Mo Dewji na GSM anzisheni timu zenu

Mo Dewji na GSM anzisheni timu zenu

Hizo Yanga na Simba waachieni kina Mpili na Manara (Waswahili).

Bakhresa aliona mbali akaanzisha timu na uwanja wake. Yupo huru kutumia hela yake pasipo majungu yoyote.

Yanga na Simba mtapoteza hela zenu na mwisho mlipwe matusi na dharau kutoka kwa maskini wasio na mbele wala nyuma.

Mtu hachangii hata mia kwenye timu ila anamtukana mfadhili aliyetoa bilioni 41 kwa kipindi cha miaka 4 tu.
Naunga mkono wanaweza kukuza brand zao na maisha yakasonga
 
Wamiliki wa Mtibwa Sugar na Kagera Sugar ni mfano.
Sijui ni mwaka gani timu hizo mbili ziliwahi kupata faida, lakini zinasajili, zinashiriki ligi na Mtibwa iliwahi kupata Ubingwa na hivyo kuwakilisha nchi kimataifa.
Hawa wengine wanaangalia faida watakazopata baada ya muda mfupi.
Kwa kuwa wamekuja kutafuta faida za haraka wajiandae na matusi, kashfa na dharau.
 
Good hili jambo la Mo and GSM kuja (brand new) team mpya kama Azam instead of Simba na Yanga lingefanya ligi yetu kuongezeka ushindani as you know mpira demand a lot of financial muscles. Ila all the best kwao kwani kila mtu huwa na maamuzi yake na mapenzi yake alafu wanafurahia wanachokifanya na wana enjoy sana either kuwa part of simba au yanga badala ya kuleta kitu kipya(New Challenge) kama Azam ila pia all the best pia kwa bakhresa family wanajitahidi sana na wanapoelekea nuru inaonekana jambo bora wa jaribu kurekebisha badhii challenge wanazo kutana nazo ili Kuboresha team ya azam ili makombe ya ligi kuu wa wachukue Mara kwa Mara yani continuous I hope wakichukua makombe Mara kwa Mara ndani ya miaka 10 au 15 watakuwa na fan base kubwa sana.
 
Hizo Yanga na Simba waachieni kina Mpili na Manara (Waswahili).

Bakhresa aliona mbali akaanzisha timu na uwanja wake. Yupo huru kutumia hela yake pasipo majungu yoyote.

Yanga na Simba mtapoteza hela zenu na mwisho mlipwe matusi na dharau kutoka kwa maskini wasio na mbele wala nyuma.

Mtu hachangii hata mia kwenye timu ila anamtukana mfadhili aliyetoa bilioni 41 kwa kipindi cha miaka 4 tu.
Hasa Mwamedi.
 
Unachokishauri ni sawa ila hizo timu watakazoanzisha zitaishia kua timu za kawaida tu kwasababu ya hulka iliyopo nchi hii.Ili timu zingine ziweze kufikia hayo mafanikio ni lazima kwanza dominance ya simba na yanga ife.Tofauti na hapo ni ngumu sana kwasababu hizi timu kwa miaka mingi zimetawala mpira wa hii nchi na kubadilisha ilo inaitajika nguvu ya ziada sana kuanzia mentalit ya viongozi wa serikali hadi mashabiki.Hilo peke yake ndilo litakalotutoa hapa tulipo.
 
Hizo Yanga na Simba waachieni kina Mpili na Manara (Waswahili).

Bakhresa aliona mbali akaanzisha timu na uwanja wake. Yupo huru kutumia hela yake pasipo majungu yoyote.

Yanga na Simba mtapoteza hela zenu na mwisho mlipwe matusi na dharau kutoka kwa maskini wasio na mbele wala nyuma.

Mtu hachangii hata mia kwenye timu ila anamtukana mfadhili aliyetoa bilioni 41 kwa kipindi cha miaka 4 tu.
Unaikumbuka African Lyon baadae Singida United?

Hizi ni timu alianzisha MoDewji lakini zote ziliangukia pua. Kumiliki timu mpaka ifikie kupata mashabiki wengi Kama Yanga ama Simba ni shughuli pevu
 
Umeongea vizuri ila umechanganya kidogo.
Kwanza GSM ni mdhamini tu anaweza kuondoka siku yoyote kwaiyo wanachama wana haki kuongea pale wanapoona kuna shida.
Mo kawekeza Simba kwa kununua sehemu 49% ya club kwa 20b Sasa hiyo 41b sijui umepata wapi na pia bado wanachama wana nguvu ya kuhoji wanapoonda mambo yanaenda ndivyo sivyo kwa sababu hajanunua club yote.
Kwenye suala la kuanzisha timu zao hapo nakuunga mkono 100%, maana sijawahi kuona S.S.Bakharesa akipigiwa kelele na Azam yake au Seif na kaka yake Nassoro wa superstar/superdoll wakipigiwa kelele na timu zao Mtibwa na Kagera sugar
 
Azam alishafeli kwa kuiga siasa za simba na yanga, ila angekua anachukua mataji, anafanya vizuri mashindano ya CAF mashabiki wengi tungehamia kwake!

kuna kampuni imewahi kufanya utafiti wa loyalty in sports especially football, wakagundua only 15% ya mashabiki ni loyal, wengine hufuata mafanikio, na hii ina apply hata bongo!

kama liverpool, utd na arsenal zimepoteza mashabiki kwa city na chelsea, bila shaka hata Azam angekua serious tusingekua hapa........ tatizo wabongo tunaendesha timu kisiasa kisha tunaishia kuilaumu tff
Umeandika ukweli.

Zamani nilikuwa Yanga.

Sitaki stress kabisa! [emoji7][emoji1732][emoji41]
 
Huwezi kupata mashabiki bila kushinda mataji
watu wengi tulifurahia ujio wa Azam, lakini wakaiga siasa za simba na yanga kusajili majina.... ikaja mbeya city watu tukafurahi nao siasa za hapo mbeya za ccm na chadema zikawaponza wakapoteana!

wabongo wengi tunatamani zitokee timu walau mbili zilizo bora kuliko simba na Yanga, zitakazokua focused na mendeleo ya mpira (miundombinu, marketing na kushinda mataji ya ndani na nje)...hizi simba na yanga zitapotea automatically
 
Hata hao matajiri wanalijua hilo na wanaliona ila itakuwa hasara kubwa kwao,kuhudumia timu kwa viwango vizuri kwa siku si chini ya milioni 5 posho chakula,malazi na mambo mengine,hawawezi hawa matajiri wetu kutupa fedha zao.wote wanataka faida ya haraka na ya uhakika.
 
Back
Top Bottom