Mo Dewji kumiliki hisa za klabu ya Simba baada ya kuwa muwekezaji pekee aliejitokeza

Mo atamiliki 49% kwa hiyo billion 20. Wengine mjiandae kununua hizo 51% zaidi ya billion 20


Sioni hizo hisa za asilimia 51 zikinunuliwa na wanachama zote. Ikiwa michango ya kadi ya buku buku kwa mwaka ilikuwa tatizo.
 

Walisema kuwa huwezi kupata hisa kama sio mwanachama.

kama kuna kampuni inataka hisa ni lazima ijitangaze kuwa hiyo kampuni ni mwanachama halali wa Simba. Imagine kampuni ku-settle upande mmoja kwenye ulimwengu wa simba na Yanga. 😀😀😀
 
Bora Mo ameamua kuwa kwenye michezo maana angebaki kwenye ubunge angeyumbishwa na wapenda kiki
Simba nguvu moja
 
Mambo ya uanachama ndiyo unakufa hivyo. Sasa wanunue hisa wawe wamiliki kwa njia hiyo. Watabaki kuwa mashabiki tu. Mo atapanga safu yake ya kuongoza kampuni. Hakuna tena mikutano ya kumng'oa mtu. Ukubwa wa hisa ndiyo kura yenyewe

Kwenye ulimwengu wa Hisa mwanachama = Shabiki.
 

Mfanyabiashara Mohammed Dewji 'MO' amesema ataifanya Simba kuwa klabu kubwa barani Afrika kwakua na viwanja viwili vya kisasa kimoja nyasi halisi na kingine za bandia kufuatia kushinda zabuni na kuwekeza hisa za zenye thamani ya sh billioni 20.

Mo amesema baada ya kufanikiwa kushinda zabuni hiyo anaenda kufanya mabadiliko makubwa na kuifanya timu hiyo kuwa ya kimataifa kwa kuijengea hostel za kisasa zenye vyumba 35, Mgahawa mkubwa wa kisasa, Gym yenye vifaa maalum vya wachezaji pamoja na Swimming Pool.

Mbali na hivyo Mo amesema pia wataanzisha kituo kikubwa cha kukuzia vipaji barani Afrika ili kusaidia kupatikana kwa wachezaji bora ambao watakuwa msaada kwa timu na taifa kwa ujumla.

Mo amesema kwa sasa Simba itakuwa haishindani na timu za nyumbani pekee bali na miamba ya Afrika kama TP Mazembe, Zamalek, Esparance kuwania mataji makubwa.

"Simba inaenda kuwa timu ya kisasa tutasajiri wachezaji bora wenye uwezo mkubwa, tutaboresha benchi la ufundi na miundombinu mizuri kama viwanja, hostel na mishahara mizuri kwa wachezaji wetu," alisema Mo.

Kwa sasa klabu ya Simba itakuwa katika kipindi cha mpito kabla ya mfumo huo kukamilika ambao unaweza kuchukua hadi miezi sita.

Source: SDF SPORTS
 
Kuna jamaa zetu wakazi wa jangwani wameanzisha mradi wa kuuza kalenda karenda...wahudumie timu.
 
Masikini alianza twiga akauzwa huyo akapandishwa denge leo tena simba jaman watanzania tupoje
 
Sioni hizo hisa za asilimia 51 zikinunuliwa na wanachama zote. Ikiwa michango ya kadi ya buku buku kwa mwaka ilikuwa tatizo.
Wanachama wanaolipiwa ada ya uanachama hawawezi kununua hisa hata siku moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…