Lamzettttt
JF-Expert Member
- May 28, 2020
- 1,218
- 3,481
Boss Mo tuletee Mayele
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaha, Kafanye kazi mkuu, mkeo unamuweka rehani kwa kujikita na Yanga unaacha kazi.CHA USHINDI WA 5 + 2 + 1 = 8 = nanenane DAY
BTW, wewe hukufanikiwa kuweka mke rehani kama Mwijaku??
Moanzu yuko wapi?Leo sitasema sana maana yanayotakiwa kusemwa nimeshayasema kwa siku kadhaa sasa zilizopita.
Baada ya hongera nitaongeza neno moja tu kwa Mwekezaji Mo Dewji. Baada ya usajili mzuri ambao kiukweli unaridhisha sana na kabisa unaona watu wa maana wanaojua mpira walikaa chini wakapanga kujenga timu ya maana.
Midfield itakaa vizuri wala sina wasiwasi nayo. Kwa upande wa beki, Kapombe na Zimbwe wawe kwenye kwenye rotation, mbadala wao wapo tena wenye viwango, hakuna tena visingizio. Tusikariri kikosi na tujenge ujasiri wa kuweka watu benchi. Kwa kipa tuna Camara, tuna Lakred, tuna Abeid....Mungu atupe nini tena jamani?
Pungufu moja kubwa ambalo linaweza kuja kuicost timu ni uhaba wa striking force. Freddy hawezi kwenda na speed ya hii timu. Imagine Yanga ina options kama Musonda, Dube, Baleke, Mzize, nk. ila Simba hata option ya kwanza bado ina mashaka. Nitampa muda zaidi kidogo Mukwala ila hajaonyesha kama ni katili na mtumiaji mzuri wa nafasi.
Ushauri wangu, kama muda unaruhusu arudi sokoni atafute striker wa maana, atanishukuru baadae. Simba ya sasa ni nzuri sana ila itakwamishwa na ukosefu wa mshambuliaji katili ambaye mambo yakiwa magumu ana uwezo wa kuibeba timu katika mgongo wake. Ukosefu wa mshambuliaji tishio utawapa pressure na kuwachosha sana mabeki wa Simba. Wote tuliona leo ilivyofika dakika ya 60 jinsi beki ilivyochoka hadi wakaanza kupoteza umakini na mipira.
Nyongeza, Mutale ana speed nzuri na uwezo wa kupiga chenga ila hana good touch na pia hana good timing kusoma kwa haraka movement na maamuzi ya mtu anayemkaba. Hilo inabidi lifanyiwe kazi haraka, anaanza kunipa wasiwasi kuwa anafuata nyayo za Saido.
Mutale ni kisinda aliyechangamkaHoja kuhusu Mutale 💯 true. Ni machachari si hatari, anahitaji msasa.
🤣🤣🤣MCHUKUUE KIBU, MUTALE, DEBORA, NA AWESU AWESU WAWEKE KWENYE BRENDA SAGA KWA DAKIKA MOJA KISHA TIA SHABALALA NA KAPOMBE KIDOGO SAGA TENA KISHA TIA SHABALALA NA KAPOMBE SAGA TENA KISHA TIA MZAMIRU NA MUKWALA KWA MBALI SAGA KIDOGO TENA HALFU WEKA BALUA VIJIKO VIWILI NA FONDO MALONE KIJIKO KIMOJA HALFU KOROGA VIZURI NDIO UNAMPATA PROFESA WA MPIRA PACOME ZOUA ZOUA😂😂😂😂🙌🏻🙌🏻
Shabiki wa ovyo asiyeweza kushauri maboresho ya timu yake zaidi ya kuwaambia wanapima umri.Mzee wa Utra Sound.
Mzamiru alipangwa kwa kazi maalum kuwaonyesha wachezaji wapya jinsi Derby inavyochezwa maana wakizembea watapigwa hata 10. Kuna defense line inayocheza kwa kutumia nguvu kama ya Yanga chini ya Aucho?Namba 6 asilia bado hakuna. Muzamilu hana anachokifanya zaidi ya kuchukua kadi zisizo na ulazima.
Na Okedjepha?Namba 6 asilia bado hakuna. Muzamilu hana anachokifanya zaidi ya kuchukua kadi zisizo na ulazima.
Ni kweli kuna uhaba wa washambuliaji Afrika na hilo niliwahi pia kulisema.Hakuna striker mkali kwny ligi za Afrika hapa beyond viwango vya hawa hawa akina baleke, mayele, mugalu, jobe nk
Mnajidanganya bure..hawapo..
Walishajiondokea Afrika wakiwa yosso siku nyingii...
Cha msingi hapa ni kuwatengeneza na kuwanoa hawa hawa akina kibu.
Kwani Chama Jr wakt anakuja Tanzania, alikuja na kiwango hiki?
Hata wewe mtoa mada tuambie huyo striker hatari yupo wapi, timu gani na anaitwa nani..huwezi kutupa jibu
Hakika nilikusoma ktk uzi huu.kabla sasa nmekuelewa nn ulichokusudia.Nadhani sasa mmeelewa kwa nini nilileta hoja hii na niliposikilizwa nikapongeza. Mpaka sasa Ateba kaifunga kila timu iliyokutana nayo na uwanja pekee ambao hajafunga goli ni ule wa Libya. Huu ndiyo ufanisi tunaoutaka kutoka kwa striker na akipata watu sahihi wa kumlisha mipira, atafunga saaana.