MO Dewji: Nataka kuwekeza bilioni 20 Simba

MO Dewji: Nataka kuwekeza bilioni 20 Simba

Hivi huyu ndio yule muhindi wa SINGIDA UNITED ama? Sorry, wrong post. Namaanisha African Lyon
 
Kwanini jamaa amekomaa hivi kuichukua simba?? Anataka nini?? Kwanini asigombee kama manji yanga?? Ni kweli tunataka MO atusaidie ila sio kwa mfumo wa hisa......... lakini pia zile timu za k/koo zina mashetani akichukua MO na bado simba ikaendelea kufanya vibaya utasikia tena kelele za MO OUT
 
Simba ni club ambayo ni association ambayo ni mali ya wanachama na sii kampuni mtu ajitokeze kununua hisa. Ila ndani ya klabu inaweza kuanzisha a subsidiary public company ya SSCC isajiliwe kama Public Company ifanye IPO ya 51% stake ya hiyo IPO ndio issued kwa MO kwa hizo bilioni 20 zake halafu ile 49 stake inabaki kwa wanachama. Vinginevyo katiba ya SSC ibadilishwe kutoka club iwe kampuni, na hizo shares ziwe floated kwa public MO azinunue kama deserving na sio kuuziwa kwa preferential.
pasco
huo n ukwel mtupu na ndio watu hawatak kuusikia
 
Tatizo la Simba sio pesa, tatizo la Simba ni uwekezaji kwa wachezaji wanaostahili kuchezea Simba. Menejimenti iliyopo pia ni tatizo, ni aibu kwa klabu kama Simba wachezaji kulalamikia mishahara.

Na hauwezi kuinua soka la bongo kwa kuiwezesha Simba. Tunatakiwa tupate timu nyingine kama Azam, ili kuongeza ushindani. Hizi billion 20 ni nyingi sana kama anapenda kuwekeza katika soka. Lakini kuna nini anachokihitaji Simba zaidi ya black markets?
Azam Yanga ziko vzr pia zinasaidia katka soka la bongo...Simba pia ikiwa fit nadhani timu nyingine na uwekezaji kama wa Mo unaweza tokea..Mpira ni Pesa sio ndumba sasa wabongo wajue..
Ofcz lazma Mo ana interest yake sio mjinga ni mtu smart sana japo nina amini anaMapenz makubwa na Club Ya Simba
 
Simba ni club ambayo ni association ambayo ni mali ya wanachama na sii kampuni mtu ajitokeze kununua hisa. Ila ndani ya klabu inaweza kuanzisha a subsidiary public company ya SSCC isajiliwe kama Public Company ifanye IPO ya 51% stake ya hiyo IPO ndio issued kwa MO kwa hizo bilioni 20 zake halafu ile 49 stake inabaki kwa wanachama. Vinginevyo katiba ya SSC ibadilishwe kutoka club iwe kampuni, na hizo shares ziwe floated kwa public MO azinunue kama deserving na sio kuuziwa kwa preferential.
pasco

kweli kabisa. Nadhani hiki ndicho anachomaanisha Mo
 
Mimi I DONT CARE, kama anataka kupiga hela nyingi nae poa tu, ila nijuacho atakuwa anawajali wachezaji na in return wana simba tutaanza kufurahi tena kwa kushonda vikombe ndani na nje ya Tz, APEWE TU TIMU.
Mo ni simba damu, nimewachoka hawa "wazungu" wa sasa na Aveva wao.
 
Huyu ndo katangaza kugawa nusu ya utajiri wake..
Karibu Tsh bilioni 600,,
bora ajenge vyuo vikuu na mahospitali,atabakiza legacy ya kudumu hapa duniani
 
Binafsi sikubaliani na MO kupewa simba, hii lugha anayosema Leo ni lugha ya kuvutia tu sio uhalisia.. Atueleze kwa nini alishindwa kwa African Lyon...!
Kuna kitu kinaitwa FAN BASE, huwezi linganisha timu yoyote hapa E. Afrika na Simba au Yanga, zina mtaji tayari wa mashabiki, ni jinsi ya kuwatumia tu, A.Lyon alishindwa sababu timu haina Fan Base, hata Azam yenyewe haina mashabiki isipokuwa wa mkopo, wakicheza na yanga wanapata wa simba na wakicheza na simba wanapata wa yanga!
 
Forbes wanasema Mo ni tajiri kumzidi hata Azam na yeye hajawahi kukanusha, sasa kama Mzee Bakhresa alikuwa mnazi mkubwa wa Simba lakini 'uswahili' ukamchosha na kwa mafanikio makubwa kaanzisha timu yake mwenyewe ni kwa nini naye asianzishe yake!? Huyu ana lake jambo na ndio maana alianza kwa kujinadi eti atagawa nusu ya mali zake wakati wafanyakazi wa makampuni yake wakiwa hoi!
 
Huyu ndo katangaza kugawa nusu ya utajiri wake..
Karibu Tsh bilioni 600,,
bora ajenge vyuo vikuu na mahospitali,atabakiza legacy ya kudumu hapa duniani
Unaweza sema hivyo, ila kuwekeza simba na kama wewe ni majority shareholder, mtaji unarudi haraka sana! Simba ni brand ambayo watu wameshindwa kuitumia, nina uhakika Mo ataweza na atafaidika yeye pamoja na timu.
 
Simba ni club ambayo ni association ambayo ni mali ya wanachama na sii kampuni mtu ajitokeze kununua hisa. Ila ndani ya klabu inaweza kuanzisha a subsidiary public company ya SSCC isajiliwe kama Public Company ifanye IPO ya 51% stake ya hiyo IPO ndio issued kwa MO kwa hizo bilioni 20 zake halafu ile 49 stake inabaki kwa wanachama. Vinginevyo katiba ya SSC ibadilishwe kutoka club iwe kampuni, na hizo shares ziwe floated kwa public MO azinunue kama deserving na sio kuuziwa kwa preferential.
pasco
hisa ziuzwe wazi, si ajabu bakhresa akaweka mzigo wake, binafsi japo yanga nitanunua kama uwekezaji......
hesabu za 20bn kuwa 51% alizipataje?
 
Sidhani kama upo sawa......udhamini wa TBL unaisha na hamna dalili za kuongeza.
Tatizo la pesa lipo Simba ndo maana hata mishahara ya wachezaji inachelewa
Pia kuna kipindi viongozi wa timu walikuwa wanalalamika kuwa wanatumia pesa yao kuendesha club
 
Hapa tusidanganyane, mpira ni biashara na Mo ni mfanyabiashara. Ni upuuzi kusema asipewe timu kisa atafaidika. Tujiulize sasa hivi timu ni ya wanachama ww kama shabiki unafaidika nini zaidi ya ushindi wa timu? Mo kawapa changamoto ni wakati wa wanasimba kubadili mfumo timu iwe kampuni wenye kutaka hisa wanunue tusioweza tubaki ushabiki.
Kila siku tunashabikia timu za ulaya huwa tunafaidika vipi?
Tuache roho mbaya, mwenzetu kaona hii fursa kama tuna uwezo tucompete nae kwa kupanda dau na si majungu
 
Mfanyabiashara kijana na mwenye mafanikio makubwa nchini, Mohammed Dewji amesema angependa kuwekeza Simba ili kubadili mfumo.

Dewji maarufu kama “MO”, amewaambia waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo jijini DAr es Salaam kwamba bajeti ya Yanga na ile ya Azam FC ni mara mbili ya ile ya Simba, jambo linaloifanya klabu hiyo kuendelea kubaki kuwa msindikizaji.

Tayari Mo amesema yuko tayari kutoa Sh bilioni 20 ili kununua hisa asilimia 51 na kuwekeza ndani ya Simba.

“Kama unataka mafanikio kwenye mpira, hakuna zaidi ya fedha. Simba haiwezi kuwa na miaka 80 leo haina hata uwanja wa mazoezi.

“Unajua kama nikiwekeza fedha hizo, tunaweza kuzipeleka kwenye mkopo na kuikopesha serikali. Baada ya hapo tutapata faida ya dola bilioni 7.5 ambazo tutaziingiza kwenye maendeleo.

“Mimi ninaamini Simba haiwezi kubadilika kwa kuwekeza kwenye bajeti ya Sh milioni 500 kwa mwaka. Haitawezekana, ndiyo maana nimekuwa nikisisitiza, kwanza Simba inahitaji muwekezaji na si mdhamini.

“Nisisitize hili,mimi ni mwanachama wa Simba, ninaumia kuona timu hii inakwenda hivi. Ndiyo maana ninaingia nikiamini nitaweza kubadilisha mambo kwa kushirikiana na wanachama wa Simba ili kuleta mabadiliko katika klabu yetu.”

good move kwa Simba wakikubali.
 
Back
Top Bottom