libeva
JF-Expert Member
- Mar 25, 2015
- 4,465
- 3,615
Bilionea Mohamed Dewji maarufu kwa jina la Mo Enterprise alikuwa anaimiliki club ya mpira ya African Lyon ndiye alikuwa anaifadhiri ikashuka daraja akaisusa, wanajua wenyewe walivyo pigana wakapanda daraja na sasa wapo ligi kuu kilio chao ni vifaa vya michezo wamelalamika na vyombo vya habari vimeripoti. Huyu Bilionea anatajwa tajwa kutaka kuinunua Simba ama kuifadhiri na kuna viongozi na mashabiki njaa eti wanamuunga mkono kwamba anunue Simba kwa bilioni 20 akinunua Simba nani mlipwaji? Na hiyo timu inamilikiwa na wanachama, swali dogo la kujiuliza kama timu yake mwenyewe ameshindwa kuidhamini atawezaje kuinunua timu kwa bili 20? Club yake hata njumu hawana, jezi hawana wameonekana kwenye vyombo vya habari wanavaa jezi dongea, Simba jiulizeni ameshindwaje kuindeleza timu yake.? Anataka arukie timu yenye wanachama lukuki nchi nzima kwa nn asitumie njia sahihi? Akinunua timu mlipwaji nani? Shtukeni wanachama, mbona Azam ameweza Huyu Mo hizo 20 bil mbona anahamisha mitaa kadhaa popote na kuiweka timu yake ya African Lyon kama alivyo fanya Azam, mashabiki mnatapeliwa mchana kweupe simamieni haki zenu timu ni ya wanachama sio ya uongozi uliopo madarakani.