Mo Dewji: Kuwekeza Simba ni hasara, nimeshatoa Bilioni 45

Sasa si aombe usaidizi kwa wanachama....
 
Mkuu, huu ndio ukweli! Nawashangaa wanaodai MO anapata faida kubwa kwa matangazo.
Tumeona GSM alikuwa anatangaziwa na timu 15,lakini akaona hakuna kitu, na kuamua kumwaga manyanga!
 
Hebu tafakari...

Azam Media wana Mkataba na Yanga wa Billions of TSh kwa MAUDHUI peke yake!!!

Je, unaamini Azam Media hawana akili hadi wawekeze pesa zote hizo kwa ajili ya maudhui peke yake?

Kwavile Yanga na Simba wana almost the same market power, sasa assume Mwamedi angekuwa ndie Mmiliki wa Yanga! Kwamba, anamiliki timu inayokula mkataba wa zaidi Sh 40 Billion (kwa miaka 10) kwa maudhui peke yake!!

Sasa linganisha huo mkataba wa Billion 40 na hiyo Billion 45 inayompa umiliki wa 49% of the club huku bado kila wakati akiendelea kulia lia kwamba anapata hasara!! Hapo hujataja mikataba ya haki za matangazo, uuzaji jezi, mikataba mingine kama ile ya SportsPesa na gharama ambayo angeingia kutangaza bidhaa kama asingekuwa anatumia Brand ya Simba!!
 
Yaani pesa ya Mwamedi full masimango...

Mwamedi wanafanana sana na Manji lakini yupo tofauti sana na GSM ambae anaona thamani anayoipata kupitia kupitia Yanga!!
 
Hujajibu swali la jamaa hapo juu halafu liko wazi kabsa ila naona unalikwepa kwa maksudi. Jamaa kauliza hivi leo hii akitokea mtu anataka kuweka 40B, Mo atakubali kuiachia kwakua anasema anapata hasara kuindesha Simba SC?!
 
Hata kama ni kweli hamna mfanyabiashara atasema anapata faida kwenye sehemu yenye faida ili wengine wasiwe interested.

Leo akitokea mwingine akisema anataka awekeze bil 40 Simba je Mo ataachia kwa ajili anapata hasara?
Nakuhakikishia nini bilioni 40 hata wa bilioni 10 hawezi jitokeza
 
Yaani pesa ya Mwamedi full masimango...

Mwamedi wanafanana sana na Manji lakini yupo tofauti sana na GSM ambae anaona thamani anayoipata kupitia kupitia Yanga!!
Umeshasahau maneno ya injinia eeh
 
Hata kama simba hampi faida ya moja kwa moja kama investment ila kuna faida nyinginezo ambazo anazipata kupitia brand ya Simba.
 
Hakuna mfanyabiashara yeyote mwenye akili anyewekeza mahala anapopata hasara!!! Mo anawafanya mashabiki wa Simba hamnazo; mtakuja kukumbuka maneno ya Kingwangalla!

Tukiacha uongo kwa sasa simba na yanga ni team za hasara but watu wanaweka pesa coz of their potential in future
After 10 years kama wataweza kuzitransform vizuri basi zitakuwa zinawapa mabillion ya pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…