Sikutaka tabu za kina Sikudhani Kiswahili kingi , lool. Joking.
Siku moja niko kwenye gari narudi home hapo Morocco, sasa hivi ni jengo la kampuni ya simu, Airtelnafikiri, siku hizo Ambassador Hotel.
Niko na mtoto wa Kinyamwezi Kinugu kwenye gari, basi akaja machinga na bidhaa bidhaa zake anamshobokea "shangazi hii ya leo leo nzuri sana itakufaa sana".
Mtoto wa Kinugu hajui Kiswahili anacheka tuu kafurahiii anasema "But I don't understand what you are saying, Kiranga translate please".
Nikamuona Machinga mwenyewe kafunga break ananifuata mimi anashangaa shangaa tu.
Nikamwambia Mmarekani huyo hajui Kiswahili, nikamwambia yule mtoto wanataka kukuuzia mazagazaga yao hao.