Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Utendaji kazi wa Rais Magufuli ni wa ajabu kweli.
Au naweza kusema ni ambao haufuati desturi ama kawaida ya utendaji wa mambo. Ni unorthodox, kwa kimombo 😜.
Hivyo ndivyo ninavyoweza kuuelezea kwa kifupi.
Fuatana nami nikuelezee kwa nini nasema hivyo;
Nimeangalia video fupi ya hotuba aliyoitoa Dkt. Bashiru mara baada ya kuapishwa kwenye hiyo nafasi yake mpya hapo jana.
Katika hotuba yake hiyo ambayo aliitoa bila kusoma, Dkt. Bashiru alisema kuwa jioni ya siku ile aliyoteuliwa, alikuwa yupo sehemu [nahisi labda alikuwa nyumbani kwake] akisoma mafaili ya kazi zake za ukatibu mkuu wa CCM, ndo eti akapata taarifa kupitia kwenye mitandao [ya kijamii] kwamba kateuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi.
Huyu hapa Dkt. Bashiru kwa maneno yake mwenyewe:
Kwa kuokoa muda, anzia dakika ya 2:30 hadi 2:50.
Maneno hayo ya Bashiru yaliuvuta uangalifu wangu na kunifanya niwaze kidogo maana kama kumbukumbu yangu ni nzuri, hii si mara ya kwanza kwa mtu aliyeteuliwa na Rais Magufuli, kuujua uteuzi wake huo kupitia mitandao ya kijamii.
Kwa akili zangu hizi za kidato cha 4, mimi huwa nadhani kuwa Rais kabla hajamteua mtu kushika wadhifa au nafasi flani, Rais huongea na huyo mtu kwanza ili kuona kama huyo mtu yuko tayari kuyabeba majukumu ya kazi atakayo kumpa, na kuhakikisha kwamba huyo mtu anaukubali uteuzi huo kabla ya umma kufahamishwa.
Sasa kama Dkt. Bashiru alizipata taarifa za uteuzi wake huo kupitia kwenye mitandao kama tulivyozipata sisi wengine, ina maana hakukuwepo na mawasiliano kati ya mamlaka ya uteuzi na mteuliwa.
Kama hivi ndivyo ilivyo kwa utendaji wa Rais Magufuli, basi daah, sijui nisemeje tu.
Utateuaje mtu, tena wa cheo kilicho nyeti, halafu mtu huyo aujulie uteuzi huo kupitia mtandaoni?
The guy is cocking a snook at just about everything....norms, traditions, common sense, comity, presidential comportment, you name it!
Man oh man.