Don't make me floss son. Ali said it ain't bragging if you did it.
Mimi sitafuti mademu, mademu wananitafuta mimi.
Wakiniona haweshi kusema "Kiranga tunakuzimia". Mimi nawaambia siku hizi ni mtawa wa Ki Buddha natafsiri vitabu vya dini kama Dhammapada, sitaki mademu.
Kuepusha ngumi tu, watu wasinipiganie.
Sasa nazungusha Macao, Azores, Ibiza, Curacao, Turks and Caicos, Copa Cabana, Angkor Wat na Las Vegas, ujanja wa Sinza niliupita 1998 tulipokuwa tunafunga muziki mkubwa Checkpoint.
Enzi tuliyofunga njia ya Mpakanjia!
Hata enzi hiyo, tuliwashusha mabinti wa Kimarekani wanatoka New York, tunawaleta Sinza Uswahilini waone pelaso la Bongo.
Wengine wanafanya safari kutoka Kampala kuja Dar. Tumewashusha mabinti wa Kampala Dar kabla ya Diamond Platnumz.
Tulikuwa hatutaki local products, tuna import wasiojua Kiswahili tu.
Huko Kinondoni natoa ufadhili wa mikopo kwa watu wanaotaka kuanzisha biashara ndogondogo, halafu nawasahaulisha kunilipa makusudi kwa sababu najua vyuma vimebana.
Nimekuacha miaka 20 nyuma kwa msingi huu.