Mo Dewji vunja benki, tafuta striker wa maana umalize kazi uliyoianza

MCHUKUUE KIBU, MUTALE, DEBORA, NA AWESU AWESU WAWEKE KWENYE BRENDA SAGA KWA DAKIKA MOJA KISHA TIA SHABALALA NA KAPOMBE KIDOGO SAGA TENA KISHA TIA SHABALALA NA KAPOMBE SAGA TENA KISHA TIA MZAMIRU NA MUKWALA KWA MBALI SAGA KIDOGO TENA HALFU WEKA BALUA VIJIKO VIWILI NA FONDO MALONE KIJIKO KIMOJA HALFU KOROGA VIZURI NDIO UNAMPATA PROFESA WA MPIRA PACOME ZOUA ZOUA😂😂😂😂🙌🏻🙌🏻
 
Moanzu yuko wapi?
 
🤣🤣🤣
 
Namba 6 asilia bado hakuna. Muzamilu hana anachokifanya zaidi ya kuchukua kadi zisizo na ulazima.
 
Namba 6 asilia bado hakuna. Muzamilu hana anachokifanya zaidi ya kuchukua kadi zisizo na ulazima.
Mzamiru alipangwa kwa kazi maalum kuwaonyesha wachezaji wapya jinsi Derby inavyochezwa maana wakizembea watapigwa hata 10. Kuna defense line inayocheza kwa kutumia nguvu kama ya Yanga chini ya Aucho?
 
Simba tunahitaji namba 10 mnyumbulifu...

Mkwala anatosha pale mbele...

Yanga haina striker wa maana, angalia goli wanazofunga...
 
Hicho ni kikundi cha burudani, hata tajiri mwenyewe anawekeza kawaida.....
 
Hakuna striker mkali kwny ligi za Afrika hapa beyond viwango vya hawa hawa akina baleke, mayele, mugalu, jobe nk

Mnajidanganya bure..hawapo..

Walishajiondokea Afrika wakiwa yosso siku nyingii...

Cha msingi hapa ni kuwatengeneza na kuwanoa hawa hawa akina kibu.

Kwani Chama Jr wakt anakuja Tanzania, alikuja na kiwango hiki?

Hata wewe mtoa mada tuambie huyo striker hatari yupo wapi, timu gani na anaitwa nani..huwezi kutupa jibu
 
Simba hii mtawaonea tu bure washambuliaji. Hebu mtuambie kwanza kwa mechi hizi mbili wamekosa nafasi zipi za wazi. Mkubali kujenga timu. Nabi alikaa na hii Yanga miezi sita anahangaika nayo. Simba leo inataka ushindi wa haraka haraka, tena wachezaji wapya zaidi ya 10. Tutaona mengi.
 
Ni kweli kuna uhaba wa washambuliaji Afrika na hilo niliwahi pia kulisema.

Freddy mwenyewe siyo mbaya kihivyoo, shida yake ni kuwa anacheza amerelax sana, anataka magoli yamfuate yeye, haonekani kutaka kuyatafuta. Anazidiwa hata na Mzize. Haishangazi kumkuta bado anahangaika Afrika, mchezaji anayetoka taifa kubwa kisoka kama Ivory Coast na mwenye mwili kama wake.

Kanoute angebakishwa akasaidiana na Mukwala pale mbele, Freddy angebaki option ya 3 kama nafasi bado ingekuwepo. Kanoute akijengewa tu mindset ya kistriker, hakosi kukupa goli 15+ kila msimu.
 
Nadhani sasa mmeelewa kwa nini nilileta hoja hii na niliposikilizwa nikapongeza. Mpaka sasa Ateba kaifunga kila timu iliyokutana nayo na uwanja pekee ambao hajafunga goli ni ule wa Libya. Huu ndiyo ufanisi tunaoutaka kutoka kwa striker na akipata watu sahihi wa kumlisha mipira, atafunga saaana.
 
Hakika nilikusoma ktk uzi huu.kabla sasa nmekuelewa nn ulichokusudia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…