Mo Dewji, msimu ujao tenga milioni 500 za ubingwa, baada ya hapo Yanga na GSM hawatakusumbua tena

Mo Dewji, msimu ujao tenga milioni 500 za ubingwa, baada ya hapo Yanga na GSM hawatakusumbua tena

Barua ya wazi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohamed Dewji.

Tajiri, nina neno moja kwako.

Msimu huu umefanya mambo makubwa sana pale Simba. Kikosi kinaeleweka, heshima inarudi katika ligi ya ndani na kimataifa.

Kuna uhuni mmoja ambao nafahamu unaujua maana malalamiko haya yamekuwepo kwa misimu kadhaa. Hapa naongelea kitendo cha mwendeshaji na mmiliki asiye rasmi wa Yanga, GSM kudhamini timu 8 katika ligi ya NBC.

Nakupa tahadhari kwamba mpango uliopo ni kuendelea kuongeza timu zinazodhaminiwa na GSM kwa kuzishusha kutoka katika ligi zile zinazokataa udhamini wa GSM na kuzipa udhamini zile zinazopanda. Walifanya hivyo kwa Pamba pale tu ilipopanda.

Pamoja na kwamba upinzani mkali ambao Simba inaupata kutoka haya matawi ya GSM ni faida kubwa kwa Simba kwa kuimarisha uwezo wa timu, ila ukweli unabaki kuwa nafasi ya kuchukua ubingwa wa ndani katika mazingira hayo inakuwa finyu sana. Huo ndiyo ukweli.

Kuna watu wamekuwa wanashauri na wewe utafute timu zako 8 uzipe udhamini ili mgawane pasu kwa pasu na hao GSM ila mimi naona wala hamna haja ya kutumia nguvu kubwa kulikabili hili. Ukituliza akili unaweza kuvuruga kabisa ramani yao ya vita.

Cha kufanya, tafuta kampuni ambayo itakuwa front na wewe simama nyuma yake. Kazi ya hiyo kampuni ni kutoa motisha ya zawadi kwa timu zote za ligi pale zinapocheza na Yanga. Weka kitita cha milioni 100 kwa kila mechi.

Ili kulikabili hilo, Yanga na GSM itabidi na wao waweke mzigo zaidi ya huo ili wachezaji wa hizo timu wakubaliane na hali.

Kumbuka siyo kila mechi utakayoweka dau Yanga itapoteza ila kwanza automatically utakuwa umetoboa mifuko ya hao GSM maana kila mechi utakayoweka dau inabidi na yeye atop up. Wakijifanya kukaza watafilisika.

GSM na Yanga wakiamua kutoweka dau wapambane haki bin haki, watatumia nguvu kubwa sana na lazima watadondosha points.

Ukishapata mechi zako 5 ambazo Yanga itapoteza, unafunga mahesabu yako. Kinachobaki ni Simba kucheza mechi zake kama ambavyo imefanya msimu huu. Sitegemei Simba ikicheza kwa nidhamu kama iliyoonyesha msimu huu inaweza kupoteza point 15 ndani ya msimu mmoja.

Nina uhakika ukifanya hivi msimu mmoja au miwili kuna watu akili zitawakaa sawa.

Ubaya Ubwela.
pamoja na gsm mnyama anachukua kombe zote mwaka huu NBC na shirikisho
 
Kila ukisema uache kuita watu mbumbumbu anajitokeza mmoja kukuprove wrong. Sasa kwa akili kama hizi mtashindwa kuendelea kudanganywa kuwa mafanikio ya timu ni kufungua group la Whatsapp na kuletewa Manzoki kwenye uchaguzi.
 
Moderators mnaruhusu hizi za kipumbavu
GSM ni mfanyabiashara na mwekezaji
Ni mlipa Kodi mkuu wa serikali
Leo member anasema eti hii kampuni ya GSM ni wahuni
Mkipelekwa mahakamani na haya maandiko yA kuichafua GSM Kwa kuwaita wahuni msilalamike
mbona wahuni wengi tu tunalipa kodi vizuri
 
Na ukweli unabaki vile vile uache kamdomo kakusema eti kwakuwa umefuzu kule basi Simba ni Bora acha upuuzi huo
Kwa hiyo baada ya kubadili jinsia, sasa hivi tukuite mwanamke au mwanaume au unazo zote mbili?
 
Uwa anakurupuka na viroja badala ya hoja,,nimeona Kuna Uzi unasema hapa jukwaani Kuna wajinga wengi wanaleta hoja za kipuuzi puuzi alikuwa sahihi
Ule Uzi hata Mimi nimeuona na Kwa watu Kama huyu mleta mada nikaamini kweli Kuna wajinga wajinga humu
 
Nadhani utakuwa umejifunza. Ukinijia njoo kwa adabu.
Kujifunza nini labda? Kujifunza ujinga wako wa kusema Simba ni Bora ama kujifunza habari ya GSM kudhamini timu 8 na kumshauri Mo na yeye adhamini timu? Mbona ueleweki? Yani Mimi nijifunze kwako huo utahira?
 
Kujifunza nini labda? Kujifunza ujinga wako wa kusema Simba ni Bora ama kujifunza habari ya GSM kudhamini timu 8 na kumshauri Mo na yeye adhamini timu? Mbona ueleweki? Yani Mimi nijifunze kwako huo utahira?
Nafikiri mimi na wewe tumemalizana....mwingine!
 
Moderators mnaruhusu hizi za kipumbavu
GSM ni mfanyabiashara na mwekezaji
Ni mlipa Kodi mkuu wa serikali
Leo member anasema eti hii kampuni ya GSM ni wahuni
Mkipelekwa mahakamani na haya maandiko yA kuichafua GSM Kwa kuwaita wahuni msilalamike
Tuvumilie tu mkuu Mh. Rage alishasema kwamba mashabiki wa Simba ni mbumbumbu!
 
Tunahitaji Tone Tone Kwanza Kutoka Kwenu Mashabiki Kindakindaki Wa Simba Alafu Tutaona Namna Ya Kumshauri Mwenyekiti Nae Atie Tone Lake...###Hapovipi###
 
Utawaponza jamii forums
We unaita kampuni ya mtu wahuni
Kisa upofu wako wa ushabiki wa mpira
Wazazi nje ya haya mashabiki
Sio sawa kuwaita GSM wahuni
Mhh hebu huko na wewe yani GSm ndo nani sasa...yani wasisemwe wao ni kina nani
 
Ukiona adui yako anakulalamikia ujue upo sahihi, ukiona anakusifia ujue kuna sehem unafeli! GSM endeleeni kakaza hapohapo hivi vilio ni ishara njema kwetu sisi wadau[emoji1787][emoji1787]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]upo sahihi mkuu
 
Back
Top Bottom