatua Mwinyi zahera anatoa hela Yake bank analipa wachezaji mishahara ( Uliza watu upewe taarifa ).
Hizi taarifa eti Simba au yanga kuwa na thamani hizo mnazozitaja kila siku na kuona MO na GSM wananufaika Ni Nyie mashabiki uchwara ndio mna hizo fikra.