Mo Dewji nakuheshimu, ila unakoelekea sasa utaharibu na utaanza hata Kutukera na Sisi tunaokubali 'Kutukanwa' kwa ajili ya Kukutetea Mitandaoni

Mo Dewji nakuheshimu, ila unakoelekea sasa utaharibu na utaanza hata Kutukera na Sisi tunaokubali 'Kutukanwa' kwa ajili ya Kukutetea Mitandaoni

Umewasilisha mawazo yetu wengi, nilikua namtetea sana ila jana kaonyesha ujinga wake na ukweli wa yale maneno ya Haji. Inabidi abadilike au atuachie timu yetu.
 
Maoni yangu,

Simba imeshabadili mfumo wa kiuwendashaji,ni wazi hata akitoka Mo sasa hiv itapata tajiri wa kuwekeza haraka sana..

Ila tatizo litakuja pale atakapodai hzi fedha alizotumia mpk sasa ambazo ni 21B ndio zitakua kikwazo kwa mwekezaji mpya,maana lazma afikirie jins ya malipo ya hilo deni..Hapa ndio Mo anaporingia na alipowashikia wana simba sasa hiv.

Angalizo; kwa tabia za kihindi kama za huyu bwana si ajabu hataki wanasimba hasa viongozi au wachezaji wawe na mawasiliano na Manara na wasipokua makini wajiangalie pia uwenda mawasiliano yao yamehakiwa pia kwa baadhi yao..

Kila anapokaa anahisi anahujumiwa tu sasa,na mtu anaemuamin ni babra tu ko makelele yetu wala hayatasaidia chochote.
 
Ndugu Gentamycine tulikuonya sana na ukajawa na matumaini hewa.Huu ni mwanzo tu next utaandika kitabu kabsa huku ukiwa unabubujikwa na machozi.Manara anajaribu kuwafumbua macho muone mbele kuna nini lakin hela za mhindi zinawaziba hahahaa.
 
Mo Dewji leo utanisamehe sana Mimi GENTAMYCINE ambaye nina tabia ya kutopenda Unafiki, Kumnyenyekea Mtu, Kujipendekeza kwa Mtu au hata Kumuogopa Mtu hata kama ni Msomi sana su Tajiri mno na hata Wazazi wangu, Ndugu na Marafiki zangu wanalijua hili kwani ndivyo nilivyoumbwa na sitobadilka hadi Umauti wangu.

Mo Dewji Wewe ni Mwekezaji wa Klabu yetu ya Simba ila hujapewa Mamlaka ya Kumiliki ( Kuzimiliki ) Akili zetu ambao kuna wengine tunajua tuna Uwezo mkubwa wa Akili Kukuzidi ila labda ulichotuzidi ni Pesa, Mali ( Utajiri ) na bahati tu.

Mo Dewji ni Mimi huyu huyu GENTAMYCINE nilianzisha Uzi hapa JamiiForums kukutaka usijiingize kabisa katika Mtego wa Kujibizana na aliyekuwa Msemaji wetu Haji Manara na badala yake utuachie Sisi Mashabiki tutapambana nae kwani tunamjua na tunammudu.

Mo Dewji kwani Mchezaji Clatous Chota Chama akimpongeza 'Adui' yako wa sasa Haji Manara Wewe unapungukiwa na nini? Kwanini unapenda sana kutaka 'Kunyenyekewa' na wana Simba SC wote kana kwamba Wewe ni Mungu Mtu?

Mo Dewji hivi Matajiri wakubwa Wenzako kama akina Aliko Dangote, Patrice Motsepe, Moise Katumbwe Chapwe, Said Salim Bakhressa, Roman Ibrahimovic, Carlos Slim, Bill Gates na Roca Fella nao wana ' Utoto' huu kama wako?

Sasa leo hii Wewe Tajiri Mo Dewji ukianza kuwa na Uswahili wa Kujibizana na Haji Manara au wale 'wanaompenda' je, Sisi Mbayuwayu ( Masikini ) kama akina GENTAMYCINE tufanyeje? Nisikufiche Mo Dewji unaboa na umeniboa mno tu.

Mo Dewji hukupewa Dhamana ya Kuwekeza Simba SC ili utunyanyase, tukuogope, utupande Vichwani, utufanye utakavyo na tukuone Mungu Mtu sawa? Na usidhani ikitokea 'ukasusa' Simba SC na Kuondoka basi tutaabika mno kwani kwa 'Brand' ya Simba SC ya sasa hata ukijitoa leo wapo Matajiri wengine wakubwa tu Mwenyezi Mungu atatuletea na Simba SC yetu itaendelea vyema tu.

Mo Dewji Mwenyezi Mungu hakukupa huo Utajiri wako ili unyanyasie Watu, tukutukuze au tukulambe Miguu bali umepewa Utajiri huo mkubwa ili ushirikiane na Sisi Masikini ( Mbayuwayu ) akina GENTAMYCINE wenye Akili Kubwa kukuzidi ili kwa pamoja tushirikiane na tuipatie Mafanikio ya Uwanjani na nje ya Uwanja Simba SC yetu sawa?

Mo Dewji aliyekuwa Msemaji wa Simba SC Haji Manara alipokusema ( alipokunanga ) Wiki hii wengi ( GENTAMYCINE nikiwemo ) tulikataa Kumuamini ila kupitia huu Upuuzi wako kwa Mchezaji Clatous Chota Chama nami sasa niseme tu kuwa kwa 65% naanza Kuyaamini baadhi ya Madai ya Haji Manara juu yako.

Mo Dewji hivi hujifunzi tu hata kwa Msanii Nasib Abdul ( Diamond Platinumz ) ambaye kutwa ananangwa ( anasemwa ) vibaya tena hadi 'Kudhalilishwa' na akina Mwinjaku lakini Kijana wa Watu ( Diamond ) hajathubutu hata Kujibizana nae Mitandaoni na katika Vyombo vya Habari. Ina maana hata Diamond Platinumz anakushinda Uvumilivu na Uungwana dhidi ya Maadui ( Enemies ) na Watesi ( Critics ) wako?

Mo Dewji nakuheshimu mno ila kwa hili ulilolifanya nisamehe sana ila niseme tu umekosea zaidi na sidhani kama Tajiri wa Mfano wako anatakiwa kuwa na 'Vijitabia' vya Utoto Utoto, Ukike Kike na Uswahili pamoja na Ushambenga kama unavyoanza kutuonyesha.

Bado hujachelewa Kubadilika na bado GENTAMYCINE sijakata Tamaa juu yako na Kukuheshimu ila nakuomba tu Jitathmini na fanyia Kazi haya niliyokusema na Kukushangaa nayo hapa. Ni kweli wana Simba SC tunakupenda na Kukuhitaji kwa Mafanikio makubwa yaliyotokana na Uwekezaji wako mkubwa ila hatutaki utunyanyase, utupelekeshe utakavyo na utufanye tukuone Wewe ni Mungu wakati Mimi najua Mungu ni Mmoja tena Yule wa Ibrahim, Isaka na Yakobo kwa Sisi Wakristo.

ID yangu hii Dawa ya GENTAMYCINE ( ANTIBIOTIC ) inayotibu Matatizo Sugu ya Mwilini hivyo naamini kwa haya niliyokuambia hapa yatakuponya nawe pia na utabadilika na uanze kuishi Kiustaarabu kama Matajiri wakubwa Wenzako duniani.

Hakuna aliye juu ya 'Klabu' hii ya Simba.
[emoji106][emoji106][emoji106]
 
mo anainyonya simba ila watu hawajajua tu, jezi kazijaza makoro koro yake alafu daily eti anasema hapati faida, alafu kwa alichofanya jana kajidhalilisha sana maana anatufanya tufikiri wachezaji wa simba ni wafanyakazi wake na si wafanya kazi wa simba, pia chama kwa kua aliomba samahani hakupaswa kuendeleza ujinga wake maana alionesha dhahiri anadharau ya kiwango cha juu.
 
Huyu Mo si anyamaze huu upepo mchafu upite mbalimbali Mambo yaendelee maana sasa anajizalilisha na kuonyesha true color yake Hadi Manara anaonekana yuko sahihi, kanisikitisha sasa kwa hii tabia yake anakua ka wanawake wa uswahili bwana, no classy at all. Hii issue ni yeye anaikuza si atulie huu upepo utulie ndo afanye yake.
Kanilazimisha taratibu sasa nianze Kumuamini Haji Manara japo nae ( Haji ) ana Mapungufu yake.
 
Shida ilianzia hapa...
IMG_20210807_170439.jpg
 
Hii tabia ndiyo ilimfanya Nkwabi akajiondoa kupost mafumbo Twitter na ajue kwenye hizi timu akiendeleza tabia zake kuna siku atanaswa vibao mpira unashabikiwa mpaka na watu wa kila aina na mnapokuwa pamoja wote hujiona wako sawa.
 
Maoni yangu,

Simba imeshabadili mfumo wa kiuwendashaji,ni wazi hata akitoka Mo sasa hiv itapata tajiri wa kuwekeza haraka sana..

Ila tatizo litakuja pale atakapodai hzi fedha alizotumia mpk sasa ambazo ni 21B ndio zitakua kikwazo kwa mwekezaji mpya,maana lazma afikirie jins ya malipo ya hilo deni..Hapa ndio Mo anaporingia na alipowashikia wana simba sasa hiv.
hawezi kudai kitu, unadhani matangazo ya bidhaa zake kwenye jezi ndani ya miaka 4 ni sawa na sh ngapi? je, kungelikua na mkataba alipaswa kutupa bei gani? alichotuweza mudi ni kuwaweka karibu watu wenye nguvu simba ili atimize malengo yake ya kujinufaisha kupitia brand ya simba.

mimi kila nikitafuta sababu ya mo kuitumia brand ya simba kutangaza bidhaa zake bila mkataba ukweli siipati.
 
Back
Top Bottom