Mo Dewji kaitelekeza timu yake African Lyon ataiweza Simba?

Mo Dewji kaitelekeza timu yake African Lyon ataiweza Simba?

libeva

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
4,465
Reaction score
3,615
Bilionea Mohamed Dewji maarufu kwa jina la Mo Enterprise alikuwa anaimiliki club ya mpira ya African Lyon ndiye alikuwa anaifadhiri ikashuka daraja akaisusa, wanajua wenyewe walivyo pigana wakapanda daraja na sasa wapo ligi kuu kilio chao ni vifaa vya michezo wamelalamika na vyombo vya habari vimeripoti. Huyu Bilionea anatajwa tajwa kutaka kuinunua Simba ama kuifadhiri na kuna viongozi na mashabiki njaa eti wanamuunga mkono kwamba anunue Simba kwa bilioni 20 akinunua Simba nani mlipwaji? Na hiyo timu inamilikiwa na wanachama, swali dogo la kujiuliza kama timu yake mwenyewe ameshindwa kuidhamini atawezaje kuinunua timu kwa bili 20? Club yake hata njumu hawana, jezi hawana wameonekana kwenye vyombo vya habari wanavaa jezi dongea, Simba jiulizeni ameshindwaje kuindeleza timu yake.? Anataka arukie timu yenye wanachama lukuki nchi nzima kwa nn asitumie njia sahihi? Akinunua timu mlipwaji nani? Shtukeni wanachama, mbona Azam ameweza Huyu Mo hizo 20 bil mbona anahamisha mitaa kadhaa popote na kuiweka timu yake ya African Lyon kama alivyo fanya Azam, mashabiki mnatapeliwa mchana kweupe simamieni haki zenu timu ni ya wanachama sio ya uongozi uliopo madarakani.
 
Wewe utakua ni watu wachache wanaonufaika na mfumo uliopo hivi sasa, bila kujali maslahi ya walio wengi, na kama hunufaiki itakuwa umetumwa na watu wanao hofia kupoteza maslahi yao. Mo asipoiweza Simba, simba itabaki kuwa Simba, hata asipoichukua Mo kwani sasahivi Simba ina fanya nini, bora tujaribu kwa Mo, kuliko kuendelea na hali hii. Nina shaka na wewe kama kweli ni mpenzi wa Simba, inaawezekana unaoogopa kuimarika kwa klabu ya Simba maana madhara yake unayajua, wehenga husema hadui yako mwombee njaa. Sidhani kama kuna mpenzi wa Simba atapingana na mawazo/ mipango mizuri ambayo ameielezea leo bw. Mo, tumpe timu akishindwa Timu itarudi kwenye mfumo huu tulionao, miaka 80, klabu haina jipya kwanini tusiapokee mawazo mapya.
 
Hivi nani asiejua upuuzi uliokua unaendelea pale African lyon? Mo aliondoka kutokana na ubabaishaji. Watu mda wote wanawaza kupiga dili
 
Amesema aliiacha africa lyon kwa sababu ilifika muda, mechi inaendelea uwanjani hakuna mashabiki.

African Lyon kongwe kuliko Azam, alipaswa kuwekeza kama Azam ye anataka ready made kesha onyesha udhaifu ajipange
 
Kwa hyo unafurahi tunavyoitwa wa mchangani

KWA SASA MPIRA PESA MO apewe timu mambo mengine baadae

Kuna hatari akipewa timu mkashuka daraja na kufutika kabisa
 
Naunga Mkono Simba Kubaki kama ilivo. Kama Dewji ana Talent za uongozi na yeye ni mwanachama wa simba anaruhusiwa kuogombea Uongozi ili afanye maendeleo anayo kusudiwa. Njia Nyengine ni kui sponsor Simba kwa udhamini wa muda mrefu .
Kuuza Simba kwa yeye kuimiliki hilo haliwezekani. Mimi ni mwanachama wa simba na mtu wa kwanza kwenda mahakamani kupinga hatua hii.
Simba ni timu ya wazee wetu wa Dar es salaam ..Pamoja na Yanga na Coastal Union na African Sports zina Historia za kipekee katika siasa za nchi hii tangu enzi za Kugombea Uhuru.
wazee wale waliziongoza timu hizi kwa mafanikio makubwa na ikawa ndio chachu ya maendelo ya Footbal Tanzania.
Simba ni Priceless..huwezi kuithamini kwa fedha kabisa. Ni club ambayo imeweza ku survive zaidi ya Miaka 70 ya dharuba kwa muundo wake huu huu uliopo ambao ni kuwa chini ya wanachama na wapenzi.
How much is share ya Club hii ?'
Na jee nani atakua beneficiary wa hizo share Jee wajukuu wa waanzilishi wa Simba au matapeli kina Hanspope na Aveva ?
Ni wa zi Simba sio Africa Lyon ambayo Dewji ilimshinda kuindesha kwa sababu moja tu..hakua tayari kuwekeza kama alivo ahidi.

Tunamshauri yeye na wote wanaopokea Rushwa waache ndoto zao halitawezekana kabisa hili.....bora simba ife kabisa kuliko kuuziwa mtu mwenye malengo ya kuifanya simba brand ya biashara yaek. Na hakika Tunaomba TAKUKURU Wachunguze wale wote wanaoshabikia hili kwani kuna kila dalili wanapokea rushwa kufanikisha mpango huu haramu
SIMBA NI YA WATANZANIA WAPENZI HAIWEZI KUUZWA NA HAITAUZWA..
 
Hapana. Tunahitaji new approaches tofauti na hoi tuliyonayo sasa. Ime fail big time
 
Wanasimba mna potea kabsa kwakuuza timu kwamtu. Manji ni sponsor wayanga. Kwa nini Mor anataka kununua umiliki.?? Na kwanini asiwe sponsor to wa club ya simba.
Mor ana maslai makubwa sanaa kama akinunua umiliki wa Club.
 
Kwani Abramovich ni sponsor wa Chelsea? Nyie kaeni na sponsor wenu sisi tunataka mmiliki
 
Daaaaah.
Wanachama wasimba wanafanya maamuzi makubwa huku wakiwa na jazba ya kutofanya vizur kwenye ligi kuu.
"Unauza Umiliki Unajisifia" yaani nyie mna applay sera za ccm kwenye business!! Sera za ubinafsishaji?? All of them they need a Punishment!! Huu ni ujinga!!
Simba hawana Wisdom of the business, thts why mnauza timu kwa mtu.
 
Kwani manji sianajiendeshea tu team yenu kama ya familia mmekaa kimya kama hamuoni
 
Back
Top Bottom