Mo Dewji kumiliki hisa za klabu ya Simba baada ya kuwa muwekezaji pekee aliejitokeza

Mo Dewji kumiliki hisa za klabu ya Simba baada ya kuwa muwekezaji pekee aliejitokeza

Mo atamilikishwa VP 51% wakati serikali imesema mwekezaji amiliki 49%!
 
Bilionea Mohammed Dewji, amepita katika mchakato wa uwekezaji wa klabu ya Simba na ofa yake ya Sh bilioni 20.

Dewji amejitokeza na kuwa muwekezaji pekee ambaye aliweka dau la Sh bilioni 20 kupata hisa asilimia 51.

Hata hivyo, baada ya mchakato huo makubaliano yalikuwa ni hisa 49 anazoruhusiwa kuchukua kwa kitita hicho cha Sh bilioni 20.

Mwenyekiti wa kamati ya mchakato huo zabuni, Jaji mstaafu Thomas Mihayo amesema, Mo Dewji amepita na kitachofuatia ni majadiliano mengine baada ya mkutano wa leo.

“Mohammed Dewji ndiye mshindi, maana katika kamati yetu. Hivyo yeye ndiye amekuwa mshindi wa kuwania kuwekeza katika klabu ya Simba. Baada ya mkutano huu kutakuwa na majadiliano,” alisema.


Mkutano huo wa wanachama bado unaendelea Katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Posta jijini Dar es Salaam.

Kwa hisani ya Saleh Jembe
=======

Wanachama wanazidi kumiminika. Mabadiliko makubwa kutokea

Kaimu rais wa Simba Sports Club Salum Abdallah anawahutubia wanachama waliohudhuria Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo unaoendelea hivi sasa kwenye ukumbi wa J.K Nyerere, Dar es Salaam.


Updates

Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kumtafuta mwekezaji Jaji Mstaafu Thomas Mihayo anazungumzia mchakato mzima uliowezesha kumpata mwekezaji katika klabu ya Simba katika Mkutano Mkuu Maalum unaoendelea hivi sasa.

Simba App iko LIVE, unaweza kuangalia kwa ku-Update Simba App yako na moja kwa moja utaweza kufuatailia mkutano huu kupitia simu yako ya mkononi.
Mkuu, Itakuwa 49% kufuatana na kanuni za Serikali
 
Rais Aveva na Makamu wake Kaburu wakitoka Kunyea Ndoo Segerea wanakuta Simba Yao ipo mikononi Mwa Muhindi!
 
Apewe tu hamna namna nyingine. Wajanja Wamekula sana pesa yake.

BUT mark my words. Baada ya mwaka au kabla, ataiuza kwa hela ndefu.

Wale wenye timu yao akina Makofia watabakia kupiga kelele tu.
Tunachotaka timu iendelee kuwepo na ifanye vizuri basi. Pesa atoe mwingine, kuumia aumie mwingine! Kweli Bongo Bahati mbaya. "Kama uligombea udiwani ukiwa huna shughuli nyingine ya kukuingizia kipato, jiuzulu!" Hao makofia wako na wengine wenye akili kama zao, watafute shughuli nyingine za kufanya. Wameshainyonya timu vya kutosha!!
 
50 shares na sio 51....! fatilia vizuri vyanzo vyako vya habari mkuu...
 
Kwani nitim ya serikali mpaka watupangie bei ya kuuza
Mashabiki na wapenzi wana kazi sana ya kufika wanapohitaji kufika....

Serikali imetoa muongozo.... simba ni taasisi iliyo sajiliwa kwa kufata kanuni na taratibu zilizopo nchini... ukielewa hayo utajua nini una zungumza... kama simba ni ya serkali au ni ya kwako?
 
Usiwe unatoa comment kama nguruwe pori njoo na analysis kuonesha timu zingine zenye mfumo wa uendeshaji wa club kama huu then u criticize
Simba imekuwa kampuni... inamilikiwa na wanahisa.... Azam Fc ni moja ya kampuni, TP mazembe... Tusker, kampala city, ulinzi.... nk... fatilia zaidi nisije kukulisha matango pori mkuu
 
Mo atamilikishwa VP 51% wakati serikali imesema mwekezaji amiliki 49%!
Bado ana uwezo wa kumiliki asilimia zaidi ya 50... kwa kuwa asilimia zingine zilizobaki zitaenda kuuzwa na wadau mnunue... na hapa anaweza nunua tena labda kama kuna sheria itakataza kununua share zilizopo sokoni... pia azim ndguye anaweza nunua share zitakazo kuwa sokoni hata asilimia 1, 2, 3 or 5.... bado mke au mtoto au kampuni yake ina weza kununua share zingine zaidi zilizo baki hata 20 au 40... ndipo hapo simba inakuwa ya mtu sio watu... ktk umiliki
 
bado ana uwezo wa kumiliki asilimia zaidi ya 50... kwa kuwa asilimia zingine zilizobaki zitaenda kuuzwa na wadau mnunue... na hapa anaweza nunua tena labda kama kuna sheria itakataza kununua share zilizopo sokoni... pia azim ndguye anaweza nunua share zitakazo kuwa sokoni hata asilimia 1, 2, 3 or 5.... bado mke au mtoto au kampuni yake ina weza kununua share zingine zaidi zilizo baki hata 20 au 40... ndipo hapo simba inakuwa ya mtu sio watu... ktk umiliki
Sheria ya serikali inataka MTU mmoja awe na 49% ya hisa fuatilia ujue.
 
Tunachotaka timu iendelee kuwepo na ifanye vizuri basi. Pesa atoe mwingine, kuumia aumie mwingine! Kwel Bongo Bahati mbaya. "Kama uligombea udiwani ukiwa huna shughuli nyingine ya kukuingizia kipato, jiuzulu!" Hao makofia wako na wengine wenye akili kama zao, watafute shughuli nyingine za kufanya. Wameshainyonya timu vya kutosha!!
Mo atamiliki 49% kwa hiyo billion 20. Wengine mjiandae kununua hizo 51% zaidi ya billion 20
 
Sheria ya serikali inataka MTU mmoja awe na 49% ya hisa fuatilia ujue.
Aliye nunua hizo hisa ni MO Dewji au Metl?

Kama ni METL basi Mo ana nafasi ya kununua, kama ni Mo basi metl ana nafasi ya kununua.... kwanini nasema hivi ni kwasababu kampuni na mtu ni vitu viwili tofauti... walio sajiri makampuni wataelewa zaidi na wanasheria pia... ila washabiki na wapenzi itaitaji nguvu ya ziada kuelewa....

pia hazuiliwi mtoto au ndg yake kununua hisa zingine zilizo baki kwa kuwa ni watu wawili tofauti...
 
Apewe tu hamna namna nyingine. Wajanja Wamekula sana pesa yake.

BUT mark my words. Baada ya mwaka au kabla, ataiuza kwa hela ndefu.

Wale wenye timu yao akina Makofia watabakia kupiga kelele tu.
Atakua ametufanya mambumbumbu wa dunia
 
aliye nunua hizo hisa ni MO dewji au Metl?

kama ni metl basi mo ana nafasi ya kununua, kama ni Mo basi metl ana nafasi ya kununua.... kwanini nasema hivi ni kwasababu kampuni na mtu ni vitu viwili tofauti... walio sajiri makampuni wataelewa zaidi na wanasheria pia... ila washabiki na wapenzi itaitaji nguvu ya ziada kuelewa....

pia hazuiliwi mtoto au ndg yake kununua hisa zingine zilizo baki kwa kuwa ni watu wawili tofauti...
aisee. Makampuni nayo yananunua hisa?
 
Back
Top Bottom