SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Barua ya wazi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohamed Dewji.
Tajiri, nina neno moja kwako.
Msimu huu umefanya mambo makubwa sana pale Simba. Kikosi kinaeleweka, heshima inarudi katika ligi ya ndani na kimataifa.
Kuna uhuni mmoja ambao nafahamu unaujua maana malalamiko haya yamekuwepo kwa misimu kadhaa. Hapa naongelea kitendo cha mwendeshaji na mmiliki asiye rasmi wa Yanga, GSM kudhamini timu 8 katika ligi ya NBC.
Nakupa tahadhari kwamba mpango uliopo ni kuendelea kuongeza timu zinazodhaminiwa na GSM kwa kuzishusha kutoka katika ligi zile zinazokataa udhamini wa GSM na kuzipa udhamini zile zinazopanda. Walifanya hivyo kwa Pamba pale tu ilipopanda.
Pamoja na kwamba upinzani mkali ambao Simba inaupata kutoka haya matawi ya GSM ni faida kubwa kwa Simba kwa kuimarisha uwezo wa timu, ila ukweli unabaki kuwa nafasi ya kuchukua ubingwa wa ndani katika mazingira hayo inakuwa finyu sana. Huo ndiyo ukweli.
Kuna watu wamekuwa wanashauri na wewe utafute timu zako 8 uzipe udhamini ili mgawane pasu kwa pasu na hao GSM ila mimi naona wala hamna haja ya kutumia nguvu kubwa kulikabili hili. Ukituliza akili unaweza kuvuruga kabisa ramani yao ya vita.
Cha kufanya, tafuta kampuni ambayo itakuwa front na wewe simama nyuma yake. Kazi ya hiyo kampuni ni kutoa motisha ya zawadi kwa timu zote za ligi pale zinapocheza na Yanga. Weka kitita cha milioni 100 kwa kila mechi.
Ili kulikabili hilo, Yanga na GSM itabidi na wao waweke mzigo zaidi ya huo ili wachezaji wa hizo timu wakubaliane na hali.
Kumbuka siyo kila mechi utakayoweka dau Yanga itapoteza ila kwanza automatically utakuwa umetoboa mifuko ya hao GSM maana kila mechi utakayoweka dau inabidi na yeye atop up. Wakijifanya kukaza watafilisika. Kwa mahesabu ya haraka, GSM itabidi atumie zaidi ya bilioni 2 ili kupambana na milioni 500 yako. Wakifanikiwa kushinda hizo mechi zote utakazoweka dau, wewe utakuwa haujatumia hata sumni ila wao watakuwa wametoboka bil 2 + pesa za mikataba na hizo timu. Hapa lazima watajitathmini upya kama njia waliyochukua ina thamani.
GSM na Yanga wakiamua kutoweka dau wapambane haki bin haki, watatumia nguvu kubwa sana na lazima watadondosha points.
Ukishapata mechi zako 5 ambazo Yanga itapoteza, unafunga mahesabu yako. Kinachobaki ni Simba kucheza mechi zake kama ambavyo imefanya msimu huu. Sitegemei Simba ikicheza kwa nidhamu iliyoonyesha msimu huu, kama inaweza kupoteza point 15 ndani ya msimu mmoja.
Nina uhakika ukifanya hivi msimu mmoja au miwili kuna watu akili zitawakaa sawa.
Ubaya Ubwela.