Mo Dewji ni tapeli na bora imeonekana mapema

Mtaendelea kudumazwa akili siku ya siku mungu akiwazindua akili mtajiona mmeachwa
 
mi nilishangaa kwenye mechi na Ud songo anatangaza pikipiki za boxer wakati mkataba wake na simba ni mo xtra ila kati ya vitu alivyoniuzi ni kuacha mchezaji mzuri kama Okwi kwa sababu anataka pesa nyingi wakati ametuaminisha anataka kushindana na Mazembe kiukweli kama mwekezaji inabidi awe na malengo ya muda mrefu na mfupi malengo ya muda mfupi ni kusajili wachezaji bora wakati malengo ya muda mrefu ni kuandaa vijana, kuwa na uwanja pamoja na viwanja vya mazoezi tumpe muda labda atajirekebisha
 
Barcelona ilipomsajili Arturo vidal alikuwa na umri gani? Na Je, uliwaelewa Barca katika hilo?

Tunajua vijana ni muhimu ila usitake kutudanganya kwamba tutakwenda klabu bingwa tufanikiwe na wachezaji wadogowadogo tu , hata hiyo Madrid na Barca ili uwe first eleven na umri mdogo lazima uwe na kiwango ambacho kinawazidi hao wenye umri mkubwa au kinalingana nao.Eg De Jong , Arthur , Nacho , Isco , carvajal sasa hawa vijana wetu akina Salamba utegemee wakufikishe Robo fainali klabu bingwa si utakuwa una shida sana kifikra?

Simba ipo sawa kabisa , na moja ya mkakati wake ni kuwasaidia vijana kupitia timu ya vijana lakini wakati huo wazee lazima wawepo kupambana kwa matokeo ya sasa.
 
Okwi alikuwepo wakati tunafungwa zile 5 5 hivyo hiyo si excuse kabisa , katika ulimwengu wa soka unatazama bajeti yako na umri wa mchezaji mwenyewe atakusaidia kweli au atakuja kuwa tiamaji tiamaji maana yule nae umri si haba.
Yaani ukiwa na umri wa miaka 29 ulipwe milion 80 ila ukiwa na umri wa 32 unataka ulipwe mil 115 inakuja vipi hiyo?

Tuwe honest tu timu bado ni nzuri
 
acha blaablaa weka na weww mzigo mezan tukupe.timu...Nataman nikutukane sema tu naogopa bann
 
we
 
Mbna inajulikana wazi Mo dewji ni msanii tu pale Simba...
 
Ndio matatizo ya kuchamba kwa kutumia mkono wa kulia.Naona umeandika ukiwa ndani ya Milembe hospital
 
ila wale wabrazil, wamepigwa mchana wa saa 8 Jua kali. Yaani wale jamaa ni weupee amna kitu. Bora Mlipili na Ndemla ila sio hao wabrazuka
 
Umeanza lini kuishabikia Simba maana kama hujui kuwa Simba kuna kipindi cha misimu mitatu mfululizo ilitumia wachezaji vijana wakititokea Simba B kina Mkude, Ajib, Singano,Mwanyika, Ndemla,Lucian,Isihaka Hassan, Miraji Athuman na kwa kipindi chote Simba ilikuwa inafukuza kivuli cha kupata ubingwa na hatimaye ilibidi hakuna namna zaidi ya kuingia sokoni kutafuta wachezaji waliokomaa na wazoefu na matunda yalionekana labda wewe bado umelazwa Milembe hospitali
 
Unaonekana una chuki binafsi ndugu, afu utakuwa ndio umeanza ushabiki, afu unaonekana sio shabiki wa simba!! Rudi nyumbani afu ujipange namna ya kutengeneza hoja bila kujulikana identity yako
Huyo jamaa ni ZIRO kabisa hana hoja ni mtuupu kabisa hivi FACTS zipi hasa unazoejea kwa MO?
 
Mleta Ufyuzi Ni Pumba Kabisa! Yaan Unatishia Kunya Aaf Unaishia Kujampa?? Kama Umevurugwa Nakina Falcao Wenu A.K.A Molinga Peleka Malalamiko Yako Kwamzee Wa Suti 100
 
Anatujengea uwanja wa bunju kwa pesa yake mwenyewe...una swali jingine???
Ndo mnavyojidanganya ? Atajenga uwanja wa pesa zinazotokana na Simba. Hujiulizi mpaka leo hajaanza kujenga kwa nini?
 
Nimefanya jambo la busara san kuanza kusoma comment najua ningetukana tu we wasikilize hao ,unazani wananchi wa mbagala ndy sawa na wacatalan ,wameitana kijiji kizima kuchangia timu B haijafika leo katokea mtu unamuona tapeli ,alafu kila kitu kinafata shelia akishindwa yeye anaondoka timu inabaki povu la nn ,ivi simba na PSG nani katumia pesa sokoni mbona hawapigi kelele wewe hujatoa ata mia mineno gunia saba au mchawi wewe maana wachawi ndy hawapendi maendeleo ,tumetumia vijana wametusaliti hujaona na sababu ilikuwa njaa au unajisahaulisha unajua sababu ya mkude kuvuliwa unahodha ajibu na wenzie kutukimbia ni njaa acha upimbi wew .
 
Anatujengea uwanja wa bunju kwa pesa yake mwenyewe...una swali jingine???
tuliambiwa mwezi wa tano nyasi zitakua tayari na hostel na vyumba vya mikutano vitaanza kujengwa, nini kinaendelea bunju?
 
Peleke Hoja yako kwenye vikao halali vya wanachama au uongozi, itafanyiwa kazi Kama unania njema.
Kwakuwa huyo mwekezajia amefuata hatua zote halari za uwekezaji.
Na ameruhusiwa kwa baraka zote za Wanachama wa Simba na Viongozi wa Simba na Serikali.
Awe amefaulu au kutofaulu katika uwekezaji wake bado haiondoi dhamana yake ya kuwa mwekezaji.
Ungelikuwa na nia njema, ungelitarajiwa kushauri namna Bora ya kuboresha juhudi za timu ya Simba kufikia malengo yake chanya yanayotarijiwa na sio kutoa kashfa na kebehi mitandaoni kwa majina bandia.
Kumwita muwekezaji huyo tapeli ni kumvunjia heshima yake katika jamii ni kosa kisheria na ni matumizi mabaya ya mtandao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…